Mafundisho na Maagano 2021
Aprili 12–18. Mafundisho na Maagano 37–40: “Kama Hamna Umoja Ninyi Siyo Wangu”


“Aprili 12–18. Mafundisho na Maagano 37–40: ‘Kama Hamna Umoja Ninyi Siyo Wangu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Aprili 12–18. Mafundisho na Maagano 37–40,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021

Watakatifu wakijiandaa kuondoka

Watakatifu Wakienda Kirtland, na Sam Lawlor

Aprili 12–18

Mafundisho na Maagano 37–40

“Kama Hamna Umoja Ninyi Siyo Wangu”

Kuandika misukumo unapojifunza ni njia moja unayoweza kutii ushauri wa Mungu wa “kuihifadhi hekima” (Mafundisho na Maagano 38:30).

Andika Misukumo Yako

Kwa Watakatifu wa mwanzo, Kanisa lilikuwa zaidi ya sehemu ya kusikia baadhi ya mahubiri ya Jumapili. Katika funuo zote kwa Joseph Smith, Bwana alielezea Kanisa kwa maneno kama kusudi, ufalme, Sayuni, na hasa mara nyingi, kazi. Hiyo inaweza kuwa sehemu ya kile kilichowavutia waumini wengi wa mwanzo kwenye Kanisa. Ilimradi walipenda mafundisho ya urejesho ya Kanisa, wengi pia walitaka kitu fulani ambacho wangeweza kuweka wakfu maisha yao kwacho. Hata hivyo, amri ya Bwana ya mwaka 1830 kwa Watakatifu kukusanyika Ohio haikuwa rahisi kwa baadhi kuifuata. Kwa watu kama Phebe Carter, ilimaanisha kuacha nyumba zenye starehe wa ajili ya mpaka usiozoeleka (ona “Sauti za Urejesho” mwishoni mwa muhtasari huu). Leo tunaweza kuona kwa uwazi kile wale Watakatifu wangeweza kukiona tu na macho ya imani: Bwana alikuwa na baraka nyingi zikiwasubiri huko Ohio.

Haja ya kukusanyika Ohio imeshapita tangu siku nyingi, lakini Watakatifu leo bado wanaungana kwenye sababu ileile, kazi ileile: “kuistawisha Sayuni” (Mafundisho na Maagano 39:13). Kama wale Watakatifu wa mwanzo, tunaacha “shughuli za ulimwengu” (Mafundisho na Maagano 40:2) kwa sababu tunaamini ahadi ya Bwana: “Utapokea … baraka kubwa ambayo kamwe hujaijua” (Mafundisho na Maagano 39:10).

Ona pia Watakatifu, 1:109–11.

ikoni ya kujifunza kibinafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi

Mafundisho na Maagano 37:1

Joseph Smith alikuwa anatafsiri nini katika mwaka 1830?

Katika mstari huu, Bwana alikuwa akitaja kazi ya Joseph Smith juu ya kupitia upya marejeo ya Biblia, ambayo ilijulikana kama “tafsiri.” Wakati Joseph alipopokea ufunuo ulioandikwa katika sehemu ya 37, alikuwa amekamilisha sura chache za kitabu cha Mwanzo na alikuwa amejifunza punde tu kuhusu Enoki na jiji lake la Sayuni (ona Mwanzo 5:18–24; Musa 7). Baadhi ya kanuni Bwana alizomfundisha Enoki ni sawa na zile zilizofunuliwa katika sehemu ya 38.

Ona pia Mada za Historia ya Kanisa, “Tafsiri ya Joseph Smith ya Biblia,” ChurchofJesusChrist.org/study/topics.

Joseph Smith na Sidney Rigdon

Joseph Smith anafanya kazi na Sidney Rigdon kwenye kupitia upya Biblia. Vielelezo na Annie Henrie Nader

Mafundisho na Maagano 38

Mungu anatukusanya ili kutubariki.

Bwana alikamilisha amri Yake ya kukusanyika Ohio kwa kusema, “Tazama, hii ni hekima” (Mafundisho na Maagano 37:4). Lakini sio kila mtu aliiona hekima katika hilo moja kwa moja. Katika sehemu ya 38, Bwana alifunua hekima yake kwa undani zaidi. Unajifunza nini kutoka mstari wa 11–33 kuhusu baraka za kukusanyika? Waumini wa Kanisa hawaamriwi tena kukusanyika kwa kwenda mahala pamoja maalumu; ni kwa njia gani tunakusanyika leo? Ni kwa jinsi gani baraka hizi zinahusika kwetu? (ona Russell M, Nelson, “Kukusanyika kwa Israeli Waliotawanyika,” Ensign au Liahona, Nov. 2006, 79–81).

