“Machi 29–Aprili 4. Pasaka: “Mimi Ni Yeye Aliye Hai, Mimi ni Yule Aliyeuawa,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)
“Machi 29–Aprili 4. Pasaka,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021
Machi 29–Aprili 4
Pasaka
“Mimi Ni Yeye Aliye Hai, Mimi ni Yule Aliyeuawa”
Unapojiandaa kusherehekea Kufufuka kwa Mwokozi Jumapili ya Pasaka, tafakari jinsi ufunuo wa siku hizi ulivyoongeza imani yako kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Pekee wa Mungu na Mkombozi wa ulimwengu.
Andika Misukumo Yako
Aprili 3, 1836 ilikuwa Jumapili ya Pasaka. Baada ya kusaidia kuhudumia sakramenti kwa Watakatifu waliokusanyika katika Hekalu la Kirtland lililokuwa limewekwa wakfu karibuni, Joseph Smith na Oliver Cowdery walipata sehemu tulivu nyuma ya pazia katika hekalu na waliinamisha vichwa vyao katika sala ya kimya. Kisha, kwenye siku hii takatifu wakati Wakristo kila sehemu walikuwa wanasherehekea Kufufuka kwa Yesu Kristo, Mwokozi mfufuka mwenyewe alitokea katika hekalu Lake, akitangaza, “Mimi ni yeye aliye hai, Mimi ni yule aliyeuawa” (Mafundisho na Maagano 110:4).
Inamaanisha nini kusema kwamba Yesu Kristo ni “ni yeye aliye hai”? Haimaanishi tu kwamba aliinuka kutoka kaburini siku ya tatu na kuonekana kwa wafuasi Wake wa Galilaya. Inamaanisha kwamba anaishi leo. Anazungumza kupitia manabii leo. Analiongoza Kanisa Lake hivi leo. Anaponya nafsi zilizojeruhiwa na mioyo iliyovunjika leo. Kwa hiyo tunaweza kurudia maneno ya Joseph Smith yenye ushuhuda wenye nguvu: “Baada ya shuhuda nyingi ambazo zimetolewa juu Yake, huu ni ushuhuda … ambao tunatoa juu yake: Kwamba yu hai! ” (Mafundisho na Maagano 76:22). Tunaweza kusikia sauti Yake katika funuo hizi. Tunaweza kushuhudia mkono wake katika maisha yetu. Na tunaweza kila mmoja wetu kuhisi “furaha sentensi hii inayotoa: ‘Najua kwamba Mkombozi Wangu yu Hai!’ ” (Nyimbo za Kanisa, na. 136).
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi
Mafundisho na Maagano 29.5; 38:7; 62.1; 76:11–14, 20–24; 110:1–10
Yesu Kristo yu hai.
Nabii Joseph Smith alimwona Mwokozi aliyefufuka mara kadhaa, na mara mbili za uzoefu huu zimeandikwa katika Mafundisho na Maagano. Unaposoma sehemu ya 76:11–14, 20–24; 110–10, nini kinakuvutia kuhusu Ushuhuda wa Joseph Smith? Kwa nini ushuhuda wake ni wa thamani kwako?
Kote katika Mafundisho na Maagano, Mwokozi alitoa ushahidi wa misheni Yake na utukufu Wake. Unajifunza nini kuhusu Kristo aliye hai kutokana na maneno Yake katika Mafundisho na Maagano 29:5.; 38:7; 62:1? Unaweza kufikiria kuandika matangazo kama haya ambayo unapata unapojifunza Mafundisho na Maagano.
ona pia Joseph Smith—Historia ya 1:17.
Mafundisho na Maagano 29:26–27; 42:45–46; 63:49.; 88:14–17, 27–31; 93:33–34
Kwa sababu ya Yesu Kristo, nitafufuka.
Joseph Smith alijua jinsi inavyokuwa kuomboleza kifo cha wapendwa. Wawili kati ya ndugu zake, Alvin, na Don Carlos, walikufa wakiwa vijana. Joseph na Emma walizika watoto sita, kila mmoja akiwa na umri mdogo wa miaka chini ya miwili. Lakini kutoka kwenye funuo alizozipokea, Joseph alipata mtazamo wa milele juu ya kifo na mpango wa Mungu wa milele. Fikiria kweli zilizofunuliwa katika Mafundisho na Maagano 29:26–27; 42:45–46; 63:49.; 88:14–17, 27–31; 93:33–34. Ni kwa jinsi gani funuo hizi huathiri jinsi unayoona kifo? Ni kwa jinsi gani zinaweza kuathiri jinsi unayoishi?
Ona pia 1 Wakorintho 15; M. Russell Ballard, “Ono la Ukombozi wa Wafu;” Ensign au Liahona, Nov. 2018, 71–74; Mafundisho ya Marais wa Kanisa: Joseph Smith (2007), 174–76.
Mafundisho na Maagano 18:10–13; 19:16–19; 45:3–5; 76:69–70
Yesu Kristo alitimiza “upatanisho kamili”
Njia moja ya kufokasi juu ya Mwokozi wakati wa Pasaka ni kujifunza funuo katika Mafundisho na Maagano zinazofundisha kuhusu dhabihu Yake ya upatanisho. Baadhi ya hizi zinaweza kupatikana katika Mafundisho na Maagano 18:10–13; 19:16–19; 45:3–5; 76:69–70. Pengine ungeweza kutengeneza orodha ya kweli kuhusu Upatanisho wa Mwokozi ambazo unapata katika mistari hii. Kuongeza kwa kina kujifunza kwako, ungeweza kuongeza kwenye orodha yako kwa kutafuta kwenye marejeo ya maandiko yaliyoorodheshwa katika “Patanisha, Upatanisho” (Mwongozo kwenye Maandiko, scriptures.ChurchofJesusChrist.org).
Haya ni baadhi ya maswali ambayo yangeweza kuongoza mafunzo yako:
-
Kwa nini Yesu Kristo aliamua kuteseka?
-
Ni nini lazima tufanye kupokea baraka za dhabihu Yake?
-
Ni kwa jinsi gani ninaweza kujua kama Upatanisho Wake una athari katika maisha yangu?
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani
-
Mkutano mkuuKwa sababu mkutano mkuu hufanyika wakati mmoja na Jumapili ya Pasaka mwaka huu, unaweza kufikiria jinsi jumbe za mkutano (pamoja na muziki) vinaweza kuongeza kwa kina zaidi ushuhuda wa familia yako wa Yesu Kristo. Kwa mfano, watoto wadogo wangeweza kuchora picha ya Mwokozi, au kushikilia juu picha Yake, wakati wanaposikia ujumbe au wimbo kuhusu Yesu Kristo. Wanafamilia wengine wangeweza kutengeneza orodha ya kweli wanazozisikia kuhusu Mwokozi. Baada ya hapo, wanafamilia wangeweza kushiriki michoro yao au orodha na shuhuda zao wenyewe za Yesu Kristo.
-
Mafundisho na Maagano 88:14–17; 138:17, 50.Familia yako inaweza kufurahia kufikiria analojia au somo la vifaa kuelezea kile inachomaanisha kufa na kufufuliwa—moja ambayo inaonesha mwili na roho zikitenganishwa na kisha kuunganishwa tena, kama vile mkono na glavu. Ni kwa jinsi gani mistari hii inaongeza shukrani zetu kwa ajili ya kile Mwokozi alichofanya kwa ajili yetu?
-
“Kristo Aliye Hai: Ushuhuda wa Mitume.”Kuchochea majadiliano kuhusu shuhuda za Mwokozi za manabii wa siku hizi, ungeweza kumpangia kila mwanafamilia kusoma sehemu ya “Kristo Aliye Hai: Ushuhuda wa Mitume” (Ensign au Liahona Mei 2017, ndani ya jalada la mbele) na kushiriki kile walichojifunza kuhusu Yesu Kristo. Ungeweza pia kuonesha video “Apostle Testimony Montage” (ChurchofJesusChrist.org). Ni kweli zipi tunazozipta ambazo zinatutia moyo?
-
“Najua kwamba Mkombozi Wangu yu Hai.”Kusaidia familia yako kufikiria njia nyingi ambazo kwazo Mwokozi aliyefufuka anatubariki leo, mngeweza kuimba pamoja “I Know that My Redeemer Lives” (Nyimbo za Kanisa, na.136) na kuunganisha kweli zilizofundishwa katika wimbo huu na zile zilizofundishwa katika maandiko yafuatayo: Mafundisho na Maagano 6:34; 45:3–5; 84:77; 98:18; 138:23. Famila yako ingeweza pia kufurahia kuandika mistari ya ziada kwa ajili ya wimbo ambao unaeleza jinsi wanavyojua kwamba Mkombozi wao yu hai.
Kwa ajili ya video ya Pasaka na nyenzo zingine, ona Easter.ComeUntoChrist.org.
Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.
Wimbo uliopendekezwa: “Jesus Has Risen,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto,70.