Mafundisho na Maagano 2021
Aprili 19–25. Mafundisho na Maagano 41–44: “Sheria Yangu Kutawala Kanisa Langu”


“Aprili 19–25. Mafundisho na Maagano 41–44: ‘Sheria Yangu Kutawala Kanisa Langu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Aprili 19–25. Mafundisho na Maagano 41–44,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021

Picha
Yesu Kristo

Aprili 19–25

Mafundisho na Maagano 41–44

“Sheria Yangu Kutawala Kanisa Langu”

“Ikiwa utaomba,” Bwana aliahidi, “utapokea ufunuo juu ya ufunuo, maarifa juu ya maarifa” (Mafundisho na Maagano 42:61). Ni maswali gani unayoweza kuuliza ili upokee ufunuo unaouhitaji?

Andika Misukumo Yako

Kukua kwa haraka kwa Kanisa katika mwaka 1830 na 1831—hususani uvamizi wa waongofu wapya kuja Kirtland, Ohio—kulikuwa kwa kufurahisha na kutia moyo kwa Watakatifu. Lakini pia kulileta changamoto kadha wa kadha. Unaunganishaje mkusanyiko unaopanuka kwa haraka wa waumini, hususani wakati wanapoleta pamoja nao mafundisho na desturi kutoka imani zao za zamani? Kwa mfano, wakati Joseph Smith alipowasili Kirtland mapema Februari 1831, aliwakuta waumini wapya wakishirikiana mali ya pamoja katika kujaribu kwa dhati kuiga Wakristo wa Agano Jipya (ona Matendo ya Mitume 4:32–37). Bwana alifanya marekebisho kadhaa muhimu na akatoa ufafanuzi kwa hili na mada zingine, kwa ujumla kupitia ufunuo uliorekodiwa katika Mafundisho na Maagano 42, ambao Yeye aliuita “sheria yangu Kutawala Kanisa Langu” (mstari wa 59). Katika ufunuo huu, tunajifunza kweli ambazo ni za msingi katika kuanzisha Kanisa la Bwana katika siku za mwisho, ikiwa ni pamoja na ahadi muhimu kuweka wazi kwamba siku zote kuna mengi ya kujifunza: “Ikiwa utaomba, utapokea ufunuo juu ya ufunuo, maarifa juu ya maarifa” (Mafundisho na Maagano 42:61).

Ona pia Watakatifu, 1:114–19.

Picha
ikoni ya kujifunza kibinafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi

Mafundisho na Maagano 41

“Yeye ambaye huipokea sheria yangu na kuitenda, huyo ndiye mwanafunzi wangu”

Mnamo mapema mwaka 1831, Watakatifu walikuwa wanaanza kukusanyika Ohio, wakiwa na hamu ya kupokea sheria ambayo Mungu aliahidi kuifunua pale (ona Mafundisho na Maagano 38:32). Lakini kwanza, Bwana alifundisha jinsi wafuasi wake wanavyopaswa kujiandaa kupokea sheria Yake. Ni kanuni gani unazozipata katika mstari wa 1–5 ambazo zingeweza kuwasaidia Watakatifu kupokea sheria ya Mungu? Ni kwa jinsi gani kanuni hizi zinakusaidia kupokea maelekezo kutoka Kwake?

Mafundisho na Maagano 42

Sheria za Mungu zinatawala Kanisa Lake na zinaweza kutawala maisha yetu.

Watakatifu walichukulia ufunuo unaopatikana katika Mafundisho na Maagano 42:1–72 kuwa mojawapo wa zile muhimu Nabii alizozipokea. Ulikuwa miongoni zile za kwanza kuchapishwa, ikitokea katika magazeti mawili ya Ohio, na ilijulikana kwa kawaida kama “sheria.” Nyingi za kanuni katika sehemu hii zilikuwa zimekwishafunuliwa na Bwana mapema. Wakati sehemu haijumuishi kila amri Bwana aliyotaka Watakatifu Wake waitii, inastahili kutafakari kwa nini kanuni hizi zilikuwa muhimu kurudiwa kwa Kanisa lililorejeshwa karibuni.

Ingeweza kukusaidia kusoma sehemu ya 42 katika sehemu ndogo ndogo kama zifuatazo na kutambua kanuni zilizofundishwa katika kila moja. Unapofanya hivyo, fikiria jinsi sheria hii ya kuongoza Kanisa ingeweza pia kusaidia kuongoza maisha yako binafsi.

Mstari wa 4–9, 11–17, 56–58 

Mstari wa 18–29 

Mstari wa 30–31 

Mstari wa 40–42 

Mstari wa 43–52 

(Ona pia 3 Nefi 15:9).

Mafundisho na Maagano 42:30–42

Ni kwa jinsi gani Watakatifu “waliweka wakfu mali [zao]” kusaidia masikini?

