Scripture Stories
Maneno ya Kujua


Maneno ya Kujua

abudu

kumsifu, kumpenda na kumtii Mungu

adilifu

utiifu kwa amri za Mungu

ahadi

kusema utafanya kitu

amini

kuhisi kwamba jambo fulani ni sahihi ama la kweli

amri

kitu ambacho Mungu huwaambia watu wafanye ili wawe na furaha

amrisha

kumwambia mtu ama kitu nini cha kufanya

anzisha

kuweka katika utaratibu Kanisa la Yesu Kristo

askari

mtu ambaye hutekeleza maagizo ya mfalme ama kiongozi

baraka

sala maalumu kumuomba Baba wa Mbinguni kumfariji au kumponya mtu; mtu anayetoa sala hii hufanya hivyo kwa nguvu ya ukuhani ambao anao. Usaidizi wowote tunaopata kutoka kwa Mungu.

bariki

kutoa vitu vizuri au kumsaidia mtu

boflo [maboflo]

umbo ambao mkate huokwa

Picha
boflo
busara

mtu ambaye ana maarifa mengi na anaelewa watu, sheria na maandiko; pia mtu ambaye hupanga kwa ajili ya siku za usoni

bwana harusi

mwanaume ambaye anaoa

chagua

kuchukua ama kuteua

daima

kila mara

danganya

kutosema ukweli

dhabihu

kutoka kitu cha maana kwa ajili ya Mungu ama watu wengine

dhambi

kutotii amri za Baba wa Mbinguni

divai

kinywaji kilichotengenezwa kwa zabibu

fuata

kufanya kile ambacho mtu mwingine anafanya

fufuka

kuwa na miili yetu na roho kurudiana pamoja baada ya kufa kwetu

fumbo

hadithi ambayo hufundisha kanuni au somo

gereza

mahali ambapo watu waliovunja sheria huwekwa

harusi

tukio ambapo mwanaume na mwanamke huoana

hekalu

nyumba ya Mungu duniani; mahali pa kumwabudu Mungu; mahali patakatifu ambapo ibada takatifu hufanywa

Picha
hekalu
hori

sanduku ambamo chakula huwekwa kwa ajili ya wanyama kula

Picha
hori
iba

kuchukua kitu ambacho ni cha mtu mwingine

ibilisi

jina lingine la Shetani

imani

kuamini na kutumaini katika Yesu Kristo

inama [aliinama]

kuinamisha kichwa chini kwa heshima

Picha
kuinamisha kichwa
injili

mafundisho ya Yesu Kristo kuhusu jinsi watu wanavyopaswa kuishi ili kwamba waweze kurudi na kuishi na Baba wa Mbinguni; ni mpango wa wokovu wa Baba wa Mbinguni

jangwa

nchi ambayo ina maji kidogo sana na mimea michache au wanyama

jaribu

kujaribu kufanya mtu afanye kitu ambacho ni kibaya

jeraha

dhara baya mwilini kwa mtu

jirani

mtu anayeishi karibu na nyumba yako; mtoto yeyote wa Mungu

jiunge

kuwa sehemu ya kundi

joho

kipande cha nguo kilicho kirefu, na kinachoburuza chini ambacho huvaliwa juu ya nguo nyingine

Picha
joho
kaburi

mahali ambapo watu waliokufa huzikwa

Picha
kaburi
karamu

mlo mkubwa ambao kwa kawaida huliwa siku maalumu

kejeli

kudhihaki

kidonda

sehemu mwilini ambayo inauma ama kuvuja damu

kiongozi

mtu anayeelekeza na anawajibika kwa ajili ya kundi la watu

kipawa cha Roho Mtakatifu

haki ya kuwa na usaidizi wa Roho Mtakatifu; hupewa mtu baada ya ubatizo na mtu aliye na mamlaka ya ukuhani

kipofu

kutoweza kuona

kiziwi

kutoweza kusikia

kufunga

kuacha kula chakula na maji unapotafuta baraka kutoka kwa Baba wa Mbinguni

kugeuzwa

badiliko kwa mtu kwa muda mfupi ambalo hufanya aweze kuwa katika uwepo wa Baba wa Mbinguni

kuhani

kiongozi katika kanisa

kujazwa na Roho Mtakatifu

Kuwa na Roho Mtakatifu kujaza akili na moyo wa mtu kwa ukweli

maandiko

vitabu ambavyo vina maneno ya Mungu yanayotolewa kupitia manabii Wake

madhabahu

muundo mtukufu unaofanana na meza hekaluni wakati Yesu alipokuwa hai. Watu walitoa dhabihu kwa Mungu juu ya madhabahu.

