Mafundisho na Maagano 2021
Septemba 13–19. Mafundisho na Maagano 102–105: “Baada ya Taabu Kubwa … Huja Baraka”


“Septemba 13–19. Mafundisho na Maagano 102–105: ‘Baada ya Taabu Kubwa … Huja Baraka,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Septemba 13–19. Mafundisho na Maagano 102–105,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi: 2021

wanaume na mikokoteni ya kuvutwa na ng’ombe

C. C. A. Christensen (1831–1912), Kambi ya Sayuni, c. 1878, mchoro kwenye kitambaa cha pamba, inchi 78 ¼ × 114. Makumbusho ya Sanaa ya Chuo Kikuu cha Brigham Young, zawadi ya wajukuu wa C. C. A. Christensen, 1970

Septemba 13–19

Mafundisho na Maagano 102–105

“Baada ya Taabu Kubwa … Huja Baraka”

Kujifunza kwako Mafundisho na Maagano 102–5 ni sehemu muhimu ya maandalizi yako ya kufundisha. Sikiliza misukumo ya kiroho kuhusu namna ya kuwasaidia watoto kuyaelewa vyema maandiko.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Wasaidie watoto kuchagua wimbo wa kuimba ambao unawakumbusha jambo fulani walilojifunza nyumbani au kanisani.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mafundisho na Maagano 103:9

Ninaweza kuwa “nuru kwa ulimwengu.”

Ni kwa jinsi gani unaweza kuwatia moyo watoto unaowafundisha kushiriki nuru ya injili pamoja na wale wanaowazunguka?

Shughuli Yamkini

  • Soma Mafundisho na Maagano 103:9 kwa watoto, na waalike kushikilia picha ya balbu, mshumaa, au aina nyingine ya chanzo cha mwanga. Waombe waoneshe picha zao kwa mtu mwingine katika darasa. Waambie watoto ni kwa jinsi gani wao ni nuru kwa wengine pale wanapomfuata Yesu Kristo.

  • Imba wimbo pamoja na watoto kuhusu kuwa mfano, kama vile “Jesus Wants Me for a Sunbeam” au “I Am like a Star” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 60–61, 163). Wasaidie kufikiria vitendo ili viendane na maneno. Je, ni kwa namna gani sisi tunaweza kuwa nuru, au mfano mwema, kwa watu wanaotuzunguka?

    Mshumaa unawaka

    Ninaweza kuwa nuru kwa ulimwengu.

Mafundisho na Maagano 104:42

Bwana atanibariki kama ninashika amri Zake.

Mara kadhaa katika sehemu ya 104, Bwana anaahidi “wingi wa baraka” kwa wale wanaotii amri Zake kwa uaminifu. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kuona kwamba Yeye anataka kutubariki sisi kwa ukarimu?

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kufanya kitendo, kama vile kuchezesha chezesha vidole vyao, kila wakati wanaposikia neno “baraka” wakati unaposoma Mafundisho na Maagano 104:42. Waambie watoto jinsi Baba wa Mbinguni alivyokubariki wewe kwa kuwa umeshika amri Zake. Waombe watoto kushiriki jinsi Yeye alivyowabariki wao. Mwalike kila mtoto ashiriki amri ambayo wanaweza kutii.

  • Ili kuwasaidia watoto kujua “wingi” inamaanisha nini, chora duara ubaoni au kwenye kipande cha karatasi. Waombe watoto wakusaidie kuzidisha idadi ya miduara hiyo—wakichora miwili, kisha minne, halafu minane, kisha kumi na sita, na kuendelea—hadi ubao wote au karatasi ijae miduara hiyo. Kila wakati uongezapo mduara, wasaidie watoto kufikiria juu ya baraka ambayo Baba wa Mbinguni amewapatia. Eleza kwamba “wingi wa baraka” inamaanisha Bwana atajaza maisha yetu kwa baraka endapo tutatii amri Zake.

Mafundisho na Maagano 105:38–40

Ninaweza kuwa mpatanishi.

Kuna masomo mengi tunayoweza kujifunza kutokana na matukio ya Kambi ya Sayuni. Moja linaloweza kuwa muhimu kwa watoto ni kwamba mabishano na ugomvi huleta matatizo, wakati umoja na amani huleta baraka.

Shughuli Yamkini

  • Kwa maneno yako mwenyewe, wasimulie watoto hadithi ya Kambi ya Sayuni (ona utangulizi kwenye muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia; Watakatifu, 1:194–206; au “The Acceptable Offering of Zion’s Camp” [Revelations in Context, 213–18]). Simama mara kwa mara ili kuonesha masomo tunayoweza kujifunza kutokana na Kambi ya Sayuni—kwa mfano, kwamba Bwana anatutaka tuwe watulivu na tufanye kazi kwa pamoja badala ya kubishana na kugombana.

  • Soma Mafundisho na Maagano 105:38–40, na watake watoto kusimama kila wakati wanaposikia neno “amani.” Eleza kwamba Bwana aliwataka Watakatifu kupatana na watu waliokuwa wakiwafanyia ukatili. Wasaidie watoto kufikiria mambo ambayo wangeweza kufanya ili kuwa wapatanishi, na waalike kufanya maigizo ya baadhi ya hali hizo.

