Mafundisho na Maagano 2021
Oktoba 11–17. Mafundisho na Maagano 115–120: “Dhabihu Yake Itakuwa Takatifu Zaidi Kwangu Mimi Kuliko Mafanikio Yake”


“Oktoba11–17. Mafundisho na Maagano 115–120: ‘Dhabihu Yake Itakuwa Takatifu Zaidi Kwangu Mimi Kuliko Mafanikio Yake,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Oktoba11–17. Mafundisho na Maagano 115–120,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021

Picha
Mbali Magharibi

Mbali Magharibi, na Al Rounds

Oktoba 11–17

Mafundisho na Maagano 115–120

“Dhabihu Yake Itakuwa Takatifu Zaidi Kwangu Mimi Kuliko Mafanikio Yake”

Mungu anataka kuzungumza nawe. Unapojifunza maandiko, sali na umuombe Yeye akusaidie kugundua jumbe Zake kwa ajili yako.

Andika Misukumo Yako

Kulikuwa na sababu ya kuwa na matumaini mema kuhusu sehemu mpya kabisa ya kukusanyika Watakatifu, Mbali Magharibi, Missouri, mnamo Julai 1838. Jiji lilikuwa linakua haraka, ardhi ilionekana kuwa yenye neema, na ilifunuliwa kwamba umbali mfupi kwenda kaskazini kulikuwa na Adam‑ondi‑Ahman, sehemu yenye umuhimu mkubwa mno kiroho (ona mafundisho na Maagano 107:53–56116). Bado, lazima ingekuwa vigumu kwa Watakatifu kutofikiria kuhusu kile walichopoteza. Wamefukuzwa kutoka Independence, sehemu ya katikati iliyochaguliwa ya Sayuni, na nafasi za kurudi wakati wowote karibuni pengine zilionekana finyu. Kwa nyongeza, Watakatifu ilibidi waikimbie Kirtland, Ohio, wakiacha hekalu lao walilolipenda baada ya miaka miwili tu. Na wakati huu haikuwa tu maadui nje ya Kanisa waliokuwa wanasababisha matatizo—waumini wengi mashuhuri walikuwa wamegeuka dhidi ya Joseph Smith, ikijumuisha mashahidi watatu wa Kitabu cha Mormoni na washiriki wanne wa Wale Kumi na Wawili. Baadhi wangeweza kujiuliza, kweli ufalme wa Mungu unakua imara zaidi au unazidi kuwa dhaifu?

Bado waaminifu hawakuruhusu maswali kama hayo yawakwamishe. Badala yake, walianza kujenga sehemu mpya takatifu, wakati huu ilikuwa huko Mbali Magharibi. Walifanya mipango kwa ajili ya hekalu jipya. Mitume wanne wapya waliitwa, ikiwa ni pamoja na wawili—John Taylor na Wilford Woodruf—ambao baadaye walikuwa Marais wa Kanisa (ona Mafundisho na Maagano 118:6). Watakatifu walijifunza kwamba kufanya kazi ya Mungu haina maana kwamba hutaanguka; inamaanisha “unainuka tena.” Na ingawa itabidi uache baadhi ya vitu, dhabihu hizo zitakuwa takatifu kwa Mungu, hata “takatifu zaidi … kuliko mafanikio [yako]” (Mafundisho na Maagano 117:13).

Ona Watakatifu, 1:296–99; “Mbali Magharibi na Adam‑ond‑Ahman,” Ufunuo katika Muktadha, 235–41.

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Mafundisho na Maagano 115:4–6

Jina la Kanisa lilidhihirishwa na Bwana.

Rais Russell M. Nelson alisema kwamba jina la Kanisa ni “jambo la umuhimu mkuu” (“Jina Sahihi la Kanisa,” Ensign au Liahona, Nov. 2018, 87). Fikiria kuhusu kwa nini hii ni kweli unaposoma Mafundisho na Maagano 115:4–6. Jina la Kanisa linahusika vipi na kazi na misheni yake?

Ona pia 3 Nefi 27:1–11.

Mafundisho na Maagano 115:5–6

Sayuni na vigingi vyake vinatoa “kimbilio kutokana na tufani.”

Licha ya shida watakatifu walizokuwa wanakumbana nazo mnamo mwaka 1838, Bwana bado alikuwa na mategemeo makubwa kwa ajili yao. Tafuta maneno katika Mafundisho na Maagano 115:5–6 ambayo yanasisitiza wajibu ambao Bwana anataka Kanisa Lake na waumini wake kukamilisha ulimwenguni. Kwa mfano, unahisi unapaswa kufanya nini ili “kuinuka na kung’ara”? (mstari wa 5). Je tufani zipi za kiroho unaziona zinakuzunguka, na jinsi gani tunapata “kimbilio” kupitia kukusanyika? (mstari wa 6).

Ona pia 3 Nefi 18:24.

Mafundisho na Maagano 117

Dhabihu zangu ni takatifu kwa Bwana.

