Mafundisho na Maagano 2021
Agosti 30–Septemba 5. Mafundisho na Maagano 94–97: “Kwa ajili ya Wokovu wa Sayuni”


“Agosti 30–Septemba 5. Mafundisho na Maagano 94–97: ‘Kwa ajili ya Wokovu wa Sayuni,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Agosti 30–Septemba 5. Mafundisho na Maagano 94–97,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021

Hekalu la Kirtland

Hekalu la Kirtland, na Al Rounds

Agosti 30–Septemba 5

Mafundisho na Maagano 94–97

“Kwa Ajili ya Wokovu wa Sayuni”

Ni kanuni zipi na mafundisho yapi yanajitokeza kwako unapojifunza Mafundisho na Maagano 94–97? Hakikisha kuandika misukumo yako.

Andika Misukumo Yako

Wakati Bwana alipomuamuru Musa kujenga hema ya kukutania, Alimwambia Musa “kufanya vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa [kwake] katika mlima.” (Waebrania 8:5; ona pia Kutoka 25:8–9). Hema ya kukutania ilikuwa iwe ni sehemu ya katikati ya kambi ya Israeli nyikani (ona Hesabu 2:1–2). Baadaye, Mungu alimuamuru Sulemani na watu wake kujenga hekalu kulingana na mpangilio Aliouonesha (ona 1 Mambo ya Nyakati 28:12,19).

Bwana aliporejesha utimilifu wa injili, Alimwamuru Joseph Smith kujenga mahekalu kuligana na mpangilio uliofunuliwa. “Nyumba na ijengwe, siyo kwa jinsi ya ulimwengu,” Bwana alitangaza. “Na ijengwe kwa jinsi ambayo nitaionyesha” (Mafundisho na Maagano 95:13–14.; ona pia 97:10). Kama hema ya kukutania katika nyika, hekalu lilikusudiwa kuwa sehemu ya katikati mwa Kirtland (ona Mafundisho na Maagano 94:1).

Leo nyumba za Bwana zinapatikana ulimwenguni kote. Hata kama hazipo katikati ya majiji yetu, zinaweza kuwa katikati ya maisha yetu. Ingawa kila hekalu linatofautiana katika mwonekano, ndani yake tunajifunza mpangilio mtakatifu ulio sawa—mpango wa kimbingu wa kuturudisha kwenye uwepo wa Mungu. Ibada takatifu, za milele zinatusaidia kujenga maisha yetu na kuimarisha familia zetu “si kulingana na jinsi ya ulimwengu” bali kwa mpangilio ambao Mungu anatuonyesha.

Ona Watakatifu, 1:169–70.; “Nyumba kwa ajili ya Mungu Wetu,” Ufunuo katika Muktadha, 165–73.

ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Mafundisho na Maagano 94; 97:15–17

Bwana anaweza kuwa nami katika maisha yangu ya kila siku.

Maelekezo katika Mafundisho na Maagano 94 na 97 yalitolewa siku moja—Agosti 2, 1833. Sehemu ya 97 inahusika kwa kiasi na hekalu lililopangwa kwa ajili ya Jackson County, Missouri, wakati sehemu ya 94 inahusika na majumba ya utawala huko Kirtland, Ohio. Unaweza kuona baadhi ya mifanano kwa kile Bwana anachokisema kuhusu aina hizi tofauti za majengo (ona Mafundisho na Maagano 94:2–12; 97:10–17). Unapotafakari maelekezo haya, fikiria nini unaweza kufanya kupata uzoefu wa utukufu na uwepo wa Bwana mara nyingi, kote ndani ya majengo ya Kanisa na katika maisha yako ya kila siku.

Mafundisho na Maagano 95

Bwana huwarudi wale Anaowapenda.

Karibia miezi mitano ilikuwa imepita tangu Januari 1833, wakati Bwana alipowaamuru Watakatifu waliopo Kirtland kujenga nyumba ya Mungu na kufanya mkutano wa ibada (ona Mafundisho na Maagano 88:117–19). Wakati ufunuo uliorekodiwa katika sehemu ya 95 ulipopokelewa mnamo Juni 1833, walikuwa bado hawajafanyia kazi amri hiyo. Unajifunza nini kutokana na jinsi Bwana alivyowarudi Watakatifu katika ufunuo huu? Je, kuna amri au maneno ya ushauri ambayo bado hujayafanyia kazi? Je, unashawishika kufanya nini?

Ona pia D. Todd Christofferson (“Kadiri ya Wengi Niwapendao, Ninawakemea na Kuwarudi,” Ensign au Liahona, Mei 2011, 97–100.

Mafundisho na Maagano 95:8, 11–17; 97:10–17

Katika Hekalu Mungu hubariki watu Wake.

