Hadithi za Maandiko
Sura ya 14: Nikodemo


Sura ya 14

Nikodemo

Nikodemo

Nikodemo alikuwa mmoja wa kikundi cha Wayahudi walioitwa Mafarisayo. Alikuwa pia ni mtawala wa Wayahudi. Mafarisayo wengi hawakuamini kwamba Yesu Kristo alikuwa ametumwa na Mungu. Lakini Nikodemo aliamini kwa sababu ya miujiza ambayo Yesu alifanya.

Yesu akizungumza na Nikodemo

Nikodemo alikuja kuongea na Mwokozi usiku mmoja. Yesu alimwambia kwamba hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kuingia ufalme wa Mungu bila kuzaliwa mara ya pili.

Nikodemo akizungumza na Yesu

Nikodemo hakuelewa. Mtu angewezaje kuzaliwa mara ya pili? Mwokozi alielezea kwamba alikuwa akizungumzia vitu vya kiroho. Ili kuzaliwa mara ya pili, mtu lazima abatizwe katika maji na apokee Roho Mtakatifu.

Yesu akizungumza

Yesu alielezea kwamba alikuwa ametumwa duniani kutusaidia sote kurudi kwa Baba wa Mbinguni. Alisema kwamba angeteseka kwa ajili ya dhambi zetu na kufa msalabani ili tuweze kuwa na uzima wa milele.

Yesu akizungumza na Nikodemo

Alisema kwamba tunahitaji kumwamini Yeye na kuchagua mema. Tukifanya kile kilicho chema, tutaishi milele katika ufalme wa Mungu.