  • Simulia hadithi kuhusu mtoto kuwa mpatanishi kutoka kwenye maisha yako mwenyewe au kutoka kwenye Friend au Liahona. Imba wimbo kuhusu kuwapenda wengine, kama vile “Jesus Said Love Everyone” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 61), au kamilisha ukurasa wa shughuli ya wiki hii.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mafundisho na Maagano 104:13–18

Bwana ananitaka nishiriki kitu nilichonacho kwa kuwapa wenye shida.

Fikiria jinsi utakavyoweza kuwasaidia watoto kuelewa njia ya Bwana ya kuwasaidia watu wake wakati wawapo katika shida.

Shughuli Yamkini

  • Wape watoto dakika chache ili watengeneze orodha ya baraka ambazo Mungu amewapa. Wahamasishe waorodheshe nyingi kadiri wanavyoweza. Kisha someni pamoja Mafundisho na Maagano 104: 13–18, mkitafuta majibu ya maswali kama haya: Je, ni nani mmiliki wa kweli wa vitu vyote? Je, ni kwa nini Yeye anatupatia sisi? Je, Yeye anataka sisi tufanye nini na vitu hivi? Wasaidie watoto kufikiria njia wanazoweza kushiriki baraka zao na wengine.

  • Shiriki uzoefu ambapo mtu fulani alikupa wewe kitu ulichokuwa na shida nacho, na waombe watoto kushiriki uzoefu wa aina hiyo. Au onesha video inayohusu kuwahudumia wengine, kama vile “The Coat” (ChurchofJesusChrist.org). Je, tunajifunza nini kutokana na uzoefu huu kuhusu kuwahudumia wengine? Waalike watoto kuwatambua watu wenye shida na wamtafute mtu wa kumhudumia wiki hii, kama vile mtu fulani shuleni au hususani mtu katika familia zao.

  • Waalike watoto kupekua Kitabu cha Nyimbo za Watoto au Nyimbo za Kanisa kwa ajili ya nyimbo ambazo zinahusiana na huduma au kuwasaidia wengine (ona vielezo vya mada). Imbeni pamoja wimbo mmoja au mbili, na jadilianeni kuhusu nyimbo hizo zinatufundisha nini sisi.

Mafundisho na Maagano 105:9–19

Ninaweza kutii amri za Bwana hata wakati ambapo sielewi sababu zake.

Uzoefu wa Kambi ya Sayuni unaweza kuwa njia yenye nguvu ya kuelezea baraka ambazo huja kutokana na kutafuta kufuata mapenzi ya Bwana.

Shughuli Yamkini

  • Onesha picha katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia, na waalike watoto kushiriki kile wanachojua kuhusu Kambi ya Sayuni. Kama wanahitaji msaada, tumia utangulizi wa muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia; Watakatifu, 1:194–206; au “The Acceptable Offering of Zion’s Camp” (Revelations in Context, 213–18). Waalike watoto wajifanye kwamba wao walikuwa washiriki wa Kambi ya Sayuni, wakiwasimulia watoto wao kuhusu uzoefu wao. Je, ni kitu gani wangetaka watoto wao wajifunze kutokana na uzoefu huo?

  • Someni pamoja Mafundisho na Maagano 105:13–14, na eleza kwamba wakati Kambi ya Sayuni ilipofika Missouri, Bwana aliwaambia wasijaribu kurejesha ardhi iliyokuwa ya Watakatifu. Baadhi ya washiriki wa kambi walihamaki na kushangaa kwa nini walikuwa wameamriwa kwenda huko. Je, tunapaswa kufanya nini wakati tunapokuwa hatuelewi sababu ya amri? Simulia baadhi ya hadithi kutoka “Sauti za Urejesho: Kambi ya Sayuni” (katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia) ili kuwasaidia watoto kuona kwamba baraka huja wakati tunapotii amri Mungu anazotupa sisi kupitia manabii Wake, hata kama hatujui sababu zote.

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Wahimize watoto kushiriki na mtu nyumbani uzoefu wa Kambi ya Sayuni, sambamba na somo moja walilojifunza kutokana na uzoefu huo. Au waalike kufikiri juu ya kitu kimoja ambacho Mungu amewabariki nacho ambacho wanaweza kushiriki na mtu mwenye shida.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Kabiliana na usumbufu kwa upendo. “Mara nyingine mtoto hutenda katika njia ambazo huvuruga kujifunza kwa wengine darasani. Wakati hili linapotendeka, kuwa mvumilivu, mwenye upendo, na mwenye kuelewa kuhusu changamoto ambazo mtoto anaweza kuwa anakabiliana nazo. … Kama mtoto anayesababisha vurugu ana mahitaji maalumu, zungumza na mtaalamu wa watu wenye ulemavu katika kata au kigingi au tembelea [disabilities.ChurchofJesusChrist.org] ili kupata jinsi unavyoweza kutatua vyema tatizo hilo” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 26).