Scripture Stories
Sura ya 29: Yesu Anatembea juu ya Maji


Sura ya 29

Yesu Anatembea Juu ya Maji

Picha
mashua katika tufani

Baada ya kuwalisha wale 5,000, Yesu alienda juu mlimani kusali. Wanafunzi wake walichukua mashua ili kuvuka Bahari ya Galilaya. Usiku ulipofika, upepo ulianza kuvuma, na mawimbi yakapanda.

Picha
Yesu anatembea juu ya maji

Baadaye usiku sana, Yesu alikuja kuungana na wanafunzi Wake. Alikuwa akitembea juu ya maji kwenda kwenye mashua.

Picha
wanafunzi wakimwangalia Yesu kutoka kwenye mashua

Wanafunzi walimuona akiwa anatembea juu ya maji. Waliogopa. Walifikiri alikuwa pepo. Yesu aliwaita, “Ni Mimi; msiogope.”

Picha
Petro na Yesu wakitembea juu ya maji

Petro alitaka kutembea juu ya maji pia. Yesu alimwambia Petro aje Kwake. Petro alishuka kutoka kwenye mashua. Alianza kutembea juu ya maji kuelekea kwa Mwokozi.

Picha
Petro akizama

Kwa sababu upepo ulikuwa unavuma sana, Petro alishikwa na hofu. Alianza kuzama majini na akapiga kelele kwa Yesu amwokoe.

Picha
Yesu akimwokoa Petro

Mwokozi alishika mkono wa Petro. Alimwuliza Petro kwa nini hakuwa na imani zaidi.

Picha
Yesu na Petro wakielekea kwenye mashua

Wakati Yesu na Petro walipokuja kwenye mashua, tufani ilikoma. Wanafunzi wote walimuabudu Mwokozi. Walijua kwamba alikuwa Mwana wa Mungu.

Chapisha