“Septemba 13–19. Mafundisho na Maagano 102–105: ‘Baada ya Taabu … Huja Baraka,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)
“Septemba 13–19. Mafundisho na Maagano 102–105,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021
Septemba 13–19
Mafundisho na Maagano 102–105
“Baada ya Taabu Nyingi … Huja Baraka”
Ni kanuni gani kutoka Mafundisho na Maagano 102–5 zina maana kwako? Fikiria kuandika mawazo yako na misukumo kuhusu kanuni hizi.
Andika Misukumo Yako
Watakatifu wa Kirtland walivunjwa mioyo kusikia kwamba kaka na dada zao wa Jackson County, Missouri, walikuwa wanafukuzwa kutoka nyumba zao. Lazima ilikuwa inatia moyo, wakati huo, wakati Bwana alipotangaza kwamba “ukombozi wa Sayuni” hauna budi “kuja kwa uwezo” (Mafundisho na Maagano 103:15). Kwa ahadi hiyo katika mioyo yao, zaidi ya wanaume 200, jumlisha wanawake kama 25 na watoto, walijisajili katika kile walichokiita Kambi ya Israeli, baadaye ilijulikana kama Kambi ya Sayuni. Kazi yake ilikuwa kutembea kwenda Missouri na kuikomboa Sayuni.
Kwa washiriki wa Kambi, kuikomboa Sayuni kulimaanisha kuwarejesha Watakatifu kwenye ardhi yao. Lakini punde kabla Kambi haijawasili Jackson County, Bwana alimwambia Joseph Smith kusimamisha na kuvunja Kambi ya Sayuni. Baadhi ya washiriki wa Kambi walitatizwa na kukasirishwa na maelekezo haya mapya; kwao, ilimaanisha msafara ulikuwa umeshindwa na ahadi za Bwana hazikutimia. Wengine, hata hivyo, waliona kitofauti. Wakati watakatifu waliofukuzwa kamwe hawakurudi Jackson County, uzoefu uliwaletea hatua ya “ukombozi” kwa Sayuni, na “ulikuja kwa uwezo.” Washiriki waaminifu wa kambi ya Sayuni, wengi wao baadaye walikuwa viongozi wa Kanisa, walishuhudia kwamba uzoefu uliongeza kwa kina imani yao katika uweza wa Bwana, katika wito mtakatifu wa Joseph Smith, na katika Sayuni—sio tu Sayuni ambayo ni sehemu bali Sayuni ambayo ni watu wa Mungu. Badala ya kuuliza thamani ya kazi hii iliyoonekana kutofanikiwa, walijifunza kwamba kazi halisi ni kumfuata Mwokozi, hata wakati hatuelewi kila kitu. Hivi ndivyo Sayuni, hatimaye, itakavyo kombolewa.
Ona Watakatifu, 1:194–206; “The Acceptable Offering of Zion’s Camp,” Ufunuo katika Muktadha, 213–18.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko
Mafundisho na Maagano 102:12–23
Ni nini lengo la maelekezo katika mistari hii?
Sehemu ya 102 ina mihutasari ya mkutano wa Kirtland, Ohio, ambako baraza kuu la kwanza la Kanisa lilianzishwa. Mistari ya 12–23 inaelezea taratibu zinazofuatwa na mabaraza makuu wakati wanapofanya mabaraza ya nidhamu kwa wale waliofanya makosa makubwa.
Rais M. Russell Ballard alifundisha, “Waumini wakati mwingine huuliza kwa nini mabaraza ya nidhamu ya Kanisa yanafanyika. Kusudi lina sehemu tatu: kuokoa roho ya mvunja sheria, kumlinda asiye na makosa, na kulinda usafi, uadilifu, na jina zuri la Kanisa” (Nafasi ya Kuanza tena: Mabaraza ya Nidhamu ya Kanisa na Urejesho wa Baraka,” Ensign, Sept. 1990, 15).
Ona pia Mada za Injili, “Mabaraza ya Nidhamu ya Kanisa,” topics.ChurchofJesusChrist.org.
Mafundisho na Maagano 103:1–12, 36; 105:1–19
Sayuni inaweza kujengwa tu juu ya kanuni za uadilifu.
Kwa nini Watakatifu walipoteza nchi yao ya ahadi huko Missouri? Na kwa nini Bwana hakuruhusu kambi ya Sayuni kuwarejesha kwenye ardhi yao? Kwa hakika matendo ya vurugu ya wavamizi wa Missouri yalisababisha, na gavana wa Missouri aliahidi msaada kwa Watakatifu lakini kamwe hakuutoa. Bali Bwana alisema kwamba “kama isingekuwa kwa ajili ya uvunjaji wa sheria wa watu wangu,” Sayuni “ingeweza kukombolewa” (Mafundisho na Maagano 105:2). Unaposoma Mafundisho na Maagano 103:1–12, 36; 105:1–19, unaweza kuona baadhi ya vitu ambavyo vilizuia kuanzishwa kwa Sayuni huko Missouri na vingine ambavyo vingeweza kusaidia. Unajifunza nini ambacho kinaweza kukusaidia kuanzisha Sayuni katika moyo wako na nyumbani?