Baada ya kuwarudi kwa kutokuijenga nyumba ya Bwana huko Kirtland, viongozi wa Kanisa walitafuta eneo kwenye shamba la ngano ambako wangejenga. Hyrum Smith, Kaka wa Nabii, mara moja alikimbia kuchukua fyekeo na kuanza kulishafisha shamba. “Tunatayarisha kujenga nyumba kwa ajili ya Bwana,” alisema, “na nimeamua kuwa wa kwanza kazini” (katika Mafundisho ya Marais wa Kanisa: Joseph Smith [2007], 271, 273). Tafakari ari ya Hyrum unaposoma, Mafundisho na Maagano 95:8, 11–17; 97:10–17. Unapata nini ambacho kinachochea msukumo sawa na huo ndani yako wa kupokea baraka za hekalu?

Hyrum Smith ameshikilia fyekeo

Hyrum Smith Akisafisha Ardhi, na Joseph Brickey

Mafundisho na Maagano 97:18–28

Sayuni ni “wasafi katika moyo.”

Nabii Joseph Smith alifundisha, “Tunapaswa kuwa na ujengaji wa Sayuni kama jambo kuu zaidi kwetu” (Mafundisho: Joseph Smith, 186). Kwa Watakatifu katika miaka ya 1830, Sayuni ilikuwa mahali, “Jiji halisi la Mungu wetu” (Mafundisho na Maagano 97:19). Lakini katika ufunuo uliorekodiwa katika sehemu ya 97, Bwana alikuza mtazamo ule. Sayuni pia inaelezea watu—“walio safi moyoni” (mstari wa 21). Unaposoma mistari ya 18–28, fikiria kuhusu ufafanuzi huu wakati unaposoma neno “Sayuni.” Inamaanisha nini kwako kuwa msafi moyoni? Ni kwa jinsi gani hekalu linasaidia kukamilisha “wokovu wa Sayuni”? (mstari wa 12).

Ona pia Musa 7:18; Mada za Injili, “Sayuni,” topics.ChurchofJesusChrist.org.

ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Nyumbani

Mafundisho na Maagano 95:8.Ni kwa jinsi gani kufanya na kutunza maagano ya hekaluni kumeleta “nguvu kutoka juu” kwenye maisha yetu? Pengine wanafamilia wangeweza kushiriki jinsi wanavyojisikia kuhusu hekalu au kushiriki uzoefu wakati walipojisikia kubarikiwa na “nguvu kutoka juu” kupitia kuabudu katika hekalu.

Ili kuwasaidia wale wanaojiandaa kuingia hekaluni, ungeweza kurejea video, picha, na maelekezo yanayopatikana kwenye temples.ChurchofJesusChrist.org. Ili kuwasaidia watoto kujifunza kuhusu hekalu, ungeweza kutumia “Njia Yako kuelekea Hekaluni” (ndani ya Mahekalu ya Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho [toleo maalumu la Ensign au Liahona, Okt. 2010], 72–75).

Mafundisho na Maagano 95:1–11.Tunajifunza nini kuhusu kukemewa kutoka kwenye mistari hii? Tunajifunza nini kuhusu Bwana? Ni jinsi gani utambuzi huu unaathiri jinsi tunavyopokea yale tuliyokemewa au kuwakemea wengine?

Mafundisho na Maagano 97:8.Kulingana na mstari huu, ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa “waliokubaliwa na” Bwana? Ni kwa jinsi gani hiyo ni tofauti na kukubaliwa na ulimwengu? Inamaanisha nini “kuyatunza maagano [yetu] kwa dhabihu”? Ni jinsi gani tumefanya hivi?

Mafundisho na Maagano 97:10–21.Nabii Joseph Smith alifundisha, “Sehemu yoyote ambapo Watakatifu watakusanyika ni Sayuni, ambapo kila mwanamume mwadilifu [au mwanamke] atajenga kwa ajili ya sehemu ya usalama kwa watoto wake” (Mafundisho: Joseph Smith, 186). Ni kwa jinsi gani tunaweza kujenga Sayuni ndani ya nyumba yetu? Ni kanuni zipi tunazipata katika Mafundisho na Maagano 97:10–21? Kama familia, chagueni kanuni ya kuifokasia wiki hii.

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “I Love to See the Temple,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 95.

Kuboresha Kujifunza Binafsi

Andika uzoefu wako. Andika uzoefu uliowahi kuwa nao kwenye kanuni na mafundisho unayojifunza kuyahusu. Uzoefu huu unaweza kuwa sehemu ya historia binafsi ambayo itabariki vizazi vijavyo.

Ujenzi wa hekalu la Kirtland

Kujenga Hekalu la Kirtland, na Walter Rane