Mafundisho na Maagano 2021
Septemba 27–Oktoba 3. Mafundisho na Maagano 109–110: “Ni Nyumba Yako, Mahali pa Utakatifu Wako”


“Septemba 27–Oktoba 3. Mafundisho na Maagano 109–110: ‘Ni Nyumba Yako, Mahali pa Utakatifu Wako,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Septemba 27–Oktoba 3. Mafundisho na Maagano 109–110,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021

Picha
Hekalu la Kirtland

Hekalu la Kirtland, na Jon McNaughton

Septemba 27–Oktoba 3

Mafundisho na Maagano 109–110

“Ni Nyumba Yako, Mahali pa Utakatifu Wako”

Akirejelea kwenye Mafundisho na Maagano 109:24–28, Mzee David A. Bednar alisema, “Ninawaalika kujifunza mara kwa mara na kutafakari kwa sala athari za maandiko haya katika maisha yako na kwa ajili ya familia yako” (“Honorably Hold a Name and Standing,” Ensign au Liahona, Mei 2009, 99). Fikiria mwaliko huu unapojifunza.

Andika Misukumo Yako

Milango kwenye Hekalu la Kirtland haikutakiwa kufunguliwa mpaka saa 2:00 asubuhi ya Machi 27, 1836. Lakini Watakatifu waliotegemea kuhudhuria huduma za kuweka wakfu walianza kujipanga mapema mathalani saa 1:00. Wakati mabenchi na njia baina ya viti zilipojaa kwa haraka kwa waumini wenye ari, Joseph Smith alipendekeza mahali maalumu kwa waliofurika. Wakati sehemu ile ilipojaa, kikao cha pili kilipangwa. Na haikuwa walio hai tu waliokuwa na ari ya kuwepo. Mashahidi wengi walishuhudia kwamba waliwaona malaika, ndani ya hekalu na hata kwenye paa, wakati na baada ya kuwekwa wakfu. Kwa kweli ilionekana kwamba “majeshi ya mbinguni” yalikuwa yamekuja “kuimba na kupaza sauti” pamoja na Watakatifu wa Siku za Mwisho (“Roho wa Mungu,” Nyimbo za Kanisa, na. 2).

Kwa nini shangwe kuu—pande zote mbili za pazia? Ahadi kwamba Watakatifu “watajaliwa uwezo kutoka juu” ilikuwa sababu moja ya wao kukusanyika Ohio kwa mara ya kwanza (Mafundisho na Maagano 38:32). Na mambo makuu mno yaliahidiwa kwa ajili ya siku za baadaye. “Huu,” Bwana alitangaza, “ni mwanzo wa baraka ambayo itamwagwa juu ya vichwa vya watu wangu” (Mafundisho na Maagano 110:10). Enzi tunayoishi sasa—na uharakishaji wa kazi ya hekaluni na ibada zinazopatikana kwa mamilioni ya wanaoishi na wafu—ilikuwa na mwanzo wake huko Kirtland, wakati “pazia juu ya dunia [lilikuwa] linaanza kufunguka” (“Roho wa Mungu”).

Ona pia Saints, 1:232–41.; “Nyumba kwa ajili ya Mungu Wetu,” Ufunuo katika Muktadha, 169–72.

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Mafundisho na Maagano 109

Bwana anataka kunibariki katika nyumba Yake takatifu.

Katika jinsi fulani, Hekalu la Kirtland lilikuwa tofauti na mahekalu tunayoyajua leo. Hapakuwa na madhabahu na hapakuwa na kisima cha kubatizia, na ibada kama ubatizo kwa ajili ya wafu na kuunganisha vilikuwa bado havijarejeshwa. Lakini baraka zinazoelezwa katika sehemu ya 109, sala ya kuweka wakfu kwa ajili ya Hekalu la Kirtland, ni baraka tunazopokea katika nyumba ya Bwana leo. Rejea mistari ifuatayo kuona baadhi ya baraka hizi. Unaposoma kuhusu baraka hizo, tafakari kwa nini ni za muhimu kwako na familia yako.