Unaposoma sehemu iliyobakia ya sehemu hii, tafuta dondoo ambazo ziliweza kuwasaidia Watakatifu kupata imani waliyohitaji kutii amri ya Mungu ya kukusanyika Ohio. Pia fikiria kuhusu amri Alizokupa wewe na imani unayohitaji kuzitii. Maswali yafuatayo yangeweza kuongoza kujifunza kwako:

  • Je, unapata nini katika mstari wa 1–4 ambacho kinakupa ujasiri katika Bwana na amri Zake?

  • Ni kwa jinsi gani mstari wa 39 unaweza kukusadia kutii amri za Mungu hata wakati zinapohitaji dhabihu?

Je, ni nini kingine unapata?

Mafundisho na Maagano 38:11–13, 22–32, 41–42

Kama nimejitayarisha, sina haya ya kuogopa.

Watakatifu walikuwa tayari wamekwisha kabiliana na upinzani mkubwa, na Bwana alijua mengi yalikuwa yanakuja (ona Mafundisho na Maagano 38:11–13, 28–29). Kuwasaidia wasiogope, Yeye alifunua kanuni ya thamani: “Kama mmejitayarisha hamtaogopa” (Mafundisho na Maagano 38:30). Chukua dakika kutafakari changamoto unazokabiliana nazo. Kisha unapojifunza sehemu ya 38, sikiliza ushawishi kutoka kwa Roho kuhusu jinsi unavyoweza kujitayarisha kwa ajili ya changamoto ili kwamba usiogope.

Ona pia Ronald A. Rasband, ““Usiwe na Hofu”,” Ensign au Liahona, Nov. 2018, 18-21.

Mafundisho na Maagano 39–40

Shughuli za ulimwengu hazipaswi kunivuruga katika kutii neno la Mungu.

Soma sehemu ya 3940, ikiwa ni pamoja na historia ya nyuma katika vichwa vya habari vya sehemu, na fikiria jinsi uzoefu wa James Covel ungeweza kutumika kwako. Kwa mfano, fikiria wakati ambapo “moyo … wako ulikuwa safi mbele ya [Mungu]” (Mafundisho na Maagano 40:1). Ulibarikiwa vipi kwa sababu ya uaminifu wako? Pia fikiria juu ya “shughuli za ulimwengu” unazokabiliana nazo (Mafundisho na Maagano 39:9; 40:2). Ni kipi unachopata katika sehemu hizi ambacho kinakutia msukumo kuwa mtiifu thabiti zaidi?

Ona pia Mathayo 13:3–23.

ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani

Mafundisho na Maagano 37:3.Kuisaidia familia yako kuelewa dhabihu Watakatifu waliyofanya kukusanyika Ohio, unaweza kurejea kwenye ramani ambayo inaambatana na muhtasari huu.

Mafundisho na Maagano 38:22.Ni kwa jinsi gani tunaweza kumfanya Yesu Kristo “mtoa sheria” wa familia yetu? Ni kwa jinsi gani kufuata sheria Zake kunatufanya “watu huru”?

Mafundisho na Maagano 38:24–27.Ili kuwafundisha watoto inamaanisha nini kuwa “wamoja,” ungeweza kuwasaidia kuhesabu washiriki wa familia yako na kuzungumza kuhusu kwa nini kila mtu ni muhimu kwenye familia yako. Sisitiza kwamba kwa pamoja ninyi ni familia moja. Ungeweza kuwasaidia watoto wako kuchora 1 kubwa kwenye bango na kuipamba kwa majina na michoro au picha za kila mwanafamilia. Ungeweza pia kuandika kwenye bango mambo mtayoyafanya kuwa wenye umoja zaidi kama familia. Mnaweza pia kuangalia video “Love in Our Hearts” (ChurchofJesusChrist.org) au soma Musa 7:18.

Mafundisho na Maagano 38:29–30.Mngeweza kujadili uzoefu wa hivi karibuni wa familia au kibinafsi ambao ulihitaji maandalizi. Ni kwa jinsi gani maandalizi yenu yaliathiri uzoefu? Bwana anatutaka sisi tujiandae kwa ajili gani? Ni kwa jinsi gani kujiandaa kunatusaidia kutokuwa na hofu? Tuweza kufanya nini ili kujiandaa?