Sehemu muhimu ya sheria iliyofunuliwa katika Sehemu ya 42 ni kile kilichokuja kujulikana kama sheria ya uwekaji wakfu na usimamizi. Sheria hii iliwafundisha Watakatifu jinsi ambavyo wangeweza, kama wafuasi wa Kristo wa kale, kuwa na “vitu vyote pamoja” (Matendo ya Mitume 2:44; 4 Nefi 1:3), na “hakuna masikini miongoni mwao” (Musa 7:18) Watakatifu waliweka wakfu mali zao kwa kuzitoa kwa Bwana, kupitia kwa askofu (ona Mafundisho na Maagano 42: 30–31). Askofu aliwarudishia kile walichohitaji (ona mstari wa 32)—kwa kawaida kile walichoweka wakfu na zaidi. Waumini walichanga cha ziada chao kusaidia masikini (ona mstari wa 33–34). Sheria hii ilikuwa baraka kuu kwa Watakatifu, hususani kwa wale walioacha kila kitu kuja Ohio. Watakatifu wengi walikuwa wakarimu katika michango yao.

Ingawa tunafanya kitofauti siku hizi, Watakatifu wa Siku za Mwisho bado wanaishi sheria ya kuweka wakfu. Unaposoma Mafundisho na Maagano 42:30–42, tafakari jinsi unavyoweza kuweka wakfu kile Mungu alichokupa ili kujenga ufalme Wake na kuwabariki wale wenye shida.

Ona pia Linda K. Burton, “Nalikuwa Mgeni,” Ensign au Liahona, May 2016,13–15; “Sheria,” Ufunuo katika Muktatha, 93–95, history.ChurchofJesusChrist.org.

Picha
Kristo na Kijana Tajiri Mtawala

Kristo na Kijana Tajiri Mtawala, na Heinrich Hofmann

Mafundisho na Maagano 42:61–68; 43:1–16

Mungu anatoa ufunuo ili kuongoza Kanisa Lake.

Fikiria kwamba unaongea na muumini mpya wa Kanisa ambaye anafurahia kujua kwamba Kanisa linaongozwa na ufunuo. Ni kwa jinsi gani ungeweza kutumia Mafundisho na Maagano 43:1–16 kumwelezea mpangilio wa Bwana kwa ajili ya kuliongoza Kanisa Lake kupitia kwa nabii Wake? Ni kwa jinsi gani ungetumia Mafundisho na Maagano 42:61, 65–68 kufundisha kuhusu kupokea ufunuo binafsi?

Ona pia “Mambo Yote Yafanyike Katika Utaratibu”,” Funuo katika muktadha, 50–53, history.ChurchofJesusChrist.org.

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani

Mafundisho na Maagano 41:1–5.Ni ipi baadhi ya mifano ya sheria za kiraia, na ni kwa jinsi gani sheria hizi zinatunufaisha? Ni kwa jinsi gani sheria za Baba wa Mbinguni au amri zinatubariki? Wanafamilia wangechora picha zao wenyewe wakitii sheria za Mungu.

Mafundisho na Maagano 42:45, 88.Nini kingesaidia familia yako “kuishi pamoja kwa upendo”? (ona pia Mosia 4:14–15). Fikiria kuandika au kusema mambo chanya kuhusu nyinyi wenyewe au kuimba wimbo kuhusu upendo kwenye familia, kama vile “Upendo Nyumbani” (Nyimbo za Kanisa, na. 294).

Mafundisho na Maagano 42:61.Labda mngeweza kusoma mstari huu wakati mkiweka chemsha bongo pamoja. Tumia chemsha bongo kufundisha jinsi Mungu anavyofunua siri zake—“ufunuo juu ya ufunuo, maarifa juu ya maarifa.” Wanafamilia wangeweza kushiriki jinsi Mungu alivyofunua ukweli kwao kidogo kidogo.

Mafundisho na Maagano 43:25.Pengine kuna kitu fulani familia yako ingeweza kutumia kutengeneza sauti za radi kama njia ya kutambulisha majadiliano kuhusu mstari wa 25. Ni kwa jinsi gani sauti ya Bwana ni “sauti ya ngurumo za radi”? Pekueni mstari pamoja kwa ajili ya njia Bwana anazoweza kutuita kutubu. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa wasikivu zaidi kwa sauti ya Bwana?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “I Want to Live the Gospel,” Kitabu cha nyimbo za watoto,148; ona “Mawazo ya Kuboresha Kujifunza Maandiko Kwa Familia Yako.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Kuza mazingira ya upendo. Jinsi wanafamilia wanavyojisikia kuhusu kila mmoja na kutendeana kunaweza kushawishi kwa kina roho ya nyumbani kwenu. Wasaidie wanafamilia wote kufanya sehemu yao ili kustawisha nyumba yenye upendo, heshima ili kwamba kila mmoja ajisikie yu salama kuelezea uzoefu, maswali, na shuhuda zao. (Ona Kufundisha katika njia ya Mwokozi,15.)

Picha
Joseph Smith akihubiri

Joseph Smith Akihubiri Nauvoo, na Sam Lawlor

Chapisha