Scripture Stories
Sura ya 55: Mitume Wanaongoza Kanisa


Sura ya 55

Mitume Wanaongoza Kanisa

Picha
Yesu akiwafundisha Mitume

Baada ya kufufuka, Yesu alikaa na Mitume Wake kwa siku 40. Aliwafundisha mambo mengi kuhusu injili na Kanisa Lake.

Picha
Yesu akiwafundisha Mitume

Aliwaambia wafundishe injili kwa watu wote. Alisema pia kwamba punde angewaacha, lakini Roho Mtakatifu angekuja kuwasaidia.

Picha
Yesu akirudi mbinguni

Mitume walimtazama Yesu akipaa angani katika mawingu. Malaika wawili wakiwa wamevaa nguo nyeupe waliwaambia Mitume kwamba Yesu angerudi kutoka mbinguni siku moja.

Picha
Petro, Yakobo, na Yohana

Mitume walikuwa sasa viongozi wa Kanisa la Yesu Kristo duniani. Petro alikuwa Rais, na Yakobo na Yohana walikuwa washauri wake.

Picha
mtu akitawazwa na Mitume

Kulikuwa tu na Mitume kumi na mmoja—Yuda alikuwa amekufa. Baba wa Mbinguni aliwaambia Mitume wamchague Mathiya kuwa mmoja wa Mitume Kumi na Wawili. Mitume wote walikuwa na wito maalumu katika ukuhani.

Picha
watu wakisali pamoja

Mitume na wanafunzi wengine walikuwa na imani katika Bwana. Walitii amri Zake. Walipendana.

Picha
Mitume wakiwafundisha watu

Wakiwa na ukuhani na nguvu ya Roho Mtakatifu, Mitume walikuwa na uwezo wa kufanya mambo mengi. Waliwaponya wagonjwa na walikuwa wamisionari. Walifundisha kuhusu Yesu Kristo na injili Yake. Watu wengi waliamini maneno ya Mitume na kujiunga na Kanisa. Waumini wa Kanisa waliitwa Watakatifu.

Chapisha