Mafundisho na Maagano 2021
Machi 1–7. Mafundisho na Maagano 20–22: “Kuinuka kwa Kanisa la Kirsto”


“Machi 1–7. Mafundisho na Maagano 20–22: ‘ Kuinuka kwa Kanisa la Kristo,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Machi 1–7. Mafundisho na Maagano 20-22,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021

Picha
Nyumba ya Peter Whitmer

Nyumba ya Peter Whitmer, na Al Rounds

Machi 1–7

Mafundisho na Maagano 20–22

“Kuinuka kwa Kanisa la Kirsto”

Unaposoma Mafundisho na Maagano 20–22, kuwa wazi kwa misukumo ya Roho Mtakatifu. Fikiria kuuandika ili uweze kuurejelea.

Andika Misukumo Yako

Kazi ya Nabii Joseph Smith ya kutafsiri Kitabu cha Mormoni sasa ilikuwa imekamilika. Lakini kazi ya Urejesho ndio kwanza ilikuwa imeanza. Ilikuwa wazi kutoka funuo za mwanzo kwamba kwa kuongezea kwenye kurejesha mafundisho na mamlaka ya ukuhani, Bwana alitaka kurejesha mpangilio wa awali—Kanisa Lake (ona Mafundisho na Maagano 10:53; 18:5). Kwa hiyo Aprili 6, 1830, zaidi ya waumini 40 walisongamana kwenye nyumba ya magogo ya familia ya Whitmer iliyokuwa Fayette, New York, kushuhudia kuanzishwa kwa Kanisa la Yesu Kristo.

Bado, baadhi ya watu wanajiuliza, kwa nini Kanisa lenye mpangilio ni muhimu? Jibu linaweza kupatikana, angalau kwa sehemu, katika funuo zinazohusiana na mkutano ule wa Kanisa wa kwanza mnamo mwaka 1830. Hapa, baraka zinaelezwa ambazo zisingewezekana kama Kanisa la Yesu Kristo la kweli lisingekuwa “kama kawaida limeundwa na kuanzishwa” katika siku za mwisho (Mafundisho na Maagano 20:1).

Ona pia Watakatifu, 1:84–86, na “Lijengeni Kanisa Langu,” Funuo katika Muktadha, 29–32.

Picha
ikoni ya kujifunza kibinafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi

Mafundisho na Maagano 20:1–36

Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho limejengwa kwenye mafundisho ya Kweli.

Sehemu ya 20 imewasilishwa kama “ufunuo juu ya mfumo na utawala wa Kanisa” (kichwa cha habari cha sehemu). Lakini kabla ya kutoa muhtasari wa sera za Kanisa, ofisi za ukuhani, na taratibu kwa ajili ya kufanya ibada, ufunuo huu unaanza na kufundisha mafundisho ya msingi. Unaposoma mistari 36 ya kwanza ya ufunuo huu, jiulize mwenyewe kwa nini hiyo inaweza kuwa. Unaweza pia kutengeneza orodha ya kweli za injili unazopata. Hapa kuna baadhi ya mifano:

Kwa nini kweli hizi ziwe muhimu kusisitizwa wakati Kanisa lilipokuwa linaanzishwa?

Mafundisho na Maagano 20:37, 75–79

Ibada takatifu ni sehemu muhimu ya Kanisa la urejesho.

Wakati Kanisa lilipoanzishwa, Bwana aliwafundisha Watakatifu Wake kuhusu ibada takatifu, ikijumuisha ubatizo na sakramenti. Unaposoma maelekezo “kuhusiana na jinsi ya ubatizo” katika mstari wa 37, fikiria kuhusu ubatizo wako wewe mwenyewe. Je, ulipata hisia zozote zilizoelezwa katika mstari huu? Je, unazo sasa? Tafakari kile unachoweza kufanya kutunza msisimko wako wa “dhamira ya kumtumikia [Yesu Kristo] hadi mwisho.”

Unaposoma kuhusu Sakramenti katika Mafundisho na Maagano 20:75–79, jaribu kusoma sala hizi takatifu katika mtazamo wa mtu fulani anayezisikiliza kwa mara ya kwanza. Ni umaizi gani unaopokea kuhusu sakramenti? Kuhusu wewe mwenyewe? Ni kwa jinsi gani umaizi huu unaathiri jinsi unavyojiandaa kushiriki sakramenti wiki hii?

Picha
shemasi akipitisha Sakramenti

Sakramenti ni ibada takatifu.

Mafundisho na Maagano 20:38–60.

