Mafundisho na Maagano 2021
Aprili 5–Aprili 11. Mafundisho na Maagano 30–36: “Umeitwa Kuhubiri Injili Yangu”


“Aprili 5–Aprili 11. Mafundisho na Maagano 30–36: ‘Umeitwa Kuhubiri Injili Yangu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Aprili 5–Aprili 11. Mafundisho na Maagano 30–36,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021

wamisionari wa mwanzo wa Kanisa

Aprili 5–Aprili 11

Mafundisho na Maagano 30–36

“Umeitwa Kuhubiri Injili Yangu”

Katika maandiko, tunaweza kupata umaizi kwa ajili ya hali zetu za kipekee. Mwombe Bwana akusaidie kupata ujumbe uliowekwa kwa ajili yako katika Mafundisho na Maagano 30–36.

Andika Misukumo Yako

Parley P. Pratt alikuwa muumini wa Kanisa kwa takribani mwezi mmoja wakati alipoitwa “nyikani” kuhubiri injili (Mafundisho na Maagano 32:2). Thomas B. Marsh alikuwa muumini kwa muda mfupi kuliko huo wakati alipoambiwa, “Saa ya huduma yako imewadia” (Mafundisho na Maagano 31:3). Orson Pratt, Edward Partridge, na wengine wengi kadhalika walikuwa ndio kwanza wamebatizwa wakati miito ya misheni zao ilipokuja. Pengine mpangilio huu ulisababishwa na haja—katika majira ya majani kupukutika ya mwaka 1830, hakuna yeyote aliyewahi kuwa muumini wa Kanisa zaidi ya miezi sita. Lakini kuna somo pia katika mpangilio huu kwa ajili yetu leo: kama unajua vya kutosha kukubali injili ya urejesho kwa ubatizo, unajua vya kutosha kuishiriki na wengine. Kwa vyovyote wote siku zote tunataka kuongeza ufahamu wetu wa injili, lakini Mungu kamwe hajasita kuwaita “wasio na elimu” kuhubiri injili Yake (Mafundisho na Maagano 35:13). Kwa kweli, Anatualika sisi sote, “Fungueni vinywa vyenu na kutangaza injili yangu” (Mafundisho na Maagano 30:5). Na tunafanya hivyo vizuri sana sio kwa kupitia hekima yetu wenyewe na uzoefu bali “kwa uwezo [wa] Roho” (Mafundisho na Maagano 35:13).

Ona pia “The Faith and Fall of Thomas Marsh,” “Ezra Thayer: From Skeptic to Believer,” “Orson Pratt’s Call to Serve,” Funuo katika Muktadha 54–69.

ikoni ya kujifunza kibinafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi

Mafundisho na Maagano 30–36

Nimeitwa kuhubiri injili ya Yesu Kristo.

Kama au sivyo una wito rasmi kama mmisionari, Bwana anakutaka kushiriki injili yake, na mengi ya maneno yake kwa wamisionari wa mwanzo wa kipindi hiki ni kwa ajili yako vilevile. Unapojifundisha Mafundisho na Maagano 30–36, andika kile unachojifunza kuhusu mwito wa kuhubiri injili. Ungeweza kutengeneza orodha ya vitu Bwana anavyovitaka kutoka kwa wamisionari Wake (kwa mfano, ona Mafundisho na Maagano 30:8) na orodha nyingine ya vitu Bwana anavyowaahidi (kwa mfano, ona Mafundisho na Maagano 30:11).

Ni kwa jinsi gani mistari hii inaweza kumtia moyo mtu fulani unayemjua anayetumikia au kujiandaa kutumikia kushawishi watu au kwa misheni ya huduma ya Kanisa? Unapata nini ambacho kinakutia msukumo kushiriki injili?

Ona pia Mafundisho na Maagano 35:13–15; Russell M. Nelson na Wendy W. Nelson, “Tumaini la Israeli” (ibada ya vijana ulimwenguni kote, Juni 3, 2018), Hopeoflsrael.ChurchofJesusChrist.org; Silvia H Allred, “Basi Enendeni,” Ensign au Liahona, Nov. 2008, 10–12.

wamisionari wakifundisha

Sisi sote ni wamisionari wa Kanisa la Yesu Kristo.