Mistari 5, 12–13 (ona pia Mafundisho na Maagano 110:6–8): ndani ya hekalu Bwana anaweza kujidhihirisha Mwenyewe kwetu na tunaweza kuhisi nguvu Zake.

Mistari 9, 17–19, 26, 78–79: Ndani ya hekalu tunajichukulia juu yetu jina la Bwana.

Mistari 22–23: Tunapofanya na kuheshimu maagano ya hekaluni, Bwana anatupatia nguvu ya kufanya kazi Yake.

Mistari 24–33: Tunapohudhuria hekaluni kwa kustahili, tunaweza kupokea ulinzi wa Bwana.

Baraka nyingine:

Je, Roho anakuvuvia kufanya nini ili kupokea baraka hizi?

Mafundisho na Maagano 109

Sala ya kuweka wakfu Hekalu la Kirtland inaweza kunifundisha mimi kuhusu sala.

Sehemu ya 109 ni sala ya kuweka wakfu ambayo Joseph Smith alipewa kwa ufunuo (ona kichwa cha habari cha sehemu). Unajifunza nini kuhusu sala kutoka sehemu hii? Unapoisoma, unaweza kufikiria kuhusu sala zako mwenyewe. Ni misukumo gani unaipokea ambayo inaweza kukusaidia kuboresha mawasiliano yako na Baba wa Mbinguni? Kwa mfano, Nabii aliomba kuhusu nini katika sala hii?

Mafundisho na Maagano 110:1–10

Bwana anaweza kujidhihirisha Mwenyewe kwangu katika hekalu.

Ni kwa jinsi gani unahisi kuhusu Mwokozi baada ya kusoma Mafundisho na Maagano 110:1–10? Ni kwa jinsi gani Amejidhihirisha Mwenyewe kwako katika hekalu? Ni kwa njia zipi Anakusaidia wewe kujua kwamba Anakubali juhudi na dhabihu zako?

Picha
Hekalu la Kirtland kwa ndani

Kila kona ya Hekalu la Kirtland ina mimbari kwa ajili ya viongozi wa ukuhani.

Mafundisho na Maagano 110:11–16

Funguo za ukuhani zinazohitajika kukamilisha kazi ya Mungu zipo Kanisani leo hii.

Kuzielewa funguo za ukuhani ambazo Musa, Elia, na Eliya walizikabidhi kwa Joseph Smith na Oliver Cowdery ndani ya Hekalu la Kirtland, unaweza kusoma ujumbe wa Mzee Quentin L. Cook “Jitayarishe Kukutana na Mungu” (Ensign au Liahona, Mei 2018, 114–17). Mzee Cook alielezea jinsi funguo hizi zinavyoendana na kazi ya Kanisa leo. Unaweza pia kufikiria kujifunza kuhusu manabii hawa wa kale kwa kusoma “Musa,” “Elia,” na “Eliya” katika Mwongozo kwenye Maandiko (scriptures.ChurchofJesusChrist.org). Tafakari kile unachoweza kufanya ili kusaidia katika kazi inayohusiana na funguo hizi.

Ona pia “Priesthood Keys,” True to the Faith, 126–27; Henry B. Eyring, “He Goes before Us,” Ensign au Liahona, Mei 2020, 66–69.

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Nyumbani

Mafundisho na Maagano 109.Kama familia, tafuteni baadhi ya mistari katika sehemu ya 109 ambayo inawavuvia kutumia muda zaidi katika hekalu (kwa mfano, ona mistari iliyoorodheshwa kwenye “Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko”). Zungumza kuhusu jinsi unavyoweza kufanya kile Rais Russell M. Nelson alichopendekeza: “Tafuta njia ya kuweka ahadi ya mara kwa mara na Bwana—kuwa katika nyumba Yake takatifu—na kisha tunza ahadi hiyo kwa usahihi na kwa shangwe” (“Kuwa Mtakatifu wa Siku za Mwisho wa Mfano,” Ensign au Liahona, Nov. 2018, 114). Kama wewe au familia yako hamjawahi kuhudhuria hekaluni, mnaweza kutembelea temples.ChurchofJesusChrist.org ili kuwasaidia kujiandaa kwa ajili ya kwenda.

