Scripture Stories
Sura ya 36: Yesu Anaelezea Mafumbo Matatu


Sura ya 36

Yesu Anaelezea Mafumbo Matatu

Picha
Yesu akila na baadhi ya watu

Siku moja Yesu alikuwa akila na kuzungumza na watu ambao wengi waliwadhania kuwa wenye dhambi. Baadhi ya Mafarisayo walimuona.

Picha
watu watatu wamesimama

Mafarisayo waliamini kwamba watu wema hawapaswi kuzungumza na wenye dhambi. Walidhani kwamba Yesu hakuwa mtu mwema kwa sababu alikuwa akizungumza na wenye dhambi.

Picha
Yesu akitazama pembeni

Mwokozi alitaka kuwasaidia Mafarisayo kuelewa ni kwa nini Yeye alikuwa na wenye dhambi. Aliwaambia mafumbo matatu. La kwanza lilikuwa kuhusu kondoo aliyepotea.

Luka 15:3; Mafundisho ya Nabii Joseph Smith, 277

Chapisha