Sura ya 61 Paulo na Sila Gerezani Msichana alikuwa na pepo ndani yake. Watu walipenda kusikiliza kile pepo lilisema kupitia yeye. Waliwalipa watu ambao msichana aliwafanyia kazi ili kusikia pepo likizungumza. Matendo ya Mitume 16:16 Wakati wowote Paulo na Sila walipopita, msichana yule aliwafuata. Alipokuwa akifanya hivyo, pepo lilizungumza. Siku moja Paulo aliliamuru pepo limtoke. Lilimtoka. Watu ambao msichana aliwafanyia kazi walikasirika. Sasa wasingeweza kupata pesa. Matendo ya Mitume 16:17–19 Watu waliwapeleka Paulo na Sila kwa viongozi wa mji. Walisema kwamba Paulo na Sila walikuwa wakisababisha matatizo. Matendo ya Mitume 16:19–22 Viongozi waliwafanya Paulo na Sila wapigwe mijeledi na kutupwa gerezani. Matendo ya Mitume 16:22–24 Usiku ule Paulo na Sila waliomba na kuimba nyimbo kwa Baba wa Mbinguni. Watu wote gerezani waliwasikia. Ghafla ardhi ilianza kutetemeka. Milango ya gereza ikafunguka. Matendo ya Mitume 16:25–26 Mlinzi aliamka na kuona milango iko wazi. Alifikiri wafungwa walikuwa wametoroka. Paulo alimwambia mlinzi asiwe na shaka. Wafungwa walikuwa wote bado wako pale. Mlinzi alipiga magoti kando ya Paulo na Sila na kuuliza jinsi anavyoweza kuokoka. Matendo ya Mitume 16:27–30 Paulo na Sila walimfundisha mlinzi na familia yake injili. Usiku ule mlinzi na familia yake walibatizwa. Matendo ya Mitume 16:31–33 Siku iliyofuata viongozi wa mji waliwaachilia Paulo na Sila. Paulo na Sila walienda mji mwingine kufanya kazi zaidi ya umisionari. Matendo ya Mitume 16:35–40