Scripture Stories
Sura ya 13: Yesu na Nyumba ya Baba Yake wa Mbinguni


Sura ya 13

Yesu na Nyumba ya Baba Yake wa Mbinguni

Picha
Yesu akiwa hekaluni

Yesu alienda hekaluni Yerusalemu. Watu wengi walikuwa huko kutoa dhabihu kwa kuua mnyama na kumchoma kwenye madhabahu. Dhabihu iliwasaidia watu kufikiria kuhusu Mwokozi, ambaye angejitoa dhabihu Mwenyewe kwa kuteseka na kufa kwa ajili yao.

Picha
watu wakiuza wanyama hekaluni

Baadhi ya watu hawakuwa na mnyama wa kutoa dhabihu. Watu waliwauzia wanyama hekaluni. Wauzaji walitaka kutengeneza pesa nyingi. Hawakufikiria kuhusu Mungu.

Picha
Yesu na muuzaji hekaluni

Yesu aliwaona watu wakiuza wanyama hekaluni. Alisema kwamba hekalu lilikuwa nyumba ya Baba wa Mbinguni, mahali patakatifu. Alisema watu hawapaswi kununua au kuuza vitu hapo.

Picha
Yesu akiwafukuza wauzaji kutoka hekaluni

Yesu alitengeneza mjeledi, akapindua meza, akatupa pesa sakafuni, na akawafanya wauzaji waondoke hekaluni. Hangewaacha wafanye vitu viovu katika nyumba ya Baba wa Mbinguni.

Chapisha