Mafundisho na Maagano 109:78–80.Wimbo “Roho wa Mungu” (Nyimbo za Kanisa, na. 2) uliandikwa kwa ajili ya kuwekwa wakfu Hekalu la Kirtland—na umekuwa ukiimbwa tangu wakati huo kwenye kuwekwa wakfu kwa kila hekalu. Mnaweza kuimba wimbo huu kwa pamoja na kutafuta virai ambavyo vinaongeza shukrani zenu kwa ajli ya mahekalu ya siku za mwisho. Ni kwa jinsi gani wimbo huu unahusiana na ujumbe wa Mafundisho na Maagano 109:78–80?

Unaweza kupata sala ya kuwekwa wakfu kwa hekalu karibu sana na wewe kwenye temples.ChurchofJesusChrist.org.

Mafundisho na Maagano 110.Wakati wanafamilia yako wanaposoma sehemu ya 110 na kutazama picha mwishoni mwa muhtasari huu, waalike wafikirie jinsi ambavyo wangehisi kama wangekuwepo pamoja na Joseph Smith na Oliver Cowdery ndani ya Hekalu la Kirtland. Ipe familia yako fursa ya kushiriki jinsi wanavyohisi kuhusu Mwokozi.

Mafundisho na Maagano 110:15.Nini kinaweza kusaidia “kugeuza mioyo” ya watoto wenu kwa mababu zao? Mnaweza kupata baadhi ya mawazo ya kufurahisha kwenye FamilySearch.org/discovery. Mnaweza kushirikiana kuwatambua mababu ambao wanahitaji ibada za hekaluni na kupanga kufanya ibada hizo hekaluni. Mngeweza pia kuzungumza kuhusu jinsi kazi iliyorejeshwa na Eliya ndani ya Hekalu la Kirtland inavyoongeza upendo wenu kwa mababu zenu.

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “Roho wa Mungu,” Nyimbo za Kanisa, na. 2.

Picha
ikoni ya sauti za urejesho

Sauti za Urejesho

Madhihirisho ya Kiroho na Hekalu la Kirtland

Picha
Kuwekwa wakfu kwa Hekalu la Kirtland

Kama Moto Uwakao, na Glen S. Hopkinson

Hapa chini ni maneno ya Watakatifu wa Siku za Mwisho ambao walikuwa ndani ya Hekalu la Kirtland wakati wa kuwekwa kwake wakfu na katika mikutano mingine ambayo ilifuata. Wengi walifananisha uzoefu wao kwa kile Watakatifu wa kale walivyohisi wakati walipokuwa “wamevikwa nguvu kutoka juu” kwenye siku ya Pentekoste (Luka 24:49; ona pia Matendo ya Mitume 2:1–4; Mafundisho na Maagano 109:36–37).

Eliza R. Snow

“Sherehe hizo za kuweka wakfu zinaweza kukaririwa, lakini hakuna lugha ya duniani inayoweza kuelezea madhihirisho ya mbinguni ya siku hiyo ya kukumbukwa. Malaika waliwatokea baadhi, wakati hali ya uwepo wa kiungu ikiwafikia wote waliokuwepo, na kila moyo ukajazwa na ‘shangwe isiyoelezeka na kujawa na utukufu.’”1

