Mafundisho na Maagano 2021
Oktoba 11–17. Mafundisho na Maagano 115–120: “Dhabihu Yake Itakuwa Takatifu Zaidi Kwangu Mimi Kuliko Mafanikio Yake”


“Oktoba 11–17. Mafundisho na Maagano 115–120: ‘Dhabihu Yake Itakuwa Takatifu Zaidi kwangu Mimi Kuliko Mafanikio Yake,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Oktoba 11–17. Mafundisho na Maagano 115–120,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2021

Picha
Mbali Magharibi

Mbali Magharibi, na Al Rounds

Oktoba 11–17

Mafundisho na Maagano 115–120

“Dhabihu Yake Itakuwa Takatifu Zaidi kwangu Mimi Kuliko Mafanikio Yake”

Mruhusu Roho akuongoze kwenye kanuni ambazo watoto wanazihitaji zaidi. Yawezekana ukapata mawazo yenye msaada katika shughuli za watoto wadogo au watoto wakubwa.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Mara chache, yaweza kuwa vyema kuongea na wazazi wa mmoja wa watoto mapema na kupendekeza kwamba mtoto huyo aje darasani akiwa amejiandaa kushiriki jambo fulani alilojifunza nyumbani. Mtoto huyo anaweza kufurahia kuliongoza darasa kwa shughuli ambayo yeye atakuwa amekwisha kuifanya na wanafamilia.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mafundisho na Maagano 115:4–5

Mimi ni wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.

Je, unawezaje kuwasaidia watoto kutambua baraka za kuwa sehemu ya Kanisa la Yesu Kristo?

Shughuli Yamkini

  • Waulize watoto kama kuna yeyote kati yao anayeweza kutamka jina kamili la Kanisa. Waoneshe nembo ya Kanisa (kwenye chapisho la Kanisa au beji ya jina la mmisionari), andika jina ubaoni, au wasomee kutoka Mafundisho na Maagano 115:4. Waombe watoto kutaja jina sambamba na wewe wakati ukionesha kwa kidole kila neno. Onesha maneno muhimu katika jina, na wasaidie watoto kuelewa kwa nini maneno haya ni muhimu (ona “Sura ya 43: Yesu Kristo Anataja Jina la Kanisa Lake,” Hadithi za Mafundisho na Maagano, 164).

  • Imbeni pamoja “The Church of Jesus Christ” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 77), na waelezee watoto jinsi unavyojisikia kuhusu kuwa muumini wa Kanisa la Yesu Kristo. Waache waeleze jinsi wanavyojisikia kuhusu Kanisa.

  • Waalike watoto kusimama wakati unaposoma neno “inukeni” katika Mafundisho na Maagano 115:5. Waalike kunyosha vidole vyao kama miale ya mwangaza wa jua wakati unaposoma “ng’ara.” Imbeni pamoja wimbo kuhusu kuwa nuru kwa wengine, kama vile “I Am like a Star” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 163). Wakumbushe watoto kwamba nuru yetu huja kutoka kwa Yesu Kristo, na wasaidie kufikiria jinsi wanavyoweza “kung’ara.”

Mafundisho na Maagano 117:6

Yesu Kristo aliumba dunia na vyote vilivyomo ndani yake.

Ili kuwatia moyo William Marks na Newel K. Whitney kutoa dhabihu ya ardhi yao na kuhamia Missouri, Bwana aliwakumbusha kwamba Yeye ndiye aliyeumba vitu vyote vya duniani. Ni kwa jinsi gani watoto wanaweza kubarikiwa kwa kujua ukweli huu?

Shughuli Yamkini

  • Leta au chora picha za uumbaji katika Mafundisho na Maagano 117:6 ambapo Bwana alisema Yeye ndiye aliyeumba (au waalike watoto kuchora picha zao wenyewe). Waalike watoto kunyanyua juu au waoneshe kwa kidole picha wakati unaposoma mstari. Waambie watoto kwa nini ni muhimu kwako wewe kujua kwamba Yesu Kristo aliumba vitu hivi vyote.

  • Imba pamoja na watoto wimbo kuhusu uumbaji wa Bwana, kama vile “My Heavenly Father Loves Me” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 228–29). Acha watoto wazungumze kuhusu baadhi ya vitu ambavyo Mungu ameviumba ambavyo vinawasaidia wao kuhisi upendo Wake.

Mafundisho na Maagano 119–20

Zaka inasaidia Kanisa kufanya kazi ya Mungu.

Wengi wa watoto unaowafundisha yawezekana ni wadogo sana kuweza kujipatia pesa na kulipa zaka, lakini ni vyema kwao kuelewa ni kwa namna gani zaka huchangia kwenye kazi kuu ambayo Kanisa linaifanya ulimwenguni kote.

Shughuli Yamkini

  • Elezea jinsi tunavyolipa zaka na inatumika kwa ajili gani (ona “Sura ya 44: Zaka,” Hadithi za Mafundisho na Maagano, 165–66, au video inayohusiana kwenye ChurchofJesusChrist.org). Chora sarafu 10 ubaoni, na waombe watoto wakusaidie kuzihesabu. Amua ni kiasi gani utampa Bwana kama zaka.