Mafundisho na Maagano 31:1–2, 5–6, 9,13

Bwana anaweza kunisaidia kwenye mahusiano ya familia yangu.

Familia katika miaka ya 1830 zilipambana na maswala mengi sawa na yale ambayo familia zinakabiliana nayo leo. Ni mwongozo na ahadi gani Bwana alizotoa kwa Thomas B. Marsh kuhusu familia yake? Ni kwa jinsi gani maneno yake yanaweza kukusaidia katika mahusiano ya familia yako?

Kwa maelezo zaidi kuhusu Thomas B. Marsh, ona Watakatifu, 1:79 –80, 119–20.

Mafundisho na Maagano 32;35

Je, misheni kwa Walamani ilikuwa ushinde?

Wakati Oliver Cowdery, Peter Whitmer mdogo, Parley P. Pratt, na Ziba Peterson walipotumwa kuhubiri kwa Wahindi wa Amerika magharibi ya Missouri, waliamini walikuwa wakitimiza unabii wa Kitabu cha Mormoni kuhusu Walamani kupokea injili katika siku za mwisho (ona, kwa mfano, 1 Nefi 13:34–41; Enoshi 1:11–18). Na bado mwishoni mwa misheni yao, hata ingawa walipata makabiliano chanya na baadhi ya makundi, hawakubatiza Mhindi wa Amerika hata mmoja. Lakini walikuwa wamebatiza zaidi ya watu mia moja karibu na Kirtland, Ohio, ambako walikuwa wamepiga kambi wakielekea Missouri. Miongoni mwa hao waongofu walikuwa viongozi wenye ushawishi katika Kanisa baadaye, ikiwa ni pamoja na Sidney Rigdon, na Kirtland baadaye ikawa eneo muhimu la kukusanyika kwa Kanisa. Uzoefu huu unakufundisha nini kuhusu jinsi Bwana anavyokamilisha kazi yake?

Ona pia “Misheni kwa Walamani,” Funuo katika Muktadha, 45–49.

Mafundisho na Maagano 33:12–18

Kama nikijenga maisha yangu juu ya injili ya Mwokozi, sitaanguka.

Mafundisho na Maagano 33 ilielekezwa kwa Northrop Sweet na Ezra Thayer, waongofu wawili wa karibuni. Northrop aliacha Kanisa mara baada ya ufunuo huu kutolewa. Ezra alihuduma kwa uaminifu kwa muda fulani, lakini yeye pia hatimaye alianguka. Hii inaweza kuwa fursa nzuri kutathmini jinsi ulivyojengwa kiuthabiti “juu [ya] mwamba” (mstari wa 13) wa injili. Ni kweli ipi katika mistari hii inaweza kukusaidia kubaki mwaminifu kwa Mwokozi?

ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani

Mafundisho na Maagano 30:2.Ni kwa jinsi gani tunafanya kama familia kwa kufokasi kwenye vitu vya Mungu kuliko “Vitu vya dunia”?

Mafundisho na Maagano 31.Unaposoma ahadi za Bwana kwa Thomas B. Marsh kuhusu familia yake, ungeweza kuzungumza kuhusu baraka ambazo zimekuja kwa familia yako kwa sababu ya kazi ya umisionari. Ungeweza pia kuimba Wimbo unaohusiana, kama vile “I’ll Go Where You Want Me to Go” (Nyimbo za Kanisa, na. 270). Ni kwa jinsi gani familia yako imebarikiwa kwa kushiriki injili na wengine?

Mafundisho na Maagano 33:7–10.Ni taswira gani Bwana alitumia katika mistari hii kuelezea kushiriki injili? Ni taswira zipi zingine au sitiari familia yako yaweza kuzifikiria? Pengine taswira hizi zingeweza kusaidia familia yako kufikiria kubuni njia za kushiriki injili. Majadiliano haya kisha yangeweza kuongoza kwenye mpango wa kushiriki injili. Fikiria kuigiza baadhi ya hali zinavyoweza kuwa.

