Mafundisho na Maagano 2021
Septemba 6–12. Mafundisho na Maagano 98–101: “Tulieni na Mjue Kuwa Mimi ni Mungu”


“Septemba 6–12. Mafundisho na Maagano 98–101: ‘Tulieni na Mjue Kuwa Mimi ni Mungu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Septemba 6–12. Mafundisho na Maagano 98–101,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi: 2021

Watakatifu wakilikimbia kundi la wasababisha vurugu

C. C. A. Christensen (1831–1912), Watakatifu wakifukuzwa kutoka Wilaya ya Jackson Missouri, c. 1878, mchoro kwenye kitambaa cha pamba, inchi 77 ¼ × 113. Makumbusho ya Sanaa ya Chuo Kikuu cha Brigham Young, zawadi ya wajukuu wa C. C. A. Christensen, 1970.

Septemba 6–12

Mafundisho na Maagano 98–101

“Tulieni na Mjue Kuwa Mimi ni Mungu”

Je, ni jumbe zipi watoto wa darasa lako wanahitaji kusikia wiki hii? Je, ni kwa namna gani kanuni zilizoko katika Mafundisho na Maagano 98–101 zitawasaidia wao kuwa wafuasi bora wa Yesu Kristo?

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Watie moyo watoto ili washiriki kitu walichojifunza nyumbani au katika Msingi kutoka kwenye Mafundisho na Maagano. Waulize ni kitu gani wanafurahia zaidi kuhusu kujifunza kutoka kwenye Mafundisho na Maagano.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mafundisho na Maagano 98:39–40

Ninaweza kuwasamehe wale wasio wakarimu kwangu.

Bwana aliwaomba Watakatifu waliokuwa wakiteswa huko Wilaya ya Jackson, Missouri, kuwasamehe wale waliowaumiza. Unapowafundisha watoto umuhimu wa msamaha, hakikisha wao pia wanaelewa kwamba kama mtu akiwaumiza, daima wanapaswa kumwambia mtu mkubwa wanayemwamini.

Shughuli Yamkini

  • Ili kuwasaidia watoto kuelewa changamoto ambazo Watakatifu katika Sayuni walikuwa wakikabiliana nazo, shiriki nao “Sura ya 34: Mungu Anawaonya Watu wa Sayuni” (Hadithi za Mafundisho na Maagano, 128–31, au video inayohusiana kwenye ChurchofJesusChrist.org). Soma Mafundisho na Maagano 98:39–40, na waombe watoto kusikiliza kile ambacho Bwana aliwaambia Watakatifu wakifanye wakati maadui zao watakapoomba msamaha. Je, ni kwa nini Bwana anatutaka sisi tuwasamehe watu, hata wale ambao si wakarimu kwetu?

  • Weka picha ya uso wa furaha kwenye ukuta mmoja na uso wa huzuni kwenye ukuta unaotazamana na wa kwanza. Shiriki na watoto hali tofauti ambapo mtu si mkarimu (unaweza kupata baadhi ya hadithi hizo katika Friend au Liahona). Pendekeza njia ambazo tungeweza kutoa mjibizo kwa matendo yasiyo ya ukarimu, na wasaidie watoto kuamua kama kila jibu lingeweza kuwafanya wafurahi au wahuzunike. Waalike watoto waoneshe kwa kidole ukutani picha ya uso inayohusiana.

Mafundisho na Maagano 101:16

Yesu Kristo anaweza kuniletea amani.

Wakati watakatifu walipokabiliwa na mateso, Bwana aliwafariji kwa kuwaambia, “Tulieni na jueni kuwa Mimi ni Mungu.” Fikiria ni kwa jinsi gani ushauri huu ungeweza kuwasaidia watoto unaowafundisha.

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto wajichezeshe chezeshe kwenye viti vyao. Kisha waambie watulie wakati unaponyanyua juu picha ya Mwokozi na kusema kifungu cha maneno “Tulieni na jueni kuwa Mimi ni Mungu” (Mafundisho na Maagano 101:16). Rudia shughuli hii mara kadhaa. Eleza kwamba wakati maisha yalipokuwa magumu kwa Watakatifu wakati wa Joseph Smith, Yesu aliwataka watulie na wamwamini Yeye badala ya kuwa na hofu. Ni kwa jinsi gani Yesu anaweza kutusaidia wakati tunapokuwa na wakati mgumu?

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu unyenyekevu, kama vile “Reverently, Quietly” au “To Think about Jesus” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 26, 71). Wasaidie watoto kutambua hisia za amani ambazo huja tunapokuwa tumetulia na kuwaza juu ya Yesu—kwa mfano, wakati tunaposali au tunaposhiriki sakramenti.

  • Wasaidie watoto kufanyia kazi ukurasa wa shughuli ya wiki hii. Wakati wakipaka rangi, waelezee jinsi gani kufikiria juu ya Yesu Kristo kumekusaidia wewe kuhisi amani hata katika nyakati ngumu.

    Yesu Kristo

    Maelezo kutoka Kristo na Kijana Tajiri Mtawala, na Heinrich Hofman

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mafundisho na Maagano 98:1–3, 11–14; 101:16

Majaribu yangu yanaweza kunisaidia mimi kuwa zaidi kama Yesu Kristo.