Mafundisho na Maagano 103:12–13; 105:1–6, 13–19
Baraka zinakuja baada ya mateso na majaribu ya imani.
Katika njia nyingi, kushiriki katika Kambi ya Sayuni ilikuwa jaribu la imani. Safari ilikuwa ndefu, hali ya hewa ilikuwa ya joto, na chakula na maji vilikuwa wakati mwingine vichache. Na baada ya yote waliyovumilia, Watakatifu walikuwa bado hawawezi kurudi kwenye ardhi yao. Fikiria jinsi kanuni katika Mafundisho na Maagano 103:12–13 na 105:1–6, 13–19 ingeweza kuwasaidia washiriki wa Kambi ya Sayuni ambao walijiuliza kama amri ya kuanzisha kweli ilitoka kwa Mungu. Ni kwa jinsi gani kanuni hizi zinakusaidia katika majaribu yako binafsi ya imani?
Ungeweza pia kusoma kuhusu uzoefu wa washiriki wa Kambi ya Sayuni katika “Sauti za Urejesho” mwishoni mwa muhtasari huu. Kipi kinakuvutia kuhusu mitazamo yao? Je, mnaweza kujifunza nini kutokana na mifano yao?
Ona pia David A. Bednar, “Upande wa Bwana: Masomo Kutoka Kambi ya Sayuni,” Ensign, Julai 2017, 26–35.
Mafundisho na Maagano 104:11–18, 78–83
Mimi ni “msimamizi wa baraka za kidunia.”
Kwa kuongezea kwenye majaribu huko Missouri, mnamo 1834 kanisa lilikabiliwa na matatizo ya kifedha, pamoja na madeni makubwa na matumizi. Katika sehemu ya 104 Bwana alitoa ushauri kuhusu hali ya kifedha ya Kanisa. Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia kanuni katika mistari ya 11–18 na 78–83 kwa maamuzi yako ya kifedha?
Kujifunza kuhusu moja ya njia ambazo Bwana aliziandaa kwa ajili ya Kanisa kutolewa kutoka kwenye kifungo cha madeni, angalia “Treasure in Heaven: The John Tanner Story” (video ChurchofJesusChrist.org).
Kujifunza zaidi kuhusu “njia” ya Bwana (mstari wa 16) kutoa kwa Watakatifu Wake, unaweza kusoma ujumbe wa Rais Dieter F. Uchtdorf “Kutoa katika Njia ya Bwana” (Ensign au Liahona, Nov. 2011, 53–56).
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Nyumbani
-
Mafundisho na Maagano 103:12, 36; 105:9–13.Je, familia yako (au mmoja wa mababu zako) wamewahi wakati wowote kuombwa kufanya kitu fulani ambacho hakikuzaa matunda kwa njia uliyotegemea? Unaweza kujifunza nini kutoka kwenye majibu ya washiriki wa Kambi ya Sayuni wakati safari yao haikuwa kama walivyotegemea? (Ona “Sauti za Urejesho” mwishoni mwa muhtasari huu).
-
Mafundisho na Maagano 104:13–18. Je, Bwana ametupatia nini sisi? Je, Yeye anatarajia tufanye nini na vitu hivi?
-
Mafundisho na Maagano 104:23–46.Familia yako ingeweza kupekua mistari hii kutafuta ni mara ngapi Bwana anaahidi “kuzidisha baraka” (mstari wa 23) kwa wale ambao ni waaminifu. Inawezekana huu utakuwa muda mzuri wa “kuhesabu baraka zako” (“Hesabu Baraka Zako,” Nyimbo za Kanisa, na. 241) na jadili jinsi kufanya hivyo kungeweza kutusaidia wakati wa matatizo. Watoto wadogo wanaweza kufurahia kuchora picha za baraka ambazo hususani wana shukrani kwazo.
-
Mafundisho na Maagano 105:38–41.Tunawezaje kufanya “mapendekezo kwa ajili ya amani” (mstari wa 40) wakati wengine wanapotutendea bila huruma au bila haki? Tunaweza kufanya nini ili kuwa “bendera ya amani” (mstari wa 39) katika nyumba yetu?
Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.
Wimbo uliopendekezwa: “Hesabu Baraka Zako,” Nyimbo za Kanisa, na. 241.
Sauti za Urejesho
Kambi ya Sayuni
Kwa sababu Kambi ya Sayuni kamwe haikuwarejesha Watakatifu kwenye ardhi yao huko Jackson County, watu wengi walihisi kwamba jitihada zao zilishindwa. Hata hivyo, washiriki wengi wa Kambi ya Sayuni waliangalia nyuma kwenye uzoefu wao na waliona jinsi Bwana alivyokamilisha azma kuu katika maisha yao na katika ufalme Wake. Hapa ni baadhi ya shuhuda zao.
