Hadithi za Maandiko
Sura ya 44: Mwokozi Anaenda Yerusalemu


Sura ya 44

Mwokozi Anaenda Yerusalemu

watu wanne wakizungumza

Baadhi ya watu waliwaambia makuhani na Mafarisayo kwamba Yesu alikuwa amemfufua Lazaro. Mafarisayo walifikiri kwamba kila mtu angeamini katika Yesu. Walihofia kwamba hakuna mtu ambaye angewasikiliza wao.

watu wanne wakizungumza

Mafarisayo walipanga njia ya kumwua Yesu. Walimngojea aje Yerusalemu kwa ajili ya karamu ya Pasaka.

Yesu akienda Yerusalemu kwa kutumia punda

Yesu alienda Yerusalemu. Watu wengi walisikia kwamba alikuwa anakuja na walienda kumlaki. Yesu alikuja amepanda mwana-punda kuingia mjini. Nabii alikuwa ameandika kwamba Mwana wa Mungu angefanya hivyo. Watu wengi waliamini kwamba Yesu alikuwa Mwana wa Mungu. Waliweka matawi ya mitende na baadhi ya nguo zao ardhini ili apite juu yake. Walipiga kelele hosanna na kusema kwamba Yesu alikuwa mfalme wao.

watu wakizungumza

Watu wa Yerusalemu walikuja kuona nini kilichokuwa kinatokea. Waliuliza Yesu alikuwa ni nani. Watu katika umati waliwaambia kwamba Yeye alikuwa ni nabii kutoka Nazareti.

watu watatu wenye hasira

Mafarisayo walikasirika. Hawakutaka watu waamini kwamba Yesu alikuwa Mwokozi. Yesu alijua Mafarisayo walitaka kumwua.

Yesu akizungumza na wanafunzi

Yesu aliwaambia wanafunzi Wake kwamba angekufa karibuni. Angeteseka kwa ajili ya dhambi za watu wote na kisha kufa msalabani. Alikuwa Mwokozi wa ulimwengu. Hii ndiyo ilikuwa sababu ya Yeye kuja duniani.