Mafundisho na Maagano 2021
Septemba 20–26. Mafundisho na Maagano 106–108: “Mbingu Kufunuliwa”


“Septemba 20–26. Mafundisho na Maagano 106–108: ‘Mbingu Kufunuliwa,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Septemba 20–26. Mafundisho na Maagano 106–108,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021

Picha
jua likiangaza mawinguni

Septemba 20–26

Mafundisho na Maagano 106–108

“Mbingu Kufunuliwa”

Mzee Ulisses Soares alifundisha, “Tunahitaji kukaa kwa [Mwokozi], tukijikita katika maandiko, tukiyafurahia, tukijifunza mafundisho Yake, na kujitahidi kuishi jinsi Alivyoishi” (“Ni jinsi gani Ninaweza Kuelewa?Ensign au Liahona, Mei 2019, 7). Unapojikita mwenyewe katika Mafundisho na Maagano 106–8, andika jinsi unavyoweza kujitahidi kuishi kweli ulizozigundua.

Andika Misukumo Yako

Kwa mtazamo wa kwanza, Mafundisho na Maagano 107 inaweza kuonekana kuwa tu kuhusu kuratibu ofisi za ukuhani kwenye muundo wa uongozi kwa ajili ya Kanisa la Bwana. Kwa kweli, wakati ufunuo huu ulipochapishwa, uumini wa Kanisa ulikuwa tayari unapita uwezo wa viongozi wachache waliokuwepo. Kwa hiyo kuelezea kwa muhtasari majukumu na wajibu wa Urais wa Kwanza, Akidi ya Wale Kumi na Wawili, Sabini, maaskofu, na urais wa akidi kwa hakika kulikuwa kunahitajika na ilisaidia. Bali kuna mengi zaidi kwenye maelekezo matakatifu katika sehemu ya 107 kuliko tu jinsi ya kuratibu ofisi za ukuhani na akidi. Hapa Bwana anatufundisha kuhusu utaratibu wa kale wa ukuhani ambao ulikuwa “umeanzishwa katika siku za Adamu” (mstari wa 41). Madhumuni yake toka mwanzo yamekuwa kufanya iwezekane kwa watoto wa Mungu—pamoja na wewe—kupokea ibada za wokovu za injili na kufurahia “baraka zote za kiroho za kanisa—kuwa na haki ya kupokea siri za ufalme wa mbinguni, [na] mbingu kufunuliwa kwao” (mistari 18–19).

Ona “Kurejesha Utaratibu wa Kale,” Ufunuo katika Muktadha, 208–12.

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Mafundisho na Maagano 106108

Bwana huwaelekeza, huhimiza, na kuwasaidia wale ambao Yeye anawaita kuhudumu.

Katika Mafundisho na Maagano 106 na 108, Bwana alitoa ushauri na ahadi kwa waumini wawili walioitwa kuhudumu katika Kanisa. Ni virai gani katika ufunuo huu vinatoa hamasa na umaizi kuhusu huduma yako katika ufalme wa Mungu? Hivi ni viwili vya kuzingatia:

Ni virai gani vingine kutoka sehemu ya 106 na 108 vina maana kwako?

Ona pia Russell M. Nelson, “Kuhudumu kwa Nguvu na Mamlaka ya Mungu,” Ensign au Liahona, Mei 2018, 68–75; “Warren Cowdery,” Ufunuo katika Muktadha, 219–23; “‘Wrought Upon’ to Seek a Revelation,” Ufunuo katika Muktadha, 224–28.

Mafundisho na Maagano 107

Bwana huliongoza Kanisa Lake kupitia mamlaka ya ukuhani.

Wakati ulipojifunza Urejesho wa injili, huenda uligundua kwamba Bwana kwa kawaida haelezi mafundisho kikamilifu katika ufunuo mmoja. Badala yake, Anafunua vitu “mstari juu ya mstari” (Mafundisho na Maagano 98:12) wakati hali inapohitaji. Ingawa Bwana hapo mwanzo alitoa maelekezo kuhusu ukuhani mapema mnamo 1829 (ona, kwa mfano, sehemu ya 20 na 84), Alitoa maelekezo ya ziada kwa Watakatifu mnamo mwaka 1835 kuhusu ofisi maalumu za ukuhani zilizohitajika kusimamia na kuongoza kundi lake lililokuwa linaongezeka.

