Mafundisho na Maagano 2021
Aprili 12–18. Mafundisho na Maagano 37–40: “Kama Hamna Umoja Ninyi Siyo Wangu”


“Aprili 12–18. Mafundisho Maagano 37–40: ‘Kama Hamna Umoja Ninyi Siyo Wangu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Aprili 12–18. Mafundisho na Maagano 37–40,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2021

Picha
Watakatifu wakijiandaa kuondoka

Watakatifu Wakihamia Kirtland, na Sam Lawlor

Aprili 12–18

Mafundisho na Maagano 37–40

“Kama Hamna Umoja Ninyi Siyo Wangu”

Mungu anajua kwamba watoto katika darasa lako wanahitaji kujifunza. Muache Yeye akuongoze pale unapochagua kanuni na shughuli za kukusaidia kuwafundisha.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Pitisha nakala ya maandiko. Pale kila mtoto anaposhikilia maandiko, mruhusu mtoto yule kushiriki jambo moja analokumbuka kutoka kwenye somo la wiki iliyopita au kutoka kwenye usomaji wa maandiko nyumbani wiki hii.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mafundisho na Maagano 38:24–27

Ninaweza kuwapenda wengine.

Bwana aliwataka Watakatifu kukusanyika pamoja Ohio na kupendana kama wenzi kwa usawa. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kuhisi umoja na upendo kwa wengine?

Shughuli za Yakini

  • Tumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii kuwaonesha watoto kwamba wakati Kanisa lilipokuwa changa, Bwana aliwaomba waumini kuhama pamoja kwenda Ohio (ona pia ramani katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Mungu aliwataka kujifunza jinsi ya kupenda na kuelewana wao kwa wao. Waulize watoto mawazo kuhusu jinsi wanavyoweza kuonesha upendo mmoja kwa mwingine.

  • Soma Mafundisho na Maagano 38:25 kwa watoto, na waambie kwa maneno yako mwenyewe kile inachomaanisha kumtendea kaka yako na dada yako kama unavyojitendea (ona pia Mathayo 7:12). Wasaidie warudie andiko, wakibadili “ndugu yako” kwa majina ya kila mmoja.

  • Imbeni wimbo kuhusu kupenda na kuwajumuisha wengine, kama vile “I’ll Walk with You” au “We Are Different” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 140–41, 263). Mnapoimba, waache watoto kuinua picha za watoto kutoka maeneo mengine ulimwenguni.

  • Wasaidie watoto kuigiza hali ambapo mtu mgeni anajiunga na darasa lao la Msingi. Ni kwa jinsi gani tungeweza kumsaidia kuhisi kukaribishwa? Watoto wangeweza kufurahia kufanya igizo hili kwa kutumia karagosi za vidole au maumbo yaliyokatwa.

Mafundisho na Maagano 38:30

Kama nimejitayarisha, sitaogopa.

Njia moja ambayo Baba wa Mbinguni hutusaidia sisi kutokuogopa ni kwa kutufundisha sisi kujitayarisha.

Shughuli za Yakini

  • Rudia mara kadhaa kirai “Kama mmejitayarisha hamtaogopa” (mstari wa 30). Baada ya mara kadhaa, acha kuandika neno, na waache watoto kusema neno linalokosekana. Waambie watoto kuhusu wakati ambapo ulikuwa umejitayarisha kwa ajili ya jambo fulani na kujitayarisha kulikusaidia wewe kutokuogopa.

  • Wasaidie watoto kufikiria mambo ambayo Baba wa Mbinguni anawataka wajitayarishe kwayo, kama vile kubatizwa au kwenda hekaluni. Tumia picha au vitu ili kuwapa mawazo. Zungumza kuhusu jinsi wanavyoweza kujitayarisha, na waache wachore picha zao wenyewe wakijitayarisha au kushiriki katika mambo waliyoyafikiria.

Mafundisho na Maagano 39:6, 23

Ninapokea kipawa cha Roho Mtakatifu wakati ninapothibitishwa.

Ni nini watoto katika darasa lako wanahitaji ili kuelewa kuhusu kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu? Maelekezo ya Bwana kwa James Covel kuhusu ibada hii yangeweza kusaidia.

Shughuli za Yakini

  • Onesha picha ya mtu akibatizwa na mtu akithibitishwa (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 104, 105). Soma Mafundisho na Maagano 39:23, na waombe watoto waoneshe kwa kidole picha sahihi wakati wanaposikia ukisoma kuhusu ubatizo au uthibitisho.

  • Someni pamoja Mafundisho na Maagano 39:6, na waoneshe watoto picha au vitu ambavyo huwakilisha njia ambazo kwazo Roho Mtakatifu hutubariki (ikijumuisha zile zilizotajwa katika mstari wa 6). Waache watoto wafanye zamu kushikilia picha au vitu, na wanapofanya hivyo, toa ushuhuda kuhusu jinsi Roho Mtakatifu alivyokubariki katika njia hizi. Wasaidie watoto kutambua nyakati walipohisi ushawishi wa Roho.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mafundisho na Maagano 37; 38:31–33

Mungu anatukusanya ili kutubariki.

