Fumbo la Kwanza
Kondoo Aliyepotea
Mchungaji mwema alikuwa na kondoo 100. Mmoja wao alikuwa amepotea.
Mchungaji aliwaacha wale kondoo 99 kumtafuta yule mmoja aliyepotea. Alipompata, alikuwa na furaha sana.
Mchungaji alimbeba kondoo kumleta nyumbani. Aliwaita rafiki zake wote na majirani waje na kufurahia pamoja naye. Alikuwa amempata kondoo aliyepotea.
Yesu Kristo aliwaambia Mafarisayo kile ambacho fumbo lilimaanisha. Alisema kwamba wale wanaotenda dhambi ni kama kondoo aliyepotea.
Kama vile mchungaji alivyotaka kumuokoa kondoo aliyepotea, Yesu anataka kuwaokoa wale wanaotenda dhambi.
Yesu alisema kwamba hiyo ndiyo sababu alikuwa akizungumza na wenye dhambi.
Mathayo 18:11 (ona rejeo chini ya ukurasa 11c); Marko 2:17
Na kama vile mchungaji alivyokuwa na furaha alipompata kondoo aliyepotea, Yesu hufurahia pale tunapotubu.