Mafundisho na Maagano 2021
Aprili 19–25. Mafundisho na Maagano 41–44: “Sheria Yangu ya Kulitawala Kanisa Langu”


“Aprili 19–25. Mafundisho na Maagano 41–44: ‘Sheria Yangu ya Kulitawala Kanisa Langu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Aprili 19–25. Mafundisho na Maagano 41–41,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi

Picha
Yesu Kristo

Aprili 19–25

Mafundisho na Maagano 41–44

“Sheria Yangu ya Kulitawala Kanisa Langu”

Wakati wa maandalizi yako wiki hii, tilia maanani misukumo unayopokea kutoka kwa Roho. Nini unahisi watoto wanahitaji kujifunza kutoka Mafundisho na Maagano 41–44?

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Rusha mpira kwa mtoto, na muombe mtoto kushiriki amri moja ambayo anajua kuihusu. Endelea kupitisha mpira mpaka kila mmoja amepata nafasi ya kushiriki jambo.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mafundisho na Maagano 42:2

Ninaweza kutii sheria za Mungu.

Wakati Kanisa lilipokua na waumini walikusanyika Kirtland, Ohio, Bwana alimfunulia Joseph Smith kile Yeye alichokiita “sheria” na kuwaamuru Watakatifu “kusikiliza na kusikia na kutii” sheria hiyo. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kuelewa kwamba tunabarikiwa wakati tunapokuwa watiifu?

Shughuli za Yakini

  • Soma Mafundisho na Maagano 42:2, ukisisitiza neno “kutii.” Wape watoto mpangilio rahisi wa matukio ambapo mtoto huchagua kutii au kutotii sheria. Waombe watoto kusikiliza kwa makini na kutabasamu ikiwa mtu katika hadithi anatii na kununa ikiwa mtu hatii. Shiriki baraka ambazo umepokea wakati ulipotii sheria za Mungu.

  • Chezeni mchezo kwa kuwapa watoto sheria ya kufuata. Kwa mfano, ungeweza kuwaambia kwamba lazima wainue mikono yao na kuitwa kwa ajili ya kujibu maswali. Kisha waruhusu wafanye mazoezi ya kutii kwa kuwauliza maswali na kuwaita wale wanaoinua mikono. Ni sheria zipi Mungu ametupatia?

  • Kamilisha ukurasa wa shughuli pamoja na watoto, au imbeni wimbo kuhusu kutii sheria za Mungu, kama vile “I Want to Live the Gospel” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 148). Waambie watoto jinsi kutii sheria za Mungu kulivyokuletea furaha.

    Picha
    Darasa la Msingi

    Tunajifunza amri za Mungu katika Msingi.

Mafundisho na Maagano 42:38

Ninamtumikia Yesu Kristo pale ninapowatumikia wengine.

Bwana anawataka Watakatifu Wake kuwajali masikini na wenye mahitaji. Wasaidie watoto kuelewa kwamba wakati wanapowatumikia watu wenye mahitaji, wanamtumikia pia Mwokozi.

Shughuli za Yakini

  • Kama Yesu Kristo angekuwa darasani kwetu leo, je, ungemwambia nini? Ni kwa jinsi gani tungemtendea Yeye? Onesha picha ya Mwokozi, na elezea fundisho la Yesu kwamba wakati tunapoonesha upendo kwa wengine, tunaonesha pia upendo Kwake. Wasaidie watoto kurudia mstari wa 38 pamoja na wewe, maneno machache kwa wakati.

  • Wasaidie watoto kufikiria njia wanazoweza kumtumikia Yesu kwa kuwatumikia wengine. Wanaweza kupata baadhi ya mawazo kutoka kwenye video “Pass It On” (ChurchofJesusChrist.org) au kutoka kwenye picha za Mwokozi akiwasaidia wengine, kama vile picha Zake akiwaponya wagonjwa au kuwa mkarimu kwa watoto (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 42, 47). Shuhudia kwamba wanapowatumikia wengine, wanamtumikia pia Yesu.

Mafundisho na Maagano 43:1–7

Bwana analiongoza Kanisa Lake kupitia nabii Wake.

Unaweza kuwasaidia watoto kuepuka kudanganywa kote katika maisha yao kwa kuwafundisha, wakati wakiwa wadogo, mpangilio wa Bwana kwa ajili ya kuongoza Kanisa Lake kupitia nabii aliye hai.

Shughuli za Yakini

  • Onesha picha za watu tofauti, ikijumuisha picha ya nabii wa sasa. Weka picha nyuso zikiwa upande wa chini, na waruhusu watoto kugeuza picha moja moja mpaka wampate nabii. Elezea mafundisho ya Bwana kwamba nabii pekee “nimemteua kwenu kupokea amri na mafunuo kutoka kwa [Bwana]” kwa ajili ya kuongoza Kanisa (Mafundisho na Maagano 43:2).