Kukusanyika katika Ohio kulikuwa dhabihu kubwa kwa wengi wa Watakatifu wa mwanzo. Leo hatuamriwi kukusanyika katika eneo moja, lakini tunakusanyika kama familia, kata na vigingi.

Shughuli za Yakini

  • Waoneshe watoto ukurasa wa shughuli ya wiki hii au ramani kwenye muhtasari wa wiki hii katika Njoo Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Someni pamoja Mafundisho na Maagano 37, na wasaidie watoto kutafuta kwenye ramani maeneo yaliyotajwa kwenye ufunuo. Ni nini Bwana aliwaamuru Watakatifu kufanya?

  • Chagua kirai muhimu au sentensi kutoka Mafundisho na Maagano 38:31–33 ambayo unahisi inaelezea kwa nini Bwana aliwataka watu wake kukusanyika pamoja. Tawanya maneno kutoka kwenye sentensi hii kuzunguka chumba, na waalike watoto kuyakusanya, kuyaweka katika mpangilio sahihi, na kutafuta wapi sentensi inatokea katika mistari. Je, ni kwa nini Bwana anatutaka tukusanyike?

Mafundisho na Maagano 38:24–27

Mungu anataka watu Wake kuwa na umoja.

Ili kuwaandaa Watakatifu kukusanyika, Bwana aliwafundisha kumuona kila mmoja sawa na “kuwa na umoja” (mstari wa 27). Ni kwa jinsi gani elekezo hili linabariki watoto unaowafundisha?

Shughuli za Yakini

  • Someni pamoja Mafundisho na Maagano 38: 24–24, na waalike watoto kuandika maneno kutoka kwenye mistari hii ambayo wanahisi ni muhimu, ikijumuisha maneno ambayo yamerudiwa. Kwa nini Bwana aliweza kuyarudia maneno haya? Waache washiriki kile walichoandika, na wajaidli kile walichojifunza kutoka kwenye maneno hayo.

  • Wasaidie watoto kufikiria hali ambapo mtu angeweza kuhisi kuachwa nje, kama vile, kuwa muumini mpya wa Kanisa au kuhamia kwenye ujirani mpya au shule mpya. Kwa nini Mafundisho na Maagano 38:24–27 inapendekeza kuhusu jinsi tunavyopaswa kumtendea mtu katika hali hizi? Igizeni baadhi ya hali zinazowezekana.

  • Shiriki somo la vitendo ambalo linaelezea kwa mfano jinsi vitu vinavyoweza kuunganishwa kuwa kitu kimoja, kama vile vipande vya nguo ambavyo vinatengeneza farishi moja au viungo vinavyotengeneza boflo moja la mkate. Ni nini mifano hii hutufundisha kuhusu kuwa na umoja kama watu wa Mungu?

Mafundisho na Maagano 39–40

Ninaweza kuzishika ahadi zangu.

James Covel alikuwa ameweka ahadi ya kumtii Bwana, lakini hakushika ahadi yake. Kujifunza kuhusu uzoefu wake kungeweza kuwasaidia watoto kukumbuka umuhimu wa kuwa watiifu.

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto wasome vichwa vya habari vya sehemu za Mafundisho na Maagano 39 na 40, na waombe wafanye ufupisho kwa maneno au kwa michoro kile wanachojifunza kuhusu James Covel.

  • Andika maswali ubaoni ambayo yatawasaidia watoto kuelewa sehemu ya 40, kama vile Ni nini James Covel aliweka agano kufanya? Kwa nini hakushika agano lake? Waalike watoto kutafuta majibu katika sehemu ya 40.

  • Wasaidie watoto kukumbuka ahadi walizofanya wakati walipobatizwa (ona Mosia 18:8–10). Wasaidie watoto kuorodhesha baadhi ya hofu au “shughuli za ulimwengu” (Mafundisho na Maagano 40:2) ambazo zingeweza kumzuia mtu kutii ahadi hizi. Waalike watoto kujiandikia ujumbe mfupi kama ukumbusho kwamba kutii amri za Baba wa Mbinguni kutawasaidia kushinda hofu au shughuli za ulimwengu. Wahimize kuweka kumbusho lao mahali ambapo wanaweza kuliona mara kwa mara.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kujadili na wazazi wao au wanafamilia wengine jinsi wanavoweza kuwa zaidi wenye umoja kama familia.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Kariri andiko. Fikiria kuchagua kifungu cha maandiko ambacho unadhani kingeweza kuimarisha shuhuda za watoto, na wasaidie kukikariri. Watoto wadogo wangeweza kukariri sehemu ya andiko au kirai tu.

Picha
ukurasa wa shughuli: ninaweza kuwapenda wengine

Chapisha