Huduma ya Ukuhani inabariki waumini wa Kanisa na familia zao.

Kama mtu angekutaka kuzitaja kazi za mwenye ukuhani, ungesema nini? Soma Mafundisho na Maagano 20:38–60, ambayo inaorodhesha kazi mbali mbali za ofisi za ukuhani. Je, kuna chochote katika mistari hii kinachobadili jinsi unavyofikiria kuhusu kazi za ukuhani na jinsi Mwokozi anavyofanya kazi Zake? Ni kwa jinsi gani umebarikiwa na kazi iliyoelezwa katika mistari hii?

Kujifunza kuhusu jinsi wanawake wanavyotumia mamlaka ya ukuhani katika kazi za Kanisa, ona Dallin H. Oaks, “Funguo na Mamlaka ya Ukuhani,” Ensign au Liahona, Mei 2014, 49–52.

Mafundisho na Maagano 21

Kanisa la Yesu Kristo linaongozwa na nabii anayeishi.

Unajifunza nini kutoka Mafundisho na Maagano 21: 4–9 kuhusu maneno ya manabii wa Bwana? Fikiria ahadi zilizoelezwa katika mstari wa 6 kwa ajili ya wale wanaopokea maneno ya Bwana kupitia nabii Wake. Ahadi hizi zina maana gani kwako?

Unawezaje kupokea neno la nabii anayeishi “kama vile linatoka kinywani mwa [Mungu]”? (mstari wa 5). Ni ushauri gani nabii wa leo ametoa ambao ungeweza kuongoza kwenye baraka zilizoahidiwa katika mstari wa 6?

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani

Mafundisho na Maagano 20.Ungesema nini kama mtu fulani angetuuliza kwa nini tunahitaji Kanisa? Majibu gani tunayapata katika Mafundisho na Maagano 20? Ona pia D. Todd Christofferson, “Kwanini Kanisa,” Ensign au Liahona, Nov. 2015, 108–11.

Mafundisho na Maagano 20:69.Ina maana gani “[kuenenda] katika utakatifu mbele za Bwana”? Inaweza kuwa burudani kwa ajili ya wanafamilia kuchora au kuandika kwenye vipande vya karatasi mambo fulani ambayo yangeweza kuwasaidia kuenenda katika utakatifu au mambo ambayo yangewazuia wasifanye hivyo. Kisha wangeweza kutengeneza njia wakitumia karatasi na kujaribu kutembea kwenye njia, wakikanyaga tu kwenye michoro ambayo itawaleta kwa Kristo.

Mafundisho na Maagano 20:37, 71–74.Kama mtu fulani katika familia yako bado hajabatizwa, mistari hii ingeweza kuongoza kwenye majadiliano kuhusu jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya ubatizo (ona mstari wa 37) na jinsi ubatizo unavyofanywa (ona Mstari wa 71–74)). Wanafamilia wanaweza kushiriki picha au kumbukumbu kutoka siku yao ya ubatizo.

Mafundisho na Maagano 20:75–79.Ni kwa jinsi gani familia yako ingeweza kutumia mistari hii kujiandaa kwa ajili ya uzoefu wenye maana, wa unyenyekevu wa sakramenti? Mistari hii inaweza kupendekeza mambo ambayo ungeweza kutafakari wakati wa sakramenti, na wanafamilia wangeweza kupata au kuchora picha za mambo hayo. Kama inafaa, unaweza kuleta picha hizi kwenye mkutano wako wa sakramenti unaofuata kama kumbukumbu ya nini cha kufikiria wakati wa sakramenti.

Mafundisho na Maagano 21:4–7.Fikiria kuwaalika wanafamilia kutafuta maneno na virai katika mstari wa 4–5 ambavyo vinatufundisha kuhusu kumfuata nabii wa Bwana. Inamaanisha nini kupokea maneno ya nabii kwa subira? katika imani? Lini tumepokea baraka zilizoahidiwa katika mstari wa 6?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “The Church of Jesus Christ,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto,77.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Iga Maisha ya Mwokozi. “Nguvu za Mwokozi za kufundisha na kuwainua wengine zilikuja kutokana na jinsi alivyoishi na aina ya mtu Aliyekuwa. Kadiri unavyojitahidi kwa bidii kuishi kama Yesu Kristo, ndivyo utakavyoweza zaidi kufundisha kama Yeye” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 13).

Picha
Oliver Cowdery akimtawaza Joseph Smith,

Oliver Cowdery Akimtawaza Joseph Smith, na Walter Rane

Chapisha