“Oktoba 25–31. Mafundisho na Maagano 124: ‘Nyumba Kwa Jina Langu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)
“Oktoba 25–31. Mafundisho na Maagano 124,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021
Oktoba 25–31
Mafundisho na Maagano 124
“Nyumba kwa Jina Langu”
Unaposoma Mafundisho na Maagano 124, tafakari baraka ambazo Bwana aliwaalika Watakatifu wa Nauvoo kuzipokea na baraka ambazo Yeye anaahidi kwako.
Andika Misukumo Yako
Ilikuwa ni miaka sita iliyopita ya ugumu kwa Watakatifu, mambo yalianza kuonekana kuja juu katika majira ya kuchipua ya 1839: Watakatifu wakimbizi walikuwa wamepata huruma miongoni mwa raia wa Quincy, Illinois. Walinzi walikuwa wamewaruhusu Nabii Joseph Smith na viongozi wengine wa Kanisa kutoroka ufungwa huko Missouri. Na Kanisa ndio kwanza lilikuwa limenunua ardhi huko Illiois ambapo Watakatifu wangekusanyika tena. Ndiyo, ardhi ilikuwa yenye majimaji, iliyojawa na mbu, lakini ikilinganishwa na changamoto ambazo Watakatifu walikuwa tayari wamekumbana nazo, hili pengine lilionekana lenye kuchukulika. Kwa hiyo walikausha majimaji na wakatengeneza mkataba wa mji mpya, ambao waliuita Nauvoo. Inamaanisha “nzuri” kwa Kiebrania, ingawa ulikuwa zaidi ni msemo wa imani kuliko maelezo sahihi, angalau hapo mwanzo. Wakati ule ule, Bwana alikuwa akimshawishi Nabii wake na hisia za uharaka. Alikuwa na kweli nyingi na ibada za kurejesha, na Alihitaji hekalu takatifu ambapo watakatifu wangeweza kuzipokea. Katika njia nyingi, hisia hizi hizi za imani na uharaka ni za muhimu katika kazi ya Bwana leo.
Wakati Nauvoo iliweza kuwa mji mzuri wenye hekalu zuri, vyote hatimaye viliachwa. Bali kazi nzuri ya kweli ya Bwana, wakati wote, imekuwa “kuwavika kwa heshima, kutokufa, na uzima wa milele” (Mafundisho na Maagano 124:55), na kazi hiyo haikomi kamwe.
Ona Saints, 1:399–427; “Organizing the Church in Nauvoo,” Ufunuo katika Muktadha, 264–71.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko
Mafundisho na Maagano 124:12–21
Ninaweza kuwa mfuasi ambaye Bwana anamwamini.
Ingawa viongozi kadhaa mashuhuri waliacha Kanisa mwishoni mwa miaka ya 1830, waumini walio wengi walibaki waaminifu. Watakatifu hawa waaminifu ni pamoja na wale waliovumilia majaribu ya Missouri pamoja na wale ambao walikuwa punde wamejiunga na Kanisa. Katika Mafundisho na Maagano 124:12–21, Bwana aliwasifia sana wachache wao. Je, ni utambuzi upi kuhusu ufuasi unaupata katika maneno Yake? Je, kuna chochote kuhusu Watakatifu hawa waaminifu ambacho kinakuvutia wewe kuwa kama wao? Unaweza pia kutafakari jinsi Bwana alivyoonesha upendo Wake kwa ajili yako.
Mafundisho na Maagano 124:22–24, 60–61
Bwana ananitaka kuwakaribisha na kuwakubali wengine.
Kwa kuzingatia kile ambacho Watakatifu walikuwa wametoka kuteseka Missouri, wangeweza kuwa walishawishika kujitenga na kuwakatisha tamaa wageni huko Nauvoo. Weka hilo akilini unaposoma Mafundisho na Maagano 124:22–24, 60–61. Nini kinakuvutia kuhusu maelekezo ya Bwana kujenga “nyumba kwa ajili ya kuishi”? (mstari wa 23). Maneno Yake yanakufundisha nini kuhusu misheni ya Kanisa Lake? Tafakari jinsi gani maelekezo haya yanaweza kutumika kwako na nyumbani kwako.
Ona pia video ya “A Friend to All,” ChurchofJesusChrist.org.
Mafundisho na Maagano 124:25–45, 55
Bwana anatuamuru tujenge mahekalu ili tupokee maagizo matakatifu.
