Scripture Stories
Sura ya 26: Yesu Anamsamehe Mwanamke


Sura ya 26

Yesu Anamsamehe Mwanamke

Picha
mtu akizungumza na Yesu

Mfarisayo alimsihi Mwokozi aende nyumbani kwake na kula pamoja naye.

Picha
mwanamke amesimama mbele ya Yesu

Mwanamke ambaye alikuwa na dhambi nyingi aliishi katika mji. Alijua kwamba Yesu alikuwa anakula kwenye nyumba ya Mfarisayo yule. Alitaka kumfanyia Yesu jambo la kipekee.

Picha
mwanamke akiosha miguu ya Yesu

Alipiga magoti na kuosha miguu ya Mwokozi kwa machozi yake. Kisha akapangusa miguu Yake na nywele zake na kuibusu. Aliipaka pia mafuta yenye manukato mazuri. Mfarisayo alijua kwamba mwanamke yule alikuwa amefanya mambo mengi ambayo yalikuwa mabaya. Alifikiria kwamba Yesu hakupaswa kumkubalia mwanamke yule kumgusa.

Picha
Yesu akizungumza na mtu

Mwokozi alijua nini Mfarisayo alikuwa akifikiria. Alimwambia Mfarisayo kwamba yule mwanamke alikuwa amefanya zaidi kumhudumia kuliko Mfarisayo alivyofanya. Mfarisayo hakuwa amempa Yesu maji ya kuosha miguu Yake ama mafuta kwa ajili ya kichwa Chake, kama vile walivyokuwa wakifanyiwa wageni kwa kawaida.

Picha
Yesu akizungumza na mwanamke

Yesu alimwambia Mfarisayo kwamba dhambi za yule mwanamke zilisamehewa kwa sababu alimpenda Mwokozi na alimwamini. Yesu alimwambia yule mwanamke aende kwa amani.

Chapisha