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu manabii, kama vile ubeti wa mwisho wa “Follow the Prophet” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 110–11). Shiriki ushuhuda wako kwamba nabii analiongoza Kanisa.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mafundisho na Maagano 41:5

Mwanafunzi ni mtu anayepokea sheria ya Mungu na kuitii.

Je, watoto unaowafundisha wanajua kile inachomaanisha kuwa mwanafunzi wa Yesu Kristo? Mafundisho na Maagano 41:5 inaweza kuwasaidia kuelewa jinsi ya kuwa wanafunzi wazuri.

Shughuli za Yakini

  • Andika Mafundisho na Maagano 41:5 kwenye kipande cha karatasi, ukiacha nafasi wazi pale neno “mwanafunzi” linapopaswa kuwa. Waombe watoto wajaze nafasi zilizo wazi, wakitafuta kwenye Mafundisho na Maagano 41:5 ikiwa wanahitaji msaada. Inamaanisha nini kuwa mwanafunzi wa Yesu Kristo? Shiriki jinsi unavyojitahidi kuwa mwanafunzi mzuri wa Yesu Kristo.

  • Baada ya kujadili Mafundisho na Maagano 41:5, waombe watoto wafikirie sheria tulizopokea kutoka kwa Bwana. Waalike wafanye zamu kuigiza kutii mojawapo ya sheria hizo wakati wengine wakijaribu kubashiri sheria hiyo ni nini.

  • Mpe kila mwana darasa kipande cha karatasi, na waombe waandike juu yake njia moja wanayoweza kuwa wanafunzi wazuri. Mwalike kila mtoto kushiriki kile walichoandika, na kisha kugundisha vipande pamoja kutengeneza mnyororo wa karatasi.

Mafundisho na Maagano 42:61, 68

Mungu hufunua hekima kwa wale wanaoomba.

Watoto wanauliza maswali mengi wakati wanapokua katika ufahamu wa ulimwengu na injili. Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia Mafundisho na Maagano 42:61, 68 kuwasaidia kujua jinsi ya kupata hekima kutoka kwa Bwana?

Shughuli za Yakini

  • Waombe watoto kushiriki pamoja nawe jambo linalowasaidia kuhisi amani na jambo linalowasaidia kuhisi shangwe. Waalike wasome Mafundisho na Maagano 42:61 wakitafuta maneno “amani” na “shangwe.” Wasaidie watoto kufikiria kweli ambazo Mungu amefunua ambazo zinawaletea amani na shangwe.

  • Soma Mafundisho na Maagano 42:61, 68 pamoja na watoto, ukisisitiza kirai “ufunuo juu ya ufunuo, maarifa juu ya maarifa.” Elezea kwamba Mungu hafunui kila kitu mara moja; badala yake, Yeye hutupatia kidogo kadiri ya muda. Onesha jinsi chemsha bongo inavyojengwa kidogo kidogo, au tumia kitu kinachofanana ili kuwasaidia watoto kuelewa kanuni hii. Shiriki uzoefu ambapo ulipokea ufunuo ambao ulikubariki.

Mafundisho na Maagano 43:1–7

Ni nabii pekee anaweza kupokea ufunuo kwa ajili ya Kanisa lote.

Watoto wanapokua, wanaweza kukutana na watu wanaotaka kuwapotosha. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kuamini mpangilio wa Mungu wa kuwaongoza watoto Wake kupitia nabii Wake aliyechaguliwa?

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto kufikiria kwamba mtu anasimama kwenye mkutano wa ushuhuda na kuiambia kata kwamba amepokea ufunuo kwa ajili ya Kanisa (kwa mfano, kwamba hatupaswi tena kunywa maziwa au kwamba tunapaswa kuanza kufanya mikutano ya sakramenti Jumanne badala ya Jumapili). Anasema kwamba tunapaswa kusikiliza kile anachosema badala ya kumsikiliza nabii. Je, nini kitakuwa si sahihi kuhusu hilo? Wasaidie watoto wasome Mafundisho na Maagano 43:1–7 ili kutafuta jinsi Bwana anavyotoa amri kwa Kanisa Lake.

  • Onesha picha ya nabii aliye hai, waalike watoto washiriki jambo alilofundisha hivi karibuni. Ikiwa wanahitaji msaada, onesha video fupi au soma kifungu cha maneno kutoka kwenye ujumbe wa mkutano mkuu wa hivi karibuni. Kwa nini ni baraka kuwa na nabii aliye hai leo?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kuchagua sheria au amri wanayohisi wanapaswa kufokasi katika kuitii wiki hii. Wahimize kushiriki lengo lao pamoja na familia zao.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wafundishe watoto kuandika misukumo. Hata watoto wanaweza kujifunza tabia ya kuandika misukumo ya kiroho. Wanaweza kuandika misukumo kwa kuwekea alama maandiko, kuchora picha, au kuweka kumbukumbu rahisi katika shajara zao.

Picha
ukurasa wa shughuli: ninakuwa na furaha pale ninapomtii Mungu

Chapisha