Joseph Smith
Zaidi ya miaka 40 baada ya Kambi ya Sayuni, Joseph Young, ambaye alikuwa mshiriki wa kambi, aliripoti kwamba Joseph Smith alisema yafuatayo:
“Ndugu, baadhi yenu mna hasira na mimi, kwa sababu hamkupigana Missouri; lakini acha niwaambieni, Mungu hakutaka ninyi mpigane. Hakuweza kuanzisha ufalme wake akiwa na wanaume kumi na wawili wakifungua mlango wa injili kwa mataifa ya dunia, pamoja na wanaume Sabini chini ya maelekezo yao ili kufuata katika nyayo zao, isipokuwa aliwachukua kutoka kundi la wanaume waliotoa maisha yao, na waliokwisha fanya dhabihu iliyo kubwa kama alivyofanya Ibrahimu.
“Sasa, Bwana amejipatia Kumi na Wawili na Sabini, na kutakuwepo na akidi zingine za Sabini zitakazoitwa, ambao watafanya dhabihu na hao ambao hawajafanya dhabihu zao na matoleo yao sasa, watazifanya baadaye.”1
Brigham Young
“Tulipofika Missouri Bwana alizungumza na mtumishi wake Joseph na alisema, ‘Nimeikubali dhabihu yenu,’ na tulikuwa na fursa ya kurudi tena. Niliporudi marafiki wengi waliniuliza kulikuwa na faida gani katika kuwaita wanaume kutoka kwenye kazi zao kwenda Missouri na kisha kurudi, bila kufanikisha chochote. ‘Imemfaidia nani?’ waliuliza. ‘Kama Bwana aliamuru ifanyike, alikuwa na maono ya jambo gani katika kufanya hivyo?’ … Niliwaambia ndugu hao kwamba nililipwa vizuri—nililipwa kwa riba kubwa—ndio kwamba kipimo changu kilijazwa mpaka kumwagika na ufahamu ambao niliupokea kwa kusafiri na Nabii.”2
Wilford Woodruff
“Nilikuwa katika Kambi ya Sayuni na Nabii wa Mungu. Niliona matendo ya Mungu kwake. Niliona nguvu ya Mungu kwake. Niliona kwamba alikuwa Nabii. Kilichodhihirishwa kwake kwa nguvu ya Mungu juu ya misheni ile kilikuwa cha thamani kubwa kwangu na kwa wote waliopokea maelekezo yake.”3
“Wakati washiriki wa Kambi ya Sayuni walipoitwa wengi wetu kamwe tulikuwa hatujawahi kuona sura za kila mmoja wetu; tulikua wageni kwa kila mmoja wetu na wengi kamwe hawakuwahi kumuona nabii. Tulikua tumetawanywa ughaibuni, kama mahindi yanavyochekechwa katika chekecheo, katika taifa zima. Tulikua vijana, na tuliitwa mapema siku hiyo kwenda na kukomboa Sayuni, na kile tulichotaka kufanya ilibidi tufanye kwa imani. Tulikusanyika pamoja kutoka majimbo tofauti pale Kirtland na tulikwenda kukomboa Sayuni, katika kukamilisha amri ya Mungu kwetu. Mungu alikubali kazi zetu kama alivyofanya kwa kazi za Ibrahimu. Tulikamilisha sehemu kubwa, ingawa waliokengeuka na wasioamini mara nyingi waliuliza swali ‘mmefanya nini?’ Tulipata uzoefu ambao kamwe tusingeweza kuupata [katika] njia nyingine yoyote. Tulikua na fursa ya kuuona uso wa nabii, na tulikuwa na fursa ya kusafiri maili elfu pamoja naye, na kuona kazi za roho wa Mungu kwake, na funuo za Yesu Kristo ndani yake na ukamilifu wa funuo hizo. Na aliwakusanya kiasi cha wazee mia mbili kutoka taifa zima mapema katika siku hiyo na alituletea tangazo kwa ulimwengu kuhubiri injili ya Yesu Kristo. Kama nisingeenda na Kambi ya Sayuni nisingeweza kuwa hapa leo [katika Jiji la Salt Lake, nikihudumu katika Akidi ya Kumi na Wawili]. … Kwa kwenda kule tuliwekwa kwenye shamba la mizabibu kuhubiri injli, na Bwana alikubali kazi zetu. Na katika kazi zetu zote na mateso, pamoja na maisha yetu mara nyingi yakiwa hatarini, ilitubidi tufanye kazi na kuishi kwa imani.”
“Uzoefu [sisi] tulioupata kwa kusafiri katika Kambi ya Sayuni ulikuwa wa thamani zaidi kuliko dhahabu.”