Scripture Stories
Sura ya 60: Petro Anamfufua Tabitha


Sura ya 60

Petro Anamfufua Tabitha

Picha
mwanamke akisaidia watu

Mwanamke mwema aliyeitwa Tabitha aliishi katika mji wa Yafa. Alikuwa mfuasi wa Yesu Kristo. Aliwasaidia watu wengi na kufanya mambo mengi mema.

Picha
watu wakilia pembeni mwa kitanda cha mwanamke

Alikuwa mgonjwa na akafa.

Picha
Petro pembeni mwa kitanda cha mwanamke

Rafiki zake walimwita Petro. Alipofika pale, aliwaomba rafiki za Tabitha waondoke chumbani.

Picha
Petro akimsaidia mwanamke kukaa vizuri

Petro alipiga magoti na kuomba, kisha akamwambia Tabitha asimame. Alifungua macho yake na alikaa vizuri.

Picha
Petro akimsaidia mwanamke kutembea

Petro alimsaidia kusimama. Aliwaita rafiki zake. Walikuja na kuona kwamba alikuwa hai. Petro alikuwa ametumia nguvu ya ukuhani kumfufua Tabitha. Watu wengi huko Yafa waliamini katika Yesu Kristo pale walipogundua juu ya ufufuo wa Tabitha.

Chapisha