Scripture Stories
Sura ya 17: Watu Wenye Hasira Nazareti


Sura ya 17

Watu Wenye Hasira Nazareti

Picha
Yesu akisafiri

Yesu alienda Nazareti, mji ambao Yeye alikuwa amelelewa.

Picha
Yesu akifundisha ndani ya sinagogi

Yesu alienda kwenye sinagogi, jumba ambapo Wayahudi huenda kanisani. Alisimama na kusoma kutoka kwenye maandiko. Alisoma maneno ya nabii Isaya. Isaya alikuwa amesema kwamba Mwokozi angekuja duniani na kuwasaidia watu wote.

Picha
watu wakimwangalia Yesu

Yesu alipofunga maandiko na kuketi chini, watu wote walimwangalia Yeye.

Picha
Yesu akifundisha

Yesu alisema kwamba maneno ya Isaya yalikuwa kumhusu Yeye — kwamba Yeye alikuwa Mwokozi. Watu walistaajabishwa na maneno Yake. Walisema, “Huyu siye mwana wa Yusufu?” Hawakuamini kwamba Yesu alikuwa Mwana wa Mungu.

Picha
Yesu akifundisha

Mwokozi alijua kile walichokuwa wakifikiria. Walimtaka Yeye afanye muujiza. Lakini Yesu aliwaambia kwamba asingewafanyia miujiza kwa sababu hawakuwa na imani Kwake.

Picha
Yesu na watu kwenye kilele cha mlima

Hii iliwafanya watu wawe na hasira. Walimpeleka Yesu kwenye kilele cha mlima na walitaka kumtupa chini.

Picha
Yesu akiondoka kutoka kwa watu wenye hasira

Yesu aliwatoroka na kwenda kwenye mji mwingine.

Chapisha