Picha
madhabahu
mahubiri

Mazungumzo yanayotolewa kwa kundi la watu kuhusu injili

Malaika

mjumbe wa mbinguni kutoka kwa Mungu

Mamajusi

wanaume ambao walikuja kutoka Mashariki kumtembelea Yesu alipokuwa mtoto mchanga

mamlaka

haki ya kutumia nguvu kama vile ukuhani au kuwa na haki ya kuwaadhibu wale ambao hawatii sheria

mbinguni

mahali ambapo Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanaishi

mchungaji

mtu anayewatunza kondoo

Picha
mchungaji
milele

kitu ambacho hakina mwisho; kinaendelea milele

misheni

wakati maalumu wa kwenda kuhudumu na kufundisha watu injili ya Yesu Kristo na kuimarisha ufalme wa Mungu duniani

mjane

mwanamke ambaye mumewe amekufa

mjeledi

uzi au kamba nyembamba; kutumia mjeledi kupiga mtu ama kitu

Picha
mjeledi
mkoma

mtu mgonjwa mwenye vidonda mwili mzima

mlima

mlima ama kilima kikubwa

mlinzi

mtu anayewaangalia watu gerezani; kuangalia watu, sehemu, ama kitu

mmisionari

mtu ambaye huenda misheni; wakati mwingine mtu huyo huitwa kwenda nchi zingine

mpatanishi

mtu anayewasaidia watu wasikasirikiane

mshauri

mtu anayesaidia ama kutoa nasaha kwa mtu mwingine

Mtakatifu

muumini wa Kanisa la kweli la Yesu Kristo

Mtume

kiongozi katika Kanisa la Yesu Kristo ambaye humshuhudia Yesu Kristo na kufundisha injili

mtumwa

mtu anayehudumu au kumfanyia kazi mtu mwingine au Mungu

muujiza

kitu kisicho cha kawaida ambacho hutokea kwa sababu ya nguvu za Mungu

muumini

mtu ambaye yuko katika kanisa ama kikundi kingine

mvivu

kutokuwa tayari kufanya kazi

mwanafunzi

mtu anayeamini katika Yesu Kristo na anayejaribu kuwa kama Yeye

mwenye dhambi

mtu ambaye hatii amri za Baba wa Mbinguni

mwenye nyumba ya wageni

mtu ambaye anamiliki nyumba ya wageni

mwiba

sehemu kali na yenye ncha ya mmea ambayo inaweza kuumiza ikiguswa

mwili wa nyama na damu

miili ambayo watu duniani wanayo ambayo imeundwa kwa ngozi, mifupa, misuli, na damu

mwizi [wezi]

mtu ambaye huiba kutoka kwa wengine

mwovu

mtu ambaye ni mwovu

mzabibu

shina kuu la mmea, kama vile zabibu, ambalo lina matawi yanayozunguka yatokanayo na mmea huo. mzabibu huyaweka matawi hai

Picha
mzabibu
nabii

mtu aliyeitwa na Mungu kuwaambia watu kile Mungu anawataka wafanye

nguvu

uwezo wa kufanya kitu fulani. Pia ona ukuhani.

njaa

ukosefu wa chakula kwa sababu hakuna cha kutosha kulisha kila mtu

nyika

mahali ambapo hakuna miji ama vijiji na watu wachache wanaishi hapo

nyumba ya wageni

mahali ambapo watu wanaweza kula na kulala wakati wakiwa safarini

nzige

mdudu mkubwa anayeruka wakati mwingine hutumika kama chakula

Picha
nzige
okoa

kukomboa kutoka kwenye hatari. Yesu alikufa ili kutuokoa kutokana na kifo cha kimwili na hatari za dhambi.

ongoza

kuwaongoza wengine

ono

aina ya ufunuo kutoka kwa Baba wa Mbinguni

pango

shimo katika upande wa mlima

Picha
pango
Pasaka

sherehe maalumu ambapo Wayahudi hukumbuka jinsi Mungu alivyowaokoa watu wao kutoka kwa Wamisri wakati wa Musa

piga magoti [kupiga magoti]

kwenda chini kwa magoti yako

Picha
Kupiga magoti
ponya

kufanya mtu aliye mgonjwa ama aliye umia kuwa mzima

roho

mmoja wa watoto wa Baba wa Mbinguni ambaye hana mwili wa nyama na mifupa

Sabato

siku maalumu ya wiki ambapo watu humwabudu Mungu kwa kwenda kanisani na kujifunza zaidi kuhusu Yeye

safiri

kwenda kutoka sehemu moja hadi nyingine

sakramenti

ibada ambapo mkate na maji hubarikiwa na kupewa waumini wa Kanisa ili kuwakumbusha juu ya Yesu Kristo na kutii amri. Ibada hiyo hufanywa na wanaume ambao wana ukuhani.