Mafundisho na Maagano 34:10.Teua kirai kutoka Mstari wa 10, na mwalike mwana familia kukinong’ona. Wanafamilia wengine wangeweza kujaribu kukisia kirai. Kisha mtake mwanafamilia aseme kirai kwa sauti kubwa. Ni kwa jinsi gani shughuli hii inatusaidia kuelewa kwa nini Bwana anatuamuru “kuinua sauti zetu”?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa “I Hope They Call Me on a Mission,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 169.

ikoni ya sauti za urejesho

Sauti za Urejesho

Waongofu wa Mwanzo

Hata kabla Kanisa halijaanzishwa, Bwana alitangaza, “Shamba ni jeupe tayari kwa mavuno” (Mafundisho na Maagano 4:4). Maelezo haya yalithibitisha kuwa kweli katika miezi ambayo ilifuata, wakati watafutaji wengi wa ukweli waliongozwa na Roho wa Mungu kutafuta Kanisa la Urejesho la Yesu Kristo.

Wengi wa hawa waongofu wa mwanzo walikuwa wamehusika na kujenga msingi wa Urejesho, na hadithi zao za uongofu ni zenye thamani kwetu leo. Imani waliyoonesha ni imani ileile tunayohitaji ili kuwa waongofu kwenye injili ya Yesu Kristo.

Abigail Calkins Leonard

Wakati Abigail Calkins Leonard alipokuwa katika umri wa miaka ya thelathini, alihisi kutamani kusamehewa dhambi zake. Mara chache alisoma Biblia, na watu kutoka makanisa ya Kikristo walimtembelea nyumbani kwake, lakini alikuwa amekanganyikiwa kuhusu nini kilichotofautisha kanisa moja kutoka lingine. “Asubuhi moja, alisema, “Nilichukuwa Biblia yangu na nilikwenda msituni, nilipopiga magoti.” Alisali kwa unyenyekevu kwa Bwana. “Mara moja ono lilipita mbele ya macho yangu,” alisema, “na madhehebu tofauti yalinipitia moja baada ya jingine, na sauti iliniita, ikisema: ‘Haya yamejengwa kwa ajili ya kupata faida.’ Kisha, kwa mbele, niliweza kuona mwanga mkubwa, na sauti kutoka juu ilisema: ‘nitawainua watu, ambao nitafurahia kuwamiliki na kuwabariki.’” Muda mfupi baadaye, Abigail alisikia kuhusu Kitabu cha Mormoni. Japokuwa alikuwa bado hana nakala ya Kitabu cha Mormoni, alitafuta “kujua ukweli wa kitabu hiki, kwa karama na nguvu ya Roho Mtakatifu,” na “mara moja alihisi uwepo wake.” Mwishowe wakati alipoweza kusoma Kitabu cha Mormoni, alikuwa “tayari kukipokea.” Yeye na mume wake, Lyman, walibatizwa mwaka 1831,1

Thomas B. Marsh

Wakati Thomas B. Marsh alipokuwa kijana mkubwa, alijifunza Biblia na alijiunga na kanisa la Kikristo. Lakini hakutosheka, mwishowe kujitoa kutoka makanisa yote. “Nilikuwa na kipimo cha roho ya unabii,” alisema, “na nilimwambia [kiongozi wa kidini] kwamba nilitegemea kanisa jipya lingeinuka, ambalo litakuwa na ukweli katika usafi wake.” Sio muda mrefu baada ya haya, Thomas alipata msukumo wa kiroho kuacha nyumba yake huko Boston, Massachusetts, na kusafiri magharibi. Baada ya kuwa kwa miezi mitatu katika New York magharibi bila kupata kile alichokuwa akikitafuta, alianza kurudi nyumbani. Akiwa njiani, mwanamke alimwuliza Thomas kama alikuwa amesikia kuhusu “Kitabu cha dhahabu kilichogunduliwa na kijana anaeitwa Joseph Smith.” Akiwa amevutiwa na wazo hili, Thomas mara moja alisafiri kwenda Palmyra na alikutana na Martin Harris kwenye duka la kupiga chapa, ndio kwanza kurasa 16 za kwanza za Kitabu cha Momoni zikiwa zinatoka kwenye mashine ya uchapishaji. Thomas aliruhusiwa kuchukuwa nakala ya kurasa hizo 16, na alizipeleka nyumbani kwa mkewe, Elizabeth. “Alipendezwa sana” na kitabu, anakumbuka, “akikiamini kuwa ni kazi ya Mungu.” Thomas na Elizabeth baadaye walihamia New York na watoto wao na walibatizwa.2 Kwa maelezo zaidi kuhusu Thomas B. Marsh, ona Mafundisho na Maagano 31.)

