Mafundisho na Maagano 2021
Machi 22–28. Mafundisho na Maagano 29: “Yesu Kristo Atawakusanya Watu Wake”


“Machi 22–28. Mafundisho na Maagano 29: ‘Yesu Kristo Atawakusanya Watu Wake,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Machi 22–28. Mafundisho na Maagano 29,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021

Picha
Yesu amesimama mbele ya watu waliopiga magoti

Kila Goti Litapigwa na J. Kirk Richards

Machi 22–28

Mafundisho na Maagano 29

Yesu Kristo Atawakusanya Watu Wake

Mojawapo ya madhumuni ya kusoma maandiko ni kujifunza mafundisho, au kweli za injili ambazo ni muhimu kwa ajili ya wokovu wetu. Unaposoma Mafundisho na Maagano 29 wiki hii, tafuta umaizi wa kimafundisho ambao una maana kwako.

Andika Misukumo Yako

Japokuwa Kanisa la Yesu Kristo lilikuwa limeanzishwa mnamo mwaka 1830, kweli nyingi za injili zilikuwa bado kufunuliwa, na baadhi ya waumuni wa Kanisa wa mwanzo walikuwa na maswali. Walikuwa wamesoma unabii katika Kitabu cha Mormoni kuhusu mkusanyiko wa Israeli na ujenzi wa Sayuni (ona 3 Nefi 21). Ni kwa jinsi gani hili lingetokea? Funuo Hiram Page alizodai kuzipokea zilielezea mada hiyo, ambayo iliongeza tu udadisi wa waumini (ona Mafundisho na Maagano 28). Watu wengine walijiuliza kuhusu Anguko la Adamu na Hawa na kifo cha kiroho. Bwana alikaribisha maswali haya mwaka 1830: “Lolote mtakaloomba katika imani,” Aliwaambia Watakatifu, “mkiwa mmeungana katika sala kulingana na amri yangu, mtapata” (Mafundisho na Maagano 29:6). Na anakaribisha maswali yetu leo; Yeye anangojea sisi tumuulize katika sala. Kwa kweli, kama ufunuo uliojaa mafundisho katika Mafundisho na Maagano 29 unavyoonesha, wakati mwingine anajibu kwa kutoa ukweli na ufahamu zaidi ya maswali tunayouliza kwanza kabisa.

Picha
ikoni ya kujifunza kibinafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi

Mafundisho na Maagano 29

Baba wa Mbinguni aliandaa mpango madhubuti kwa ajili ya kuinuliwa kwetu.

Mafundisho na Maagano 29 inafundisha kweli nyingi kuhusu mpango wa Mungu kwa ajili ya watoto Wake. Unaposoma, tafuta kweli unazojifunza kuhusu kila moja ya sehemu zifuatazo za mpango:

Ni umaizi gani mpya ulioupata? Ni kwa jinsi gani maisha yako yangekuwa tofauti kama usingejua kuhusu kweli hizi?

Unaweza kujifunza zaidi kuhusu mpango wa Baba wa Mbinguni katika “Mpango wa Wokovu” (Preach My Gospel: A Guide to Missionary , Service rev. ed. [2018], ChurchofJesusChrist.org/manual/missionary).

Mafundisho na Maagano 29:1–8

Yesu Kristo atawakusanya watu Wake kabla ya Ujio Wake wa Pili.

Yesu Kristo anazungumzia juu ya kuwakusanya watu Wake “kama kuku avikusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake” (Mafundisho na Maagano 29:2). Picha hii inakufundisha nini kuhusu shauku ya Mwokozi kukukusanya wewe? Unaposoma Mafundisho na Maagano 29:1–8, tafuta umaizi kuhusu kwa nini tunakusanyika, nani watakusanyika, na jinsi tunavyoweza kusaidia kukusanya “wateule” (mstari wa 7).

Katika siku ya leo, kukusanyika Sayuni kunamaanisha kuunganika katika vigingi vya Sayuni ulimwenguni kote. Ni kwa jinsi gani kukusanyika kama Watakatifu kunatusaidia “kujitayarisha katika mambo yote” kwa ajili ya taabu ambazo zitakuja kabla ya ujio wa pili wa Mwokozi? (mstari wa 8; ona pia mstari wa 14–28).

