Mafundisho na Maagano 2021
Oktoba18–24. Mafundisho na Maagano 121–123: “Ee Mungu, Uko Wapi?”


“Oktoba 18–24. Mafundisho na Maagano 121–123: ‘Ee Mungu, Uko Wapi?’” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Oktoba 18–24. Mafundisho na Maagano 121–123,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2021

Picha
Gereza la Liberty

Gereza la Liberty Spring, na Al Rounds

Oktoba 18–24

Mafundisho na Maagano 121–123

“Ee Mungu, Uko Wapi?”

Unapojifunza Mafundisho na Maagano 121–23, zingatia kile ambacho watoto darasani kwako tayari wanakijua. Omba kujua namna ya kujenga juu ya kile wanachokijua.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Kama uliwatia moyo watoto kushiriki na familia zao kitu walichojifunza darasani wiki iliyopita, wape muda wa kusimulia uzoefu wao.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mafundisho na Maagano 121:7–8; 122:7

Nyakati ngumu zinaweza kuwa ni kwa faida yetu.

Maneno ya Bwana kwa Joseph Smith katika Gereza la Liberty yanatoa fursa ya kuwasaidia watoto kutambua kwamba nyakati fulani maisha ni magumu, lakini Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanaweza kutusaidia.

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kusikiliza neno “amani” wakati ukishiriki nao “Sura ya 46: Joseph Smith katika gereza la Liberty” (Hadithi za Mafundisho na Maagano, 172–74) au Mafundisho na Maagano 121:7–8). Wasaidie watoto kufikiria juu ya njia tunazoweza kumwamini Bwana kama Joseph alivyofanya ili tuweze kujisikia amani. Elezea kwamba ingawa Joseph alipitia mambo magumu, Bwana alikuwa pamoja naye.

  • Ili kuwasaidia watoto kutambua kwamba majaribu yetu “yatakuwa kwa faida [yetu]” (Mafundisho na Maagano 122:7), ongea nao kuhusu namna gani misuli yetu inakua wakati tunapobeba kitu kizito. Acha waigize kuinua kitu kizito au kufanya kazi nzito. Elezea kwamba kupitia nyakati ngumu kunaweza kusaidia roho zetu kukua—kama tutamgeukia Bwana kwa ajili ya msaada. Simulia baadhi ya mifano ambayo watoto unaowafundisha wanaweza kujihusisha nayo. Waalike kurudia pamoja nawe kifungu cha maneno “Mambo haya yote yatakuwa … kwa faida [yetu].”

Mafundisho na Maagano 122:8

Yesu Kristo anajua jinsi ninavyojisikia.

Katika Gereza la Liberty, Yesu Kristo alimwambia Joseph Smith kwamba Yeye alijishusha chini ya vitu vyote (ona Mafundisho na Maagano 122:8). Hii inamaanisha kwamba Yeye anajua kile tunachopitia na kwamba tunaweza kumgeukia Yeye.

Shughuli Yamkini

  • Ili kuwasaidia watoto kujifunza kumgeukia Kristo wakati wanapopitia mambo magumu, omba wakuoneshe nyuso zao hufananaje wakati wakiwa na huzuni au wameumizwa au wanaogopa. Je, ni nani anaweza kutusaidia tunapojisikia hivi? Soma Mafundisho na Maagano 122:8, na ueleze kwamba hii ina maana kwamba Yesu Kristo anajua jinsi tunavyojisikia, na Anaweza kutusaidia.

  • Imbeni pamoja “Jesus Once Was a Little Child” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 55), na shuhudia kwamba Yesu Kristo anaweza kutusaidia kwa sababu anajua namna tunavyojisikia.

    Picha
    Yesu katika ardhi ya Gethsemani

    Yesu anaelewa mateso yetu. Si kama Nitakavyo Mimi, bali kama Utakavyo Wewe, na Walter Rane

Mafundisho na Maagano 123:17

Mungu ananitaka kwa furaha kabisa nifanye lile ninaloweza.

Ingawa Joseph Smith alikuwa gerezani na watakatifu walikuwa wamefukuzwa kutoka majumbani mwao, aliwatia moyo Watakatifu kwa “furaha na tufanye mambo yote yaliyo katika uwezo wetu.”

Shughuli Yamkini

  • Wasomee watoto Mafundisho na Maagano 123:17, na waalike watoto kusimama na kushangilia wakati wanaposikia neno “kwa furaha.” Waalike wao kujifanya wanatenda matendo tofauti ya huduma katika njia ya furaha.

  • Imbeni kwa pamoja wimbo kuhusu huduma ya furaha kama vile “When We’re Helping” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 198). Wasaidie watoto kufikiria njia wanazoweza kutumikia familia na marafiki zao kwa furaha.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mafundisho na Maagano 121:7–9; 122:7–9.

Majaribu yangu yanaweza kuwa kwa faida yangu.

Njia mojawapo Mwokozi aliyomfariji Joseph Smith wakati akiteseka katika Gereza la Liberty ilikuwa kwa kumfundisha kwamba “mambo haya yote yatakupa uzoefu, na yatakuwa kwa faida yako” (Mafundisho na Maagano 122:7). Ukweli huu unaweza kuwabariki watoto wakati wanapokabiliwa na majaribu yao wenyewe.

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kuelezea kile wanachojua kuhusu tukio la Joseph Smith kuwekwa gerezani na Watakatifu wakilazimishwa kuondoka Missouri (ona sura za 45–47 za Hadithi za Mafundisho na Maagano, 167–75). Waulize watoto ni jinsi gani wangejisikia kama wao wangekuwa Joseph Smith au mmoja wa Watakatifu wa wakati huu. Soma pamoja na watoto Mafundisho na Maagano 121:7–9; 122: 7–9, na waalike kutafuta kitu ambacho Bwana alisema ambacho kingewaletea amani. Ni kwa jinsi gani uzoefu wetu mgumu unaweza “kuwa kwa faida [yetu]”?

  • Waombe watoto wawili kushika kila mwisho wa kamba ambayo ni ndefu kiasi cha urefu wa darasa. Mwalike mtoto mwingine kufunga fundo kwenye kamba. Soma Mafundisho na Maagano 121:7–8, na uelezee kwamba kamba ile inawakilisha miaka ya milele na kwamba fundo dogo lililofungwa ni kama miaka yetu duniani. Inamaanisha nini kwamba majaribu yetu duniani ni ya “muda mfupi”?

  • Wasaidie watoto kufikiria kuwa ingekuwaje kutumikia kifungo cha miezi minne mahali kama Gereza la Liberty. Je, ni kitu gani tungekosa zaidi? Je, tungeutumiaje muda wetu? Je, Joseph Smith alijifunza nini katika Mafundisho na Maagano 121:7–9; 122:7–9 ambacho kilimsaidia kuvumilia uzoefu huu? Watie moyo watoto kuandika barua kwa mtu ambaye ana wakati mgumu, na pendekeza watumie kitu fulani kutoka Mafundisho na Maagano 121:7–9; 122:7–9 katika barua zao.

Mafundisho na Maagano 121:34–46

Ni lazima tuwe waadilifu ili tuwe na “nguvu za mbinguni.”

Wasaidie watoto unaowafundisha kutambua kwamba