Kwa kweli ilikuja kama jambo lisiloshangaza kwa Watakatifu wa Siku za Mwisho kwamba baada ya kuweka makazi huko Nauvoo, Bwana aliwapa maelekezo kuhusu kujenga hekalu—kama Alivyofanya huko Ohio na Missouri. Unapata nini katika Mafundisho na Maagano 124:25–45, 55 ambacho kinakusaidia kuelewa kwa nini Bwana alisema, “watu Wangu daima wanaamriwa kujenga [mahekalu] kwa jina langu takatifu”? (mstari wa 39).
Tangu Hekalu la Nauvoo lilipojengwa, zaidi ya mahekalu 200 yamejengwa au kutangazwa. Rais Russell M. Nelson alifundisha: “Tunajua ya kwamba muda wetu katika hekalu ni muhimu kwa wokovu na kuinuliwa kwetu na kwa familia zetu. … Mashambulizi ya adui yanaongezeka kwa kasi, kwa ukali na kwa namna nyingi. Hitaji letu la kuwa hekaluni mara kwa mara halijawahi kuwa kubwa kiasi hiki” (“Kuwa Mtakatifu wa Siku za Mwisho wa Mfano,” Ensign au Liahona, Nov. 2018, 114). Ni kwa jinsi gani hekalu limekusaidia kuhimili “mashambulizi ya adui”? Je, unahisi kutiwa msukumo kufanya nini ili kufuata ushauri wa Rais Nelson?
Ona pia Church History Topics, “Nauvoo Temple,” ChurchofJesusChrist.org/study/church-history.
Mafundisho na Maagano 124:84–118
Bwana anatamani kunipa ushauri maalum kwa ajili ya maisha yangu.
Mistari 84–118 imejazwa na ushauri kwa ajili ya watu binafsi maalum, na baadhi yake inaweza isionekane kuwa na uhusiano kwenye maisha yako. Lakini unaweza pia kupata kitu fulani unachohitaji kusikia. Fikiria kumuuliza Bwana ni ujumbe gani alionao kwa ajili yako katika mistari hii, na tafuta mwongozo wa Roho kuupata. Kisha amua kile utakachokifanya kuutendea kazi. Kwa mfano, ni kwa jinsi gani kwa kuwa mnyenyekevu zaidi kunakusaidia kumpokea Roho? (ona mstari wa 97).
Ungeweza pia kutafakari ushauri mwingine Bwana aliokupa. Ni jinsi gani unafanyia kazi hilo?
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani
-
Mafundisho na Maagano 124:2–11.Kama Bwana angeiambia familia yako “kufanya tangazo la dhati la injili yangu” kwa “wafalme wote wa ulimwengu” (mistari 2–3), tangazo lako lingesema nini? Fikirieni kubuni moja kwa pamoja, na waalike wanafamilia kupendekeza kweli za injili wanazotaka kuzijumuisha.
-
Mafundisho na Maagano 124:15.Inamaanisha nini kuwa na uadilifu? Kwa nini Bwana anathamini uadilifu? Ni mifano gani ya uadilifu ambayo familia yako imepata kuiona? (Ona pia Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, 19.)
-
Mafundisho na Maagano 124:28–29, 40–41, 55.Tunajifunza nini kutoka katika mistari hii kuhusu kwa nini Bwana anatuamuru kujenga mahekalu? Familia yako ingeweza kutaka kuchora picha ya hekalu au kujenga moja la matofali au nyenzo nyingine. Mnapofanya hivyo, mngeweza kujadili kwa nini mna shukrani kwamba tuna mahekalu leo na kwa nini tunahitaji kuabudu ndani yake mara kwa mara.
-
Mafundisho na Maagano 124:91–92.Je, familia yako ingenufaika kutokana na majadiliano kuhusu baraka za patriaki? Wanafamilia ambao wamepokea baraka zao za patriaki wangeweza kushiriki jinsi ilivyokuwa kwenye kupokea baraka hiyo na jinsi ilivyowabariki. Mngeweza pia kurejea “Baraka za Patriaki” (Mada za Injili, topics.ChurchofJesusChrist.org).
Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.
Wimbo uliopendekezwa: “I Love to See the Temple,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 95.
