Baada ya Agano Jipya Viongozi wa Kanisa walifanya kazi kwa bidii kuwafundisha watu kuhusu Yesu Kristo. Waliwatembelea Watakatifu na kuwaandikia barua. Watu walijiunga na Kanisa katika nchi nyingi. Watu waovu hawakutaka watu waamini katika Yesu Kristo. Matendo ya Mitume 6:2–4, 7; 11:19–21 Watu waovu walitaka kubadilisha amri. Baadhi ya Watakatifu waliwasikiliza. Wengi waliacha kuamini katika Yesu na hawakutii amri Zake. Wagalatia 1:6–8; Tito 1:10–11; 1Yohana 2:18–19 Mitume na Watakatifu wengi waliuwawa. Hakuna aliyeachwa kuongoza Kanisa. Funguo za ukuhani zilichukuliwa kutoka duniani. Watu hawakuwa na manabii wa kuwaongoza. Kanisa la Yesu Kristo halikuwepo duniani tena. Mitume Petro na Paulo walikuwa wamesema haya yangetokea. Mathayo 23:34; 24:8–10; Warumi 8:36; 1 Wakorintho 4:9–13; 1 Petro 4:12; Yesu Kristo, 745–46 Mamia ya Miaka ilipita. Kulikuwa na makanisa mengi tofauti. Hakuna lolote miongoni mwao lililokuwa na Mitume ama ukuhani wa Mungu. Hakuna kanisa lolote lililokuwa Kanisa la Yesu Kristo. Lakini manabii walikuwa wamesema kwamba baada ya miaka mingi Kanisa la Yesu Kristo lingerejea duniani tena. Matendo ya Mitume 3:19–26; 2 Wathesalonike 2:1–4; 2 Timotheo 4:3–4 Mnamo 1820 mvulana aliyeitwa Joseph Smith alitaka kujua ni kanisa gani lililokuwa Kanisa la Yesu Kristo. Alienda katika msitu mdogo karibu na nyumba yao na kusali. Alimwomba Mungu amwambie kanisa gani lilikuwa sahihi. Joseph Smith—Historia ya 1:3, 5, 10, 14–15 Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo walimjia Joseph Smith. Mwokozi alimwambia Joseph asijiunge na kanisa lolote kwa sababu hakuna lolote ambalo lilikuwa Kanisa Lake. Joseph Smith—Historia ya 1:17–19 Mungu alichagua kurejesha Kanisa la Yesu Kristo duniani kupitia Joseph Smith. Mungu aliwatuma malaika kumpa Joseph Smith ukuhani. Alimsaidia Joseph kutafsiri Kitabu cha Mormoni. Mnamo Aprili 6, 1830, Kanisa la Yesu Kristo lilianzishwa duniani tena. Joseph Smith—Historia ya 1:33, 66–75 Kama vile Yesu alivyowachagua Mitume Kumi na Wawili alipokuwa duniani, Mungu alimsaidia Joseph Smith kuchagua Mitume Kumi na Wawili kumsaidia kuongoza Kanisa. Wanaume hawa walipewa nguvu ya kufundisha injili na kufanya miujiza. Mafundisho na Maagano 102:3; 107:22–23, 35 Yesu anataka kila mtu ajue kuhusu Kanisa Lake. Alimwambia Joseph Smith atume wamisionari kufundisha watu wote kuhusu Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Mafundisho na Maagano 1:18, 30 Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ni kanisa sawa na lile ambalo Yesu alianzisha alipoishi duniani. Mafundisho na Maagano 115:4