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu zaka, kama vile “I Want to Give the Lord My Tenth” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 150), na waambie watoto kwa nini unachagua kulipa zaka. Kama inawezekana, Simulia hadithi yako binafsi.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mafundisho na Maagano 115:4–6

Mfano wangu unaweza kuwasaidia wengine kuja kwa Kristo na kupata usalama.

Watoto unaowafundisha wanaweza kuwajua watu ambao wanaathiriwa na dhoruba za maisha na wanahitaji “kimbilio” (mstari wa 6) linalotolewa katika Kanisa. Fikiria namna gani utawapatia mwongozo wa kiungu watoto ili “wainuke na wang’are” (mstari wa 5) na kushiriki nuru yao na watu hawa.

Shughuli Yamkini

  • Pitisha tochi, picha ya jua, au kitu kingine ili kuwakilisha nuru ya injili ya Mwokozi. Inapofikia zamu yao kushika tochi, waalike watoto kusoma Mafundisho na Maagano 115:4–5 na kutaja kitu fulani wanachoweza kufanya ili “wang’are” kama nuru kwa wengine (ona 3 Nefi18:24).

  • Waalike watoto wachore picha inayofafanua Mafundisho na Maagano 115:6. Kwa mfano, wanaweza kuchora picha ya dhoruba, pamoja na watu wakikimbilia katika jengo la Kanisa. Je, ni baadhi ya vitu gani vinaweza kuwakilishwa na dhoruba? Je, ni kwa jinsi gani Kanisa hutoa kimbilio kutokana na mambo haya?

Mafundisho na Maagano 117

Dhabihu zangu ni takatifu kwa Bwana.

Katika sehemu ya 117, Bwana aliwashauri William Marks na Newel K. Whitney kutoa dhabihu mali zao katika Kirtland kwa ajili ya baraka kubwa huko Missouri. Pia alimpa heshima Oliver Granger kwa ajili ya dhabihu aliyofanya. Je, unahisi watoto wanaweza kujifunza nini kutokana na mifano yao?

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kufikiria kwamba wao walikuwa wafanya bishara waliomiliki maduka makubwa huko Kirtland, kama Newel K. Whitney. Wangejisikiaje kama Bwana angewataka kuacha maduka yao na kuhamia sehemu nyingine mpya? Wasomee watoto Mafundisho na Maagano 117:1–11, na waombe watoto wakusimamishe wakati wanaposikia kitu ambacho kingewasaidia wao kuwa na imani ya kufanya dhabihu hizo na kumtii Bwana. Je, ni kitu gani tunatoa dhabihu leo ili kumtii Bwana?

  • Kwa kifupi waambie watoto kwa nini Watakatifu walitakiwa kuondoka Kirtland, au acha mtoto mmoja kati yao afanye hivyo (ona “Sura ya 41: Matatizo Kirtland,” Hadithi za Mafundisho na Maagano, 158–60). Elezea kwamba Bwana alimwomba Oliver Granger abaki Kirtland na alipe madeni ya Kanisa. Je, ni kwa nini hiyo ingekuwa kazi ngumu? Je, Bwana alisema nini katika Mafundisho na Maagano 117:13 ambacho kingemsaidia Oliver—au yeyote miongoni mwetu—kufanya dhabihu ya kumtii Bwana?

Mafundisho na Maagano 119–20

Zaka inasaidia Kanisa kufanya kazi ya Mungu.

Tafakari jinsi utakavyowasaidia watoto kuelewa jinsi zaka—hata kiasi kidogo wanachoweza kulipa—huchangia katika kuujenga ufalme wa Bwana (ona True to the Faith, 180–82).

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto wafikirie kwamba rafiki anaona jengo la Kanisa na anauliza, “Je, ni kwa namna gani Kanisa lenu linalipia gharama za jengo kama hili?” Je ni kwa jinsi gani tutaielezea zaka kwa rafiki huyu? Pendekeza kwamba watoto warejelee katika Mafundisho na Maagano 119:4; 120:1 wakati wanapolifikiria swali hili.

  • Wasaidie watoto kufikiria juu ya vitu ambavyo Kanisa linaweza kufanya kwa sababu ya zaka. Je, ni kwa namna gani vitu hivi vinabariki maisha yetu? Shiriki hisia zako kuhusu sheria ya zaka na jinsi ilivyokubariki wewe.

    Picha
    mvulana akilipa zaka

    Kwa kulipa zaka, tunaweza kuonesha upendo wetu kwa Mungu na kusaidia katika kazi Yake.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kutambua kile walichokihisi katika mioyo yao au mawazo yao ambacho kilikuja kwenye akili zao wakati wa darasa la Msingi leo. Watie moyo kushiriki hisia na mawazo yao hayo kwa familia zao.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Saidia Wazazi. Tafuta mbinu za kuwaelezea wazazi kile watoto wao wanachojifunza katika darasa la Msingi, na waulize namna gani wewe unaweza kuwasaidia katika jitihada zao kama wazazi (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 25).

Chapisha