Sylvia Cutler Webb

“Moja ya kumbukumbu zangu za mwanzo kabisa zilikuwa kuwekwa wakfu kwa Hekalu. Baba yangu alituchukua juu ya mapaja yake na alituambia kwa nini tulikua tunakwenda na kile ilichomaanisha kuweka wakfu nyumba ya Mungu. Na ingawa tulikuwa wadogo sana wakati ule, ninakumbuka bayana tukio lile. Ninaweza kutazama nyuma katika miaka iliyopita na kuona kama nilivyoona wakati huo Joseph Nabii, amesimama na mikono yake imeinuliwa kuelekea mbinguni, uso wake ukiwa kijivu kilichofifia, machozi yakitiririka mashavuni mwake alipokuwa akinena kwenye siku ile isiyosahaulika. Karibu wote walionekana kuwa katika machozi. Nyumba ilikuwa imejaa mno watoto walikuwa kwa kiasi kikubwa wamekaa katika mapaja ya watu wazima; dada yangu alikaa juu ya mapaja ya baba na mimi juu ya mapaja ya mama. Ninaweza kukumbuka hata nguo tulizovaa. Akili zangu zilikuwa changa mno wakati ule kuelewa umuhimu kamili wa yote, lakini jinsi muda ulivyosonga nilianza kufahamu zaidi na zaidi, na ninashukuru sana kwamba nilipata fursa ya kuwa pale.”2

Oliver Cowdery

“Jioni nilikutana na maofisa wa kanisa katika nyumba ya Bwana. Roho alimwagwa kwa wingi—Niliona utukufu wa Mungu, kama wingu kubwa, likija chini na kutua juu ya nyumba, na kuijaza kama upepo mkali upitao wenye nguvu. Niliona vilevile miale ya ndimi, kama vile ya moto ikitua juu ya wengi, … wakati walipozungumza kwa lugha zingine na kutabiri.”3

Benjamini Brown

“Maono mengi yalionwa. Mmoja aliona mto au wingu likitua juu ya nyumba, liking’aa kama wakati jua linapong’aa kwenye wingu kama dhahabu. Wawili wengine waliona viumbe watatu wakivinjari vinjari katika chumba wakiwa na funguo zinazong’aa mikononi mwao, na pia mnyororo unaong’aa mikononi mwao.”4

Orson Pratt

“Mungu alikuwa pale, malaika zake walikuwa pale, Roho Mtakatifu alikuwa katikati ya watu … na walikuwa wamejazwa kutoka vichwani mwao mpaka nyayo za miguu yao kwa nguvu na msukumo wa Roho Mtakatifu.”5

Nancy Naomi Alexander Tracy

“[Wakati] Hekalu lilipoisha na kuwekwa wakfu … zilikuwa siku zangu mbili za shangwe kuu katika maisha yangu. Wimbo wa kufaa ambao ulitungwa kwa ajili ya tukio hili ulikuwa ‘Roho wa Mungu Wawaka Kama Moto.’ Ilikuwa hakika kweli kwamba ushawishi wa Mbinguni ulitua juu ya nyumba ile. … Nilihisi kwamba mbingu ilikuwa duniani.”6

Muhtasari

  1. Katika Edward W. Tullidge, The Women of Mormondom (1877), 95.

  2. Katika Karl Ricks Anderson, oseph Smith’s Kirtland: Eyewitness Accounts (1996), 182–83.

  3. Oliver Cowdery diary, Machi 27, 1836, Church History Library, Salt Lake City.

  4. Benjamin Brown letter to his wife, Sarah, circa April 1836, Benjamini Brown family collection, Church History Library, Salt Lake City; vituo and herufi kubwa vimeboreshwa.

  5. Orson Pratt, “Remarks,” Deseret News, Jan. 12, 1876, 788.

  6. Katika Richard E. Turley Jr. Na Brittany A. Chapman, eds., Women of Faith in the Latter Days (2011), 1:442.

Picha
Musa, Elia, na Eliya wakitokea katika Hekalu la Kirtland

Musa, Elia, na Eliya wanatokea ndani ya Hekalu la Kirtland, na Gary E. Smith

Chapisha