Sura ya 34 Mvulana mwenye Pepo mchafu Siku moja mtu alimsihi Mwokozi amsaidie mwanawe. Mvulana alikuwa na pepo mchafu ndani yake. Wanafunzi walikuwa wameshajaribu kumponya mwanawe, lakini hawakuweza. Marko 9:14–18 Yesu alimwambia mtu yule amlete mwanawe Kwake. Mvulana alipokuja, pepo mchafu lilimfanya aanguke chini. Marko 9:19–20 Mwokozi aliuliza pepo lilikuwa ndani ya mvulana kwa muda gani. Baba alisema kwamba lilikuwa limekuwa ndani yake tangu alipokuwa mtoto. Marko 9:21 Yesu alisema angemponya mwanae kama baba angekuwa na imani. Baba alianza kulia. Alisema kwamba alikuwa na imani. Lakini alimsihi Yesu amsaidie awe na imani zaidi. Marko 9:23–24 Yesu aliliamuru pepo limtoke mvulana na kamwe lisimuingie tena. Pepo lilikasirika. Lilimuumiza mvulana tena. Kisha lilimtii Yesu na kutoka. Marko 9:25–26 Mvulana alikuwa kimya sana kiasi kwamba watu walisema alikuwa amekufa. Lakini Yesu alichukua mkono wake na kumsaidia kusimama. Mvulana alikuwa ameponywa. Pepo lilikuwa limeondoka. Marko 9:26–27 Baadaye wanafunzi walimuliza Yesu ni kwa nini hawakuweza kulifanya pepo limtoke mvulana. Yesu aliwaambia kwamba wakati mwingine walihitaji kufunga na kusali ili mtu aweze kuponywa. Mathayo 17:20–21; Marko 9:28–29