Kuondoka Kirtland kunaweza kuwa kulikuwa kugumu hasa kwa watu kama Newel K. Whitney, aliyeanzisha maisha yenye ustawi kwa ajili ya familia yake huko. Unapata nini katika Mafundisho na Maagano 117:1–11 ambacho kingeweza kuwasaidia kufanya dhabihu hii? Ni jinsi gani mistari hii inabadilisha mtazamo wako juu ya kile kilicho muhimu hasa?

Dhabihu iliyoombwa kwa Oliver Granger ilikuwa tofauti: Bwana alimpangia abaki Kirtland na kulipa madeni yote ya Kanisa. Ilikuwa kazi ngumu, na wakati akiliwakilisha Kanisa kwa uadilifu, hatimaye hakuweza kupata tena fedha nyingi. Fikiria jinsi gani maneno ya Bwana katika mistari ya 12–15 yanavyoweza kutumika katika vitu ambavyo Bwana amekutaka wewe ufanye.

Ona pia Mathayo 6:25–33; Boyd K. Packer, “Mdogo Kati ya Hawa,” Ensign au Liahona, Nov. 2004, 86–88; “Mbali Magharibi na Adam‑ond‑Ahman,” Ufunuo katika Muktadha, 239–40.

Picha
Adam‑ond‑Ahman katika Daviess Country, Missouri

Newel K. Whitney aliamriwa kuhamia Adam‑ondi‑Ahaman, iliyopigwa picha hapa.

Mafundisho na Maagano 119–20

Kwa kulipa zaka, ninasaidia kujenga na “kutakasa nchi ya Sayuni.”

Maelekezo katika sehemu ya 119 na 120 yanafanana na jinsi kazi ya Bwana inavyogharamiwa katika wakati wetu. Leo, watakatifu wanachangia “moja ya kumi ya faida zao [sasa ikijulikana kama mapato] kila mwaka” (Mafundisho na Maagano 119:4.), na michango hii inasimamiwa na baraza ambalo linajumuisha Urais wa Kwanza, Akidi ya Wale Kumi na Wawili, na Uaskofu Simamizi. Fikiria maswali yafuatayo unapojifunza sehemu hizi:

  • Ni kwa jinsi gani kushika sheria ya zaka “kunaitakasa nchi ya Sayuni”? Ni kwa jinsi gani sheria hii inaweza kusaidia kufanya mahali ambapo unaishi kuwa “nchi ya Sayuni kwako”? (Mafundisho na Maagano 119:6).

  • Ni nini cha maana kwako kuhusu kirai “na kwa sauti yangu mwenyewe kwao” katika Mafundisho na Maagano 120?

Ona pia Malaki 3:8–12; David A. Bednar, “The Windows of Heaven,” Ensign au Liahona, Nov. 2013, 17–20; “Zaka za Watu Wangu,” Ufunuo katika Muktadha, 250–55.

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Nyumbani

Mafundisho na Maagano 115:4–6.Je itawezekana kwa familia yako kusoma mistari hii wakati wakiangalia mapambazuko? Inaweza kusaidia kujadili kile inachomaanisha “kuinuka na kung’ara” (mstari wa 5). Au mngeweza pia kujadiliana jinsi ilivyo kutafuta hifadhi wakati wa tufani. Ni jinsi gani uzoefu huo ungekuwa kama kutafuta “kimbilio” katika Kanisa? (mstari wa 6). Mngeweza kisha kuzungumza kuhusu jinsi familia yako inavyoweza kuwasaidia wengine kufurahia kimbilio linalotolewa na kanisa.

Mafundisho na Maagano 117:1–11.Familia yako ingeweza kufananisha ‘tone” na kitu kingine chenye “uzito” zaidi (mstari wa 8), kama jagi la maji. Hii ingeweza kuwapeleka kwenye mjadala kuhusu vitu vyenye umuhimu mdogo katika maisha yetu ambavyo vinaweza kutuzuia kupokea baraka nyingi za Mungu.

Mafundisho na Maagano 119.Mgeweza kuimba wimbo kama vile “I Want to Give the Lord My Tenth” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 150). Je, wimbo na sehemu ya 119 vinatufundisha nini kuhusu kwa nini tunalipa zaka? Watoto wadogo wangeweza pia kunufaika kutokana na somo la vitendo: ungeweza kuwapa vitu vidogo, wasaidie kukokotoa moja ya kumi, na waambie kwa nini unalipa zaka.  (Ona pia True to the Faith, 180–82.)

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “I Want to Give the Lord My Tenth,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 150.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Himiza kujitegemea. “Wakati [Wanafamilia] wana maswali, mara nyingine ni bora kuwafundisha jinsi ya kuyatafutia majibu wao wenyewe, kuliko kuyajibu maswali mara moja” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 28).

Picha
matumizi ya zaka

Kutoa asilimia 10 kwa Bwana kama zaka kunasaidia kuendeleza kazi Yake ya wokovu.

Chapisha