Wakati watoto wanakabiliana na changamoto maisha yao yote, watahitaji kuwa na imani kwamba Mwokozi anaweza kuwasaidia wakati wa majaribu yao na kwamba majaribu hayo yanaweza “kufanya kazi pamoja kwa faida yao” (Mafundisho na Maagano 98:3).

Shughuli Yamkini

  • Waombe watoto wakusaidie kutengeneza orodha ubaoni ya baadhi ya changamoto ambazo mtoto wa umri wao anaweza kukabiliana nazo. Waambie watoto kuhusu baadhi ya changamoto za Watakatifu walioishi katika Wilaya ya Jackson, Missouri, mnamo mwaka 1833 (ona Sura ya 34 na 35 katika Hadithi za Mafundisho na Maagano, 128–34). Je, ni ushauri gani wangeutoa kwa mtoto anayepitia changamoto hizi? Waombe watoto wasome Mafundisho na Maagano 98:1–3, 11–14, wakitafuta mwongozo ambao Bwana aliutoa. Je, ni kwa jinsi gani wao wanaweza kufuata ushauri huu wakati wakikabiliana na changamoto kama hizo zilizoorodheshwa ubaoni?

  • Waalike watoto kutulia na kukaa kimya kadiri wawezavyo kwa dakika chache wakati huo wakiangalia picha ya Mwokozi au wakisikiliza wimbo juu Yake. Kisha waalike kushiriki kile walichohisi na kukipitia wakati wa kutulia huko. Soma Mafundisho na Maagano101:16. Ni jinsi gani kutulia na kufikiria juu ya Yesu kunatusaidia sisi? Wasaidie watoto kuelewa muunganiko baina ya utulivu wa unyenyekevu na uwezo wetu wa kumsikia Roho na kufikiria juu ya Yesu.

Mafundisho na Maagano 98:23, 39–40

Yesu ananitaka niwasamehe wale wasio wakarimu kwangu.

Tumeamriwa kupendana, kuwasamehe wengine “saba mara sabini” na kugeuza shavu jingine (ona Mathayo 5:39, 43–44; 18:21–22). Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia mistari hii kuwafundisha watoto kweli hizi?

Shughuli Yamkini

  • Waambie watoto juu ya mateso ambayo yalitokea katika Wilaya ya Jackson, Missouri, mnamo mwaka 1833 (ona sura ya 34 na 35 katika Hadithi za Mafundisho na Maagano, 128–34). Waulize watoto ni jinsi gani wangejisikia kama wao wangekuwa waumini wa Kanisa wa wakati huo. Waalike kusoma Mafundisho na Maagano 98:23, 39–40 kutafuta kile ambacho Bwana aliwataka Watakatifu wafanye. Je, ni kwa nini inaweza kuwa vigumu kuwasamehe wale waliotuumiza? Je, ni kwa jinsi gani tunabarikiwa tunapofanya hivyo?

  • Waulize watoto kama wanaweza kufikiria wakati ambapo Yesu Kristo au mtu mwingine katika maandiko alifanya kile Mafundisho na Maagano 98:23 inachofundisha. Ili kuwapa mfano mmoja, onesha picha ya Kusulubiwa (kama vile Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 57). Waombe watoto washiriki na wengine kile wanachokijua kuhusu Kusulubuwa kwa Mwokozi (ona Luka 23). Waalike kusoma Luka 23:34. Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kufuata mfano wa Yesu Kristo?

Mafundisho na Maagano 101:23–32, 36, 38

Kupitia Yesu Kristo ninaweza kupata shangwe.

Maisha hayajakusudiwa kutokuwa na ugumu, lakini unaweza kuwasaidia watoto kugundua kwamba bado wanaweza kupata utimilifu wa shangwe kupitia Yesu Kristo.

Shughuli Yamkini

  • Weka maji katika kikombe. Waombe watoto wataje mambo ambayo Mwokozi amefanya kwa ajili yetu ili sisi tuwe na shangwe, na waalike kudondosha changarawe moja katika kikombe hicho kwa kila jambo wanalotaja hadi kikombe kijae. Soma pamoja na watoto Mafundisho na Maagano 101:36, na waombe watafute ni kwa namna gani tunaweza kuwa na utimilifu wa shangwe. Je, nini baadhi ya mambo tunayoweza kufanya ili “kumtafuta … Bwana” (mstari wa 38) ili tuweze kuwa na shangwe Yeye anayotaka sisi tuwe nayo?

  • Eleza kwamba Mafundisho na Maagano 101:23–32 inafundisha kuhusu maisha yatakavyokuwa wakati Yesu atakapokuja tena. Mnaposoma mistari hii pamoja, zungumzia kuhusu mambo watoto wanayopata ambayo yatatuletea shangwe wakati Yeye atakapokuja. Je, kwa nini inasaidia kujua kuhusu mambo haya wakati tunapokuwa na wakati mgumu?

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Wasaidie watoto kuchagua mstari kutoka Mafundisho na Maagano 98–101 ambao wangependa kushiriki pamoja na familia zao. Wasaidie kupanga namna watakavyoshiriki na wengine kile wanachokipenda kutoka kwenye mstari huo.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Jiboreshe kama mwalimu aliye kama Kristo. Tafakari juu ya njia unazoweza kuwa mwalimu kwa mfano wa Kristo. Fikiria kutumia maswali ya kujitathimini binafsi kwenye ukurasa wa 37 wa Kufundisha katika Njia ya Mwokozi ili kukusaidia kujiboresha.