Unaposoma kuhusu ofisi za ukuhani zifuatazo, fikiria jinsi unavyoweza kuwathibitisha wale wanaohudumu katika miito hii “kwa kuaminiwa kwako, imani, na sala” (Mafundisho na Maagano 107:22).

Mafundisho na Maagano 107:1–20

Ibada za ukuhani zinatoa baraka za kiroho na kimwili kwa watoto wote wa Baba wa Mbinguni.

Mzee Neil L. Andersen alifundisha: “Ukuhani ni nguvu na mamlaka ya Mungu yaliyotolewa kwa ajili ya wokovu na baraka kwa wote—wanaume, wanawake, na watoto. … Tunapostahili, ibada za ukuhani zinarutubisha maisha yetu hapa duniani na kutuandaa kwa ajili ya ahadi adhimu za ulimwengu ujao” (“Nguvu katika Ukuhani,” Ensign au Liahona, Nov. 2013, 92). Unaposoma Mafundisho na Maagano 107:1–20 (ona hasa mistari 18–20) na sehemu yote iliyobakia ya ujumbe wa Mzee Andersen, fikiria kuandika misukumo unayopokea kuhusu jinsi nguvu za Mungu zinavyorutubisha maisha yako duniani na zinavyokuandaa kwa ajili ya maisha ya milele. Unafanya nini kupokea kikamilifu zaidi—na kusaidia wengine kupokea—baraka hizo?

Ona pia Mafundisho na Maagano 84:19–27; Dallin H. Oaks, “Ukuhani wa Melkizedeki na Funguo,” Ensign au Liahona, Mei 2020, 69–72.

Mafundisho na Maagano 107:41–57

Ukuhani unabariki familia.

Adamu alitaka uzao wake ubarikiwe na ukuhani. Ni ahadi zipi alizipokea? (Ona mistari 4255). Unaposoma kuhusu nini Adamu alifanya, fikiria matamanio yako binafsi kwa ajili ya familia yako kufurahia baraka za ukuhani. Je unavuviwa kufanya nini ili kusaidia familia yako ipokee baraka hizi?

Picha
Adamu akibariki uzao wake

Adamu Akibariki Uzao Wake, na Clark Kelley Price

Picha
ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Mafundisho na Maagano 106:6.Familia yetu inaweza kufanya nini kusababisha “shangwe mbinguni”?

Mafundisho na Maagano 107:22.Nini tunafanya kuwathibitisha viongozi wetu “kwa … ujasiri, imani, na sala”?

Mafundisho na Maagano 107:27–31, 85.Kanuni zinazoongoza mabaraza ya Kanisa zinaweza pia kutusaidia kushauriana pamoja kama familia. Ni kanuni zipi katika mistari hii tunaweza kuzitumia kwenye mabaraza ya familia zetu? (Ona M. Russell Ballard, “Mabaraza ya Familia,” Ensign au Liahona, Mei 2016, 63–65.)

Mafundisho na Maagano 107:99–100.Mpe mwanafamilia maelekezo yaliyoandikwa kwa ajili ya kazi ya nyumbani, na mwalike kuchagua jinsi ya kufanya kazi hiyo: kwa bidii, kivivu, au bila kusoma maelekezo. Ruhusu familia nzima imwangalie akifanya kazi na kukisia mtazamo gani mwanafamilia amechagua. Kisha ruhusu wanafamilia wengine wafanye kwa zamu. Kwa nini Bwana anatutaka sisi kujifunza majukumu yetu na kuyafanya kwa bidii? (Ona Becky Craven, “Makini dhidi ya Kawaida,” Ensign au Liahona, Mei 2019, 9–11.)

Mafundisho na Maagano 108:7.Ni kwa jinsi gani tunaweza kuimarishana katika mazungumzo yetu? katika sala zetu? katika ushawishi, au kutiana moyo? katika matendo yetu yote? Unaweza kuchagua moja ya hizi kufanyia kazi kama familia.

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “We Listen to a Prophet’s Voice,” Nyimbo za Kanisa, na. 22.

Kuboresha Kujifunza Binafsi.

Andika Misukumo. Wakati misukumo ya kiroho au utambuzi unapokujia, viandike. Unapofanya hivyo, unamwonyesha Bwana kwamba unathamini maelekezo Yake. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 1230.)

Picha
Melkizedeki akimbariki Abramu

Melkizedeki Akimbariki Abramu, na Walter Rane

Chapisha