Sura ya 18 Yesu Anachagua Mitume Wake Siku moja Yesu aliwafundisha watu kutoka kwenye mashua kwenye ufukwe wa Bahari ya Galilaya. Mashua ilikuwa ni ya Mtu aliyeitwa Petro. Luka 5:1–3 Petro na rafiki zake walikuwa wamevua samaki usiku mzima bila ya kushika samaki wowote. Baada ya Yesu kumaliza kufundisha, Alimwambia Petro apeleke mashua kilindini. Kisha akamwambia Petro na rafiki zake washushe nyavu zao za kuvua majini. Luka 5:4–5 Walivua samaki wengi sana hadi nyavu zao zikaanza kukatika. Luka 5:6 Petro aliwaita rafiki zake katika mashua nyingine kuja kuwasaidia. Samaki walijaza mashua zote mbili kiasi kwamba zikaanza kuzama. Luka 5:7 Petro na rafiki zake walishangaa. Walijua kwamba Yesu Kristo alikuwa amefanya hili litendeke. Luka 5:8–9 Petro alipiga magoti kwenye miguu ya Mwokozi. Alisema kwamba hakustahili kuwa karibu na Yesu. Yesu alimwambia Petro asiwe na hofu. Luka 5:8–10 Marafiki wawili wa Petro, Yakobo na Yohana, walikuwa ndugu. Yesu aliwaambia Petro, Yakobo na Yohana wamfuate na wawe “wavuvi wa watu.” Wanaume hao waliacha kila kitu walichokuwa nacho na kwenda pamoja na Yesu. Mwokozi pia aliwaambia wanaume wengine wamfuate Yeye. Mathayo 4:18–22; 9:9; Luka 5:10–11; Yohana 1:35–51 Yesu aliwachagua Mitume kumi na wawili waongoze Kanisa Lake. Aliomba usiku mzima ili kwamba angeweza kuchagua wanaume wanaofaa. Asubuhi iliyofuata alichagua na kuwatawaza wanaume kumi na wawili, akiwapa ukuhani na mamlaka ya kuwa Mitume. Marko 3:14; Luka 6:12–16; Yohana 15:16 Mitume walisafiri kwenda miji mingi. Walifundisha injili na kuwaponya watu. Walirudi kumwambia Yesu kile walichokuwa wamefanya. Marko 6:30; Luka 9:1–6