Scripture Stories
Sura ya 38: Farisayo na Mtoza Ushuru


Sura ya 38

Farisayo na Mtoza Ushuru

Picha
Yesu akizungumza na watu

Siku moja Mwokozi alizungumza na baadhi ya watu ambao walifikiri kwamba walikuwa waadilifu zaidi ya watu wengine. Yesu aliwaambia hadithi.

Picha
mtu akiwa hekaluni

Watu wawili walienda hekaluni kusali. Mmoja alikuwa Farisayo. Mwingine alikuwa mtoza ushuru, ambaye ni mkusanya kodi. Watu hawakuwapenda wakusanya kodi. Walifikiri wakusanya kodi hawakuwa waaminifu.

Picha
watu wawili wakisali

Farisayo alisimama mbele ya wengine kusali. Alimshukuru Mungu kwamba alikuwa bora kuliko watu wengine. Alisema kwamba alifunga mara mbili kila wiki na alilipa zaka yake. Mtoza ushuru alisimama peke yake, akainamisha kichwa chake, na kusali, “Mungu uniwie radhi mimi mwenye dhambi.”

Picha
Yesu akiwafundisha watu

Farisayo alifikiri alikuwa mkamilifu na hakuhitaji usaidizi wa Mungu. Lakini mtoza ushuru alijua kwamba hakuwa mkamilifu na alihitaji msaada wa Mungu. Alikuwa mnyenyekevu na alimsihi Mungu amsamehe.

Picha
Yesu akiwafundisha watu

Yesu alisema kwamba watu walipaswa wawe kama mtoza ushuru. Wasifikirie wao ni bora zaidi ya watu wengine. Wanapaswa watubu dhambi zao na kumsihi Mungu awasamehe.

Chapisha