Scripture Stories
Sura ya 24: Binti wa Yairo Anafufuliwa kutoka Wafu


Sura ya 24

Binti wa Yairo Anafufuliwa kutoka Wafu

Picha
mtu amepiga magoti

Siku moja Yairo, mtawala wa sinagogi, alianguka miguuni pa Mwokozi.

Picha
mtu akimwomba Yesu msaada

Yairo alisema kwamba binti yake wa miaka 12 alikuwa mgonjwa sana. Alimuomba Yesu aende na kumbariki. Aliamini kwamba Yesu angemponya.

Picha
Yesu akizungumza na mwanamke

Yesu alianza kumfuata Yairo nyumbani, lakini alisimama ili kumponya mwanamke. Alipokuwa akiongea naye, mtu alikuja kumwambia Yairo kwamba alikuwa amechelewa sana—bintiye alikuwa amekufa.

Picha
Yesu akizungumza na mtu

Yesu alisikia kile kilichosemwa. Alimwambia Yairo asiwe na hofu lakini amuamini Yeye.

Picha
watu wakilia

Kisha Yesu akaenda na Yairo nyumbani kwake. Nyumba ilikuwa imejaa watu ambao walikuwa wakilia kwa sababu ya kifo cha msichana huyo mdogo.

Picha
watu wakimcheka Yesu

Yesu aliwaambia kwamba msichana hakuwa amekufa ila alikuwa amelala. Watu walimcheka. Walikuwa na uhakika msichana alikuwa amekufa.

Picha
watu pembeni ya kitanda cha msichana

Mwokozi alitaka kila mtu aondoke ndani ya nyumba isipokuwa wanafunzi Wake, Yairo na mkewe Yairo. Walienda chumbani ambako msichana huyo mdogo alikuwa amelala.

Picha
Yesu akimponya msichana

Yesu alimshika msichana kwa mkono. Alimwambia aamke. Alisimama na kutembea. Wazazi wake walishangaa. Yesu aliwaambia wasimwambie yeyote kile kilichotokea. Kisha Yeye aliwaambia wazazi wake wampe msichana kitu cha kula.

Chapisha