Scripture Stories
Watu wa Kujua


Watu wa Kujua

Agripa

mfalme wa Kirumi aliyetawala Israeli. Paulo alimwambia Agripa huhusu Yesu Kristo.

Ana

mjane mwaminifu ambaye alimwona Yesu akiwa mtoto na kuwafundisha watu kwamba Yesu alikuwa Mwana wa Mungu na Mkombozi

Anania

mwanafunzi wa Yesu Kristo aliyeishi Dameski. Alimbariki Paulo na kumhudumia baada ya Paulo kupofushwa wakati wa ono.

Baba wa Mbinguni

Baba wa miili yetu ya kiroho. Sisi tunaomba Kwake.

Elisabeti

mama yake Yohana Mbatizaji

Eliya

nabii wa Agano la Kale

Gabrieli

malaika ambaye alimtembelea Mariamu na kumwambia kwamba angekuwa mama wa Yesu. Gabrieli pia alimjia Zakaria na kumwambia angekuwa na mwana ambaye angekuwa Yohana Mbatizaji.

Herode

mfalme mwovu aliyetawala Yerusalemu wakati Yesu alipozaliwa. Aliwaua watoto wote Bethlehemu kwa matumaini ya kumwua mtoto Yesu.

Isaya

nabii wa Agano la Kale ambaye aliandika kuhusu Yesu

Joseph Smith

Joseph Smith alipokuwa kijana, Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo walimtembelea. Walimwambia asijiunge na mojawapo ya makanisa ambayo yalikuwa duniani kwa sababu yote yalikuwa yamepotoka kutoka kwenye ukweli. Kupitia Joseph Smith, Kanisa la ukweli la Yesu Kristo lilirejeshwa duniani.

Kayafa

kuhani mkuu Myahudi ambaye alishiriki katika kumtia hatiani Yesu kwenye kushitakiwa Kwake

Lazaro

mtu ambaye Yesu alimfufua

Mafarisayo

viongozi wa Wayahudi. Wengi wao walimchukia Yesu na wanafunzi Wake.

Mariamu

mama yake Yesu

Mariamu and Martha

dada zake Lazaro na marafiki wa Yesu

Mariamu Magdalene

Rafiki wa Yesu na mtu wa kwanza kumwona Yesu baada ya Ufufuko Wake

Masiya

jina lingine la Yesu Kristo

Mathiya

mwanafunzi wa Yesu ambaye aliitwa kuchukua nafasi ya Yuda Iskariote kama mmoja wa Mitume Kumi na Wawili

Mungu

linaweza kuhusu Baba wa Mbinguni ama Yesu Kristo

Musa

nabii wa Agano la Kale

Mwokozi

Yesu Kristo ndiye Mwokozi. Aliteseka na kufa kwa ajili ya dhambi zetu. Kwa sababu Yake, tunaweza kusamehewa dhambi zetu, kama tukitubu, na tutaishi milele.

Nikodemo

mtawala wa Wayahudi ambaye aliamini kwamba Yesu alikuwa Mwokozi. Yesu alimfundisha Nikodemo kuhusu ubatizo.

Paulo

mtu ambaye hakuwapenda wanafunzi wa Yesu hadi alipomwona Yesu katika ono na kuongoka. Kisha alimtumikia Mungu na kuwa mmoja wa Mitume. Alijulikana pia kama Sauli.

Petro

mmoja wa Mitume Kumi na Wawili wa Yesu na Rais wa Kanisa baada ya kifo cha Yesu

Pontio Pilato

gavana Mrumi katika Yerusalemu. Wayahudi walimwambia Pilato amsulubishe Yesu, na Pilato alikubali Yesu kuuawa.

Roho Mtakatifu

mmoja wa washiriki watatu wa Uungu. Huwasaidia Yesu Kristo na Baba wa Mbinguni. Ana uwezo wa kusaidia watu kujua ukweli. Yeye ni roho na hana mwili wa nyama na mfupa.

Sauli

ona Paulo

Shetani

mwana wa kiroho wa Baba wa Mbinguni. Hakumtii Baba wa Mbinguni, hivyo alifukuzwa mbinguni. Akawa ibilisi. Shetani hujaribu kushawishi watu kufanya yale ambayo ni maovu.

Sila

mmisionari na rafiki wa Paulo

Simioni

mtu mwadilifu ambaye alimwona mtoto Yesu hekaluni huko Yerusalemu

Simoni

mtu katika Samaria. Alijaribu kununua ukuhani kutoka kwa Petro na Yohana. Walimfundisha kwamba mtu hawezi kununua ukuhani.

Stefano

kiongozi mwadilifu wa Kanisa la Yesu Kristo. Mafarisayo walimwua.

Tabitha

mwanamke mwema ambaye Petro alimfufua

Warumi

watu waliodhibiti nchi ambayo Yesu aliishi wakati wa maisha Yake

Wasamaria

Kundi la watu ambao waliishi katika nchi ambayo Yesu aliishi. Wayahudi na Wasamaria kwa kawaida hawakupendana.

Wayahudi

Waisraeli ambao walikuwa sehemu ya ufalme wa Yuda. Yesu alikuwa Myahudi.

Yairo

kiongozi Myahudi katika Kapernaumu. Yesu alimfufua binti yake.

Yakobo

mmoja wa Mitume Kumi na Wawili wa Yesu. Alikuwa mmoja wa washauri wa Petro baada ya kifo cha Yesu.

Yesu Kristo

Mwana wa Mungu na Mwokozi wa ulimwengu. Aliteseka na kufa kwa ajili ya dhambi zetu.

Yohana

mmoja wa Mitume Kumi na Wawili wa Yesu. Alikuwa mmoja wa washauri wa Petro baada ya kifo cha Yesu.

Yohana Mbatizaji

nabii aliyembatiza Yesu. Alikuwa mwana wa Zakaria na Elisabeti.

Yuda Iskariote

mmoja wa Mitume wa Yesu. Yuda alimsaliti Yesu kwa watu waovu kwa vipande 30 vya fedha.

Yusufu

Mume wa Mariamu. Yusufu aliwatunza vyema Yesu na Mariamu.

Zakaria

baba yake Yohana Mbatizaji

Chapisha