Scripture Stories
Sura ya 45: Senti za Mjane


Sura ya 45

Senti za Mjane

Picha
mtu akiweka pesa ndani ya sanduku

Yesu alienda hekaluni huko Yerusalemu. Alitazama watu wakitoa pesa kwa ajili ya kanisa. Watu wengi matajiri walitoa pesa nyingi.

Picha
mwanamke akiweka sarafu ndani ya sanduku

Mjane maskini alitoa vipande viwili vya pesa vilivyoitwa senti. Haikuwa pesa nyingi sana, lakini ilikuwa pesa yote ambayo alikuwa nayo.

Picha
Yesu akizungumza

Yesu alimwona mjane na akawaambia wanafunzi nini alichokuwa amefanya.

Picha
mtu akihesabu pesa

Alisema watu matajiri walikuwa wametoa kiasi kikubwa zaidi cha pesa kuliko kile mjane alichokuwa ametoa, lakini walikuwa na zaidi za kutoa.

Picha
mwanamke akiondoka hekaluni

Mjane hakuwa na pesa nyigine zaidi. Alitoa zote alizokuwa nazo. Alitoa zaidi kwa Mungu kuliko watu wote matajiri.

Chapisha