sala

yale yanayosemwa wakati mtu anaposali

sali

kuzungumza na Mungu, ukimpa shukrani na kuomba baraka

saliti

kumgeuka rafiki au kumkabithi kwa adui

samehe

kuacha kumkasirikia mtu ambaye amefanya vitu vibaya au vya kudhuru

sarafu

kipande cha pesa, kilicho bapa

Picha
sarafu
sega la asali

vyumba vya nta vilivyotengenezwa na nyuki. Nyuki hujaza vyumba hivi vya nta kwa asali.

Picha
sega la asali
sherehekea

kukumbuka siku muhimu kwa kufanya kitu maalumu

shitaka

tukio ambapo watu hujaribu kuthibitisha ikiwa mtu amevunja sheria au la

shuhudia

kuwaambia watu wengine kwamba tunajua kitu fulani ni cha kweli

sifu

kusema mambo mazuri kuhusu mtu fulani

sinagogi

jengo ambapo Wayahudi hukutana ili kumwabudu Mungu

sulubisha

kuua mtu kwa kumning’iniza kwenye msalaba wa mbao kama walivyomfanyia Yesu Kristo

tafsiri

kubadilisha maneno yaliyoandikwa ama kuzungumzwa katika lugha moja kwenye maneno yaliyo na maana sawa katika lugha tofauti

taji ya miiba

miiba mikali iliyopangwa kwa duara iliyowekwa kichwani kwa Yesu

Picha
taji ya miiba
takatifu

kitu ambacho ni halisi na kisafi na kilichotengwa kwa ajili ya matumizi ya Mungu

takatifu

chochote kilichotolewa kwetu na Mungu ambacho ni cha kuheshimiwa na kustahiwa

tawaza

wanaume ambao wana ukuhani wanaweka mikono yao juu ya kichwa cha mwanaume mwingine ili kumpa nguvu na mamlaka ya ukuhani

Picha
utawazo
teka [tekwa]

kuchukua nchi ama mtu kwa nguvu

teseka

kuhisi uchungu mwingi

tetemeko la ardhi

mtetemo wa nguvu sana wa ardhi

tii

kufanya kile ambacho kinatakiwa au kuamriwa

tubu

kuhisi huzuni kwa jambo ulilofanya na kuahidi kamwe kutolirudia tena

ubatizo [batiza]

ibada ama utaratibu ambapo mtu mwenye mamlaka ya ukuhani kutoka kwa Mungu anamweka mtu mwingine ndani kabisa ya maji na kumwinua kutoka kwenye maji. Ubatizo unahitajika ili kuwa muumini wa Kanisa la Yesu Kristo. Pia ona Kipawa cha Roho Mtakatifu.

Picha
ubatizo
ufalme wa Mungu

Kanisa ama mahali ambapo waadilifu wataishi na Baba wa Mbinguni baada ya maisha haya

ufunuo

kitu Mungu huwaambia watu Wake

Ujio wa Pili

wakati Yesu atakaporudi duniani tena ili kuokoa watu waadilifu na kuwaangamiza waovu

ukuhani

mamlaka ya kutenda katika jina la Mungu

ukweli

kile ambacho ni cha kweli na sahihi

uovu

kitu ambacho ni kibaya na hakitoki kwa Mungu

ushuhuda

hisia ama wazo kutoka kwa Roho Mtakatifu kwamba injili ni ya kweli

ushuru

pesa ambazo watu hulipa serikalini

uzima wa milele

kuwa kama Baba wa Mbinguni na kuishi Naye milele

vita

mapigano kati ya maadui

wimbo

wimbo wa kanisa ama wimbo unaomtukuza Mungu

wokovu

kuokolewa kutokana na dhambi na kifo ili tuweze kuishi na Baba wa Mbinguni tena

zaa

kutengeneza ama kukuza kitu

zaka

pesa ambayo hutolewa kwa Mungu ili kujenga Kanisa Lake

zama

kufa kwa kuwa majini kwa muda mrefu sana

zawadi

kitu kizuri ambacho Mungu ama wengine hutupatia

zika [zikwa]

kuweka mwili wa mtu aliyekufa katika kaburi au ardhini na kufunika kwa udongo; kuweka kitu fulani ardhini ambacho mtu anataka kuficha

Chapisha