Parley na Thankful Pratt

Kama Thomas Marsh, Parley na Thankful Pratt waliitikia msisimko wa kiroho kuacha mashamba yao yaliyostawi Ohio kwa nia ya kuhubiri injili walivyoielewa kutoka kwenye Biblia. Wakati Parley alipomwambia ndugu yake, “Roho wa mambo haya aligusa akili yangu kwa nguvu mno hivi karibuni kiasi kwamba sikuweza kupumzika.”3 Wakati walipofika mashariki ya New York, Parley alipata msukumo kubaki kwa muda katika eneo. Thankful, waliaamua, angeendelea bila Yeye. “Nina kazi ya kufanya katika jimbo hili la nchi,” Parley alimwambia, ”na ni kitu gani, au ni muda gani itachukuwa kukifanya, mimi sijui, lakini nitakuja wakati kitakapokuwa kimekamilika.”4 Ilikuwa pale ambapo Parley kwa mara ya kwanza alisikia juu ya Kitabu cha Mormoni. “Nilihisi mvuto wa ajabu katika kitabu,” alisema.5 Aliomba nakala na kusoma usiku mzima. Ilipofika asubuhi, alijua kitabu kilikuwa cha kweli, akakithamini “zaidi ya utajiri wote wa ulimwengu.”6 Ndani ya siku chache tu Parley alibatizwa. Kisha alirudi kwa Thankful, ambaye pia alibatizwa. (Kwa maelezo zaidi kuhusu Parley P. Pratt, ona Mafundisho na Maagano 32.)

Parley P. Pratt

Picha ya kuchora ya Parley P. Pratt na Jeffrey Hein

Sidney na Phebe Rigdon

Akiwa njiani kutoka New York kwenye Misheni huko Missouri, Parley Pratt na watumishi wenzake walipumzika Mentor, Ohio, nyumbani kwa Sidney na Phebe Rigdon—marafiki wa zamani wa Parley aliowajua kutoka siku zake Ohio. Sidney alikuwa mchungaji wa Kikristo, na Parley hapo mwanzo alikua muumini wa mkusanyiko wa watu wake na alimfikiria kama mshauri wa kiroho. Parley kwa shauku aliwaambia rafiki zake kuhusu Kitabu cha Mormoni na Urejesho wa injili ya Yesu Kristo. Sidney mwenyewe alikuwa akitafuta urejesho wa Kanisa la kweli ambalo alilipata limeelezwa katika Agano Jipya, ingawa alikuwa mwenye kushuku kuhusu Kitabu cha Mormoni hapo mwanzo. “Lakini nitakisoma kitabu chako,” alimwambia rafiki yake Parley, “na nitajaribu kuhakikisha, kama kitakuwa ufunuo kutoka kwa Mungu au la.”7 Baada ya wiki mbili za kujifunza na sala, wote yeye na Phebe waliridhika kitabu kilikuwa cha kweli. Lakini Sydney pia alijua kwamba kujiunga na Kanisa kungekuwa dhabihu kubwa kwa familia yake. Kwa dhahiri angepoteza kazi yake kama mchungaji, pamoja na hadhi yake ya kijamii katika jumuiya. Wakati yeye na Phebe walipojadili uwezekaano huu, Phebe alitangaza “nimehesabu gharama, na … ni tamanio langu kufanya mapenzi ya Mungu, iwe kwa uzima au iwe kwa kifo.”8

wanaume wakitembea katika theluji

Nenda Nyikani, na Robert T. Barrett