Sauti za Urejesho
Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama
Mnamo mwaka 1842, baada ya Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama kuanzishwa huko Nauvoo, Illinois, Nabii Joseph Smith alisema, “Kanisa halikuwahi kamwe kuratibiwa kikamilifu mpaka wanawake waliporatibiwa hivi.”1 Vile vile, mafunzo ya Urejesho wa Kanisa la Bwana na ukuhani Wake (ona Mafundisho na Maagano 107) hayajakamilika mpaka yatakapojumuisha mafunzo ya Muugano wa Usaidizi wa Akina Mama, ambao wenyewe ni “urejesho wa mpangilio wa kale” wa wafuasi wa kike wa Yesu Kristo.2
Eliza R. Snow alifanya jukumu muhimu katika urejesho huo. Alikuwepo wakati Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama ulipoanzishwa kwa mara ya kwanza na, kama katibu wa muungano, aliandika mihutasari wakati wa mikutano. Alishuhudia moja kwa moja kwamba Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama ulianzishwa “kwa mpangilio wa ukuhani.”3 Hapa chini ni maneno yake, yaliyoandikwa wakati alipokuwa akihudumu kama Rais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama, kuwasaidia dada zake waelewe kazi takatifu iliyokabidhiwa kwa mabinti wa agano wa Mungu.
Kujifunza zaidi kuhusu jinsi Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama ulivyoanzishwa, ona Daughters in My Kingdom: The History and Work of Relief Society (2017), 1–25; Miaka Hamsini ya Kwanza ya Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama (2016), 3–175.
Eliza R. Snow
“Ingawaje jina [Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama] linaweza kuwa la kisasa, taasisi hiyo ni ya asili ya kale. Tuliambiwa na [Joseph Smith], kwamba mpangilio kama huu ulikuwepo katika kanisa hapo kale, madokezo ambayo yamefanywa katika baadhi ya nyaraka zilizoandikwa katika Agano Jipya, yakitumia jina, ‘mama mteule’ [ona 2 Yohana 1:1; Mafundisho na Maagano 25:3].
“Huu ni mpangilio ambao hauwezi kuwepo bila ukuhani, kutokana na ukweli kwamba unapata mamlaka yake yote na ushawishi kutoka chanzo hicho. Wakati Ukuhani ulipochukuliwa kutoka duniani, taasisi hii sawa na kila kiambatisho kingine cha utaratibu wa kweli wa Kanisa la Yesu Kristo duniani, ikawa imekufa. …
“Kuwepo kwenye mpangilio wa ‘Muungano wa Kike wa Usaidizi wa Akina Mama wa Nauvoo,’ … na pia nikiwa na uzoefu mkubwa katika muungano huo, pengine ninaweza kuwasilisha dokezo chache ambazo zitawasaidia mabinti wa Sayuni katika kupiga hatua mbele katika nafasi hii muhimu mno, ambayo imejaa majukumu mapya na yaliyoongezwa. Ikiwa yeyote kati ya mabinti na akina mama katika Israeli wanahisi kupungukiwa katika nafasi zao za sasa, sasa watapata uwanda wa kutosha kwa kila nguvu na uwezo wa kutenda mema kwa yale ambayo wamewezeshwa kwa nguvu kutoka juu. …
“Swali linaweza kuja akilini, kwa yeyote, Ni nini kusudi la Muungano wa Kike wa Usaidizi wa Akina Mama? Ningejibu—kufanya mema—kuleta kwenye hali ya kuhitaji kila uwezo tulionao kwa ajili ya kufanya mema, siyo tu katika kuwasaidia maskini bali katika kuokoa nafsi. Juhudi zilizounganika zitakamilisha kupita kipimo zaidi kuliko inavyoweza kukamilishwa na nguvu binafsi za kufaa sana. …
“Katika kuhudumia maskini, Muungano wa Kike wa Usaidizi wa Akina Mama una kazi zingine za kufanya kuliko kutuliza tu mahitaji ya kimwili. Umaskini wa akili na ugonjwa wa moyo, pia vinahitaji umakini; na mara nyingi onesho la ukarimu—maneno machache ya ushauri, au hata ukunjufu na kushikana mikono kwa upendo kutaleta mema mengi na kushukuriwa mno zaidi ya mfuko wa dhahabu. …
“Wakati Watakatifu wanapokusanyika kutoka mbali, ni wageni kwa kila mtu, na wanakuwa kwenye hali ya kupotezwa na wale wanaowangojea kuwadanganya, Muungano wa [Usaidizi] wa Akina Mama hauna budi mara moja [kuwatunza], na kuwatambulisha kwenye muungano ambao utawasafisha na kuwainua na juu ya yote kuwaimarisha katika imani ya Injili, na kwa kufanya hivyo, wanaweza kuwa vyombo katika kuwaokoa wengi.
“Itahitaji juzuu nyingi ambazo zitahitajika kufafanua majukumu, fursa na wajibu ambavyo huja katika uwepo wa macho ya Muungano. … Iendee (chini ya maelekezo ya askofu wako) kwa utulivu, kwa nguvu, kwa kuungana na kwa sala, na Mungu atavika taji juhudi zenu kwa mafanikio.”4