Ona pia Makala ya Imani 1:10; Russell M. Nelson na Wendy W. Nelson, “Hope of Israel” (vijana WSM ulimwenguni kote, Juni 3, 2018, ChurchofJesusChrist.org).

Picha
kuku na vifaranga

Ni Mara Ngapi, na Liz Lemon Swindle

Mafundisho na Maagano 29:31–35

“Mambo yote kwangu ni ya kiroho.”

Ni katika mantiki ipi amri zote ni za Kiroho? Kujua kwamba amri zote ni za kiroho kunakufundisha nini kuhusu kusudi la amri? Unaweza kuorodhesha amri chache na kufikiria kanuni za kiroho zinazohusiana na kila moja.

Nini kinaweza kubadilika kama ungetafuta maana ya kiroho au kusudi la kiroho katika kazi zako za kila siku, hata zile ambazo zinaonekana za kimwili au kidunia?

(Ona pia Warumi 8:6; 1 Nefi 15:30–32.

Mafundisho na Maagano 29:36–50

Yesu Kristo anatukomboa kutoka kwenye Anguko.

Ufunuo huu unaanza na Bwana akijitambulisha mwenyewe kama Mkombozi, aliyefanya “upatanisho kwa ajili ya dhambi [zetu]” (mstari wa 1). Ufunuo unaendelea kuelezea baadhi ya sababu za sisi kuhitaji Mkombozi. Fikiria jinsi ambavyo ungetumia Mstari wa 36–50 kuelezea kwa nini tunahitaji ukombozi kupitia Mwokozi Yesu Kristo. Katika desturi nyingi za imani, Anguko linaonekana kama janga; unapata nini katika mistari hii kinachofundisha matokeo chanya ya Anguko? (Ona pia 1 Wakorintho 15:22; 2 Nefi 2:6–8, 15–29; Mosia 3:1–19; Musa 5:9–12.)

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani

Mafundisho na Maagano 29.Ungeweza kutumia picha mwishoni mwa muhtasari huu pamoja na Mafundisho na Maagano 29 kufundisha familia yako kuhusu mpango wa wokovu. Kwa mfano, wanafamilia wangeweza kujifunza kuhusu sehemu tofauti za mpango kwa kusoma na kujadili mistari iliyopendekezwa. Wangeweza kupata kweli za ziada katika mada za injili (topics.ChurchofJesusChrist.org) au Mwongozo kwenye Maandiko (scriptures.ChurchofJesusChrist.org). Andika kile unachojifunza. Kwa nini tuna shukrani kujua kuhusu mpango wa wokovu? Ni kwa jinsi gani kujua kuuhusu kunaathiri maisha yetu ya kila siku?

Mafundisho na Maagano 29:2, 7–8.Inamaanisha nini kukusanywa na Mwokozi? Ni kwa jinsi gani tunaweza kumsaidia Yeye kukusanya wateule?

Mafundisho na Maagano 29:3–5.Tunajifunza nini kuhusu Mwokozi katika mistari hii kinachotusaidia “kuinua mioyo [yetu] na kuwa na furaha”? (mstari wa 5). Video “Tunaweza kupata furaha” (ChurchofJesusChrist.org) ingeweza kuwasaidia kujadili jinsi kujua kuhusu mpango wa wokovu kulivyoiletea familia yako furaha.

Mafundisho na Maagano 29:34–35.Kusoma mistari hii kungeweza kuipa familia yako fursa kuzungumza kuhusu sababu za kiroho nyuma ya baadhi ya amri au ushauri wa kinabii unaojaribu kuufuata. Kwa mfano, kwa nini Bwana anatutaka tusome maandiko kama familia? Ni faida gani za kiroho tulizoziona kutokana na kutii amri?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “Israel, Israel, God Is Calling,” Nyimbo za Kanisa, na. 7.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Mtafute Yesu Kristo. Maandiko yanatufundisha kwamba vyote vilivyoumbwa na Mungu vinamshuhudia Yesu Kristo (ona Musa 6:62–63), kwa hivyo mtafute unaposoma maandiko haya. Fikiria kuandika au kuwekea alama mistari ambayo inafundisha kumhusu Yeye.

Chapisha