Mafundisho na Maagano 40.Kirai “shughuli za ulimwengu” (mstari wa 2) kina maana gani kwetu? Je, kuna shughuli zozote za ulimwengu ambazo zinatuzuia kupokea neno la Mungu “kwa furaha”? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuzishinda?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa. “Jesus Said Love Everyone,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 61.

ikoni ya sauti za urejesho

Sauti za Urejesho

Kukusanyika Ohio

Majengo ya Kirtland

Kijiji cha Kirtland, na Al Rounds

Phebe Carter Woodruff

Miongoni mwa Watakatifu wengi waliokusanyika Ohio katika miaka ya 1830 alikuwa Phebe Carter. Alijiunga na Kanisa katika kaskazini mashariki mwa Marekani akiwa na umri wa kati ya miaka ishirini, ingawa wazazi wake hawakujiunga. Baadaye aliandika juu ya uamuzi wake kuhamia Ohio kujiunga na Watakatifu:

“Marafiki zangu walishangaa kwa mwelekeo wangu, kama mimi nilivyoshangaa, lakini kitu fulani ndani yangu kilinisukuma niendelee. Huzuni ya Mama yangu kwa kuondoka kwangu nyumbani ilikuwa takribani zaidi ya ninavyoweza kuvumilia; na isingekuwa kwa roho ndani yangu ningesita mwishowe. Mama yangu aliniambia afadhali angeniona mimi nikizikwa kuliko kuondoka hivi peke yangu nje katika ulimwengu katili.

“‘[Phebe],’ alisema, kwa kuvutia, ‘je, utarudi kwangu kama utaona umormoni ni uongo?’

“Nilijibu, ‘ndiyo, mama; nitarudi.’ … Jibu langu lilituliza wasiwasi wake; lakini lilitusababishia wote huzuni kubwa kutengana. Wakati muda ulipofika wa kuondoka kwetu sikudhubutu kujiamini mwenyewe kusema kwaheri; kwa hiyo niliandika kwaheri zangu kwa kila mmoja, na kuziacha juu ya meza yangu, nikakimbia kushuka ngazi na kurukia kwenye gari la farasi. Hivyo niliacha nyumba niliyoipenda ya utoto wangu kuunganisha maisha yangu na watakatifu wa Mungu. ”1

Katika moja ya jumbe hizo za kuagana, Phebe aliandika:

“Wazazi Wapendwa—Mimi sasa niko karibu kuacha paa la baba yangu kwa muda … sijui kwa muda gani—lakini sio bila hisia ya shukrani kwa ukarimu ambao nimeupata kutoka utoto wangu mpaka sasa—lakini Majaliwa yanaonekana kuamua vinginevyo sasa kuliko ilivyokuwa. Wacha tuache vitu hivi vyote kwenye mikono ya Majaliwa na tuwe wenye shukrani kwamba tumeruhusiwa kuishi pamoja kwa muda mrefu chini ya hali za kufaa kama tulivyoishi, tukiamini kwamba vitu vyote vitafanya kazi kwa ajili ya faida yetu kama tunampenda Mungu kikamilifu. Wacha tutambue kwamba tunaweza kusali kwa Mungu mmoja ambaye atasikia sala za dhati za viumbe vyake vyote na kutupatia kile ambacho ni kizuri zaidi kwa ajili yetu. …

“Mama, ninaamini ni mapenzi ya Mungu kwangu mimi kwenda magharibi na nimeshawishika kwamba imekuwa kwa muda mrefu. Sasa njia imefunguka … ; ninaamini kwamba ni roho wa Bwana ambaye amefanya kile ambacho kinatosha kwa ajili ya mambo yote. Usiwe na wasiwasi kwa ajili ya mtoto wako; Bwana atanifariji. Ninaamini kwamba Bwana atanitunza na kunipa kile ambacho ni kwa ajili ya kilicho bora zaidi. … Ninakwenda kwa sababu Bwana wangu anaita—ameifanya kazi yangu rahisi.”2

Muhtasari

  1. Katika Edward W. Tullidge, The Women of Mormondom (1877), 412.

  2. Barua ya Phebe Carter kwa wazazi wake, hakuna tarehe, Maktaba ya Historia ya Kanisa, Jiji la Salt Lake, vituo vya uandishi vimebadilishwa. Phebe alijiunga na Kanisa mwaka 1834, akahamia Ohio mnamo 1835, na akaolewa na Wilford Woodruff mwaka 1837.