Scripture Stories
Sura ya 7: Mamajusi


Sura ya 7

Mamajusi

Picha
mamajusi wakiiona nyota mpya

Mamajusi fulani waliishi katika nchi nyingine. Walijua kile ambacho manabii walikuwa wamesema kuhusu kuzaliwa kwa Yesu. Walipoiona nyota mpya angani, walijua kwamba mfalme mpya alikuwa amezaliwa.

Picha
mamajusi wakizungumza na Mfalme Herode

Mamajusi walienda kumwona Herode, mfalme wa Wayahudi, huko Yerusalemu. Walimuuliza wapi mfalme mpya alipokuwa. Herode aliwaambia wakatafute Bethlehemu. Watakapompata mtoto wangerudi na kumwambia Herode.

Picha
mamajusi wakimtembelea mtoto Yesu

Mamajusi walienda Bethlehemu na kumpata Yesu. Walimwabudu na kumpa zawadi. Waliambiwa katika ndoto wasirudi Yerusalemu na kumwambia Herode wapi alipo mtoto. Hawakurudi.

Chapisha