Scripture Stories
Fumbo la Pili: Sarafu Iliyopotea


Fumbo la Pili

Sarafu Iliyopotea

Picha
mwanamke akitafuta sarafu

Mwanamke alikuwa na sarafu 10 za fedha. Aliipoteza moja ya sarafu hizo. Aliitafuta kote nyumbani.

Picha
mwanamke ameshikilia sarafu

Mwishowe aliipata sharafu. Alifurahi sana. Aliwaita rafiki zake na majirani ili kuwaambia. Wao pia walifurahi kwamba alikuwa ameipata sarafu iliyopotea.

Picha
Yesu amesimama na mikono iliyonyooshwa

Viongozi wa kanisa na waumini ni kama yule mwanamke katika hadithi; sarafu iliyopotea ni kama muumini wa Kanisa ambaye haendi kanisani au hajaribu tena kuishi amri. Ni kama wamepotea kutoka Kanisani. Yesu Kristo anataka waumini wa Kanisa kuwatafuta akina kaka au dada wowote waliopotea na kuwasaidia kumrudia Yeye. Anafurahia sana wakati haya yanapotendeka.

Yesu Kristo, 455–56

Picha
kundi la watu waliovalia mavazi meupe

Marafiki na majirani katika hadithi hii ni kama malaika wa Mungu. Malaika hufurahia sana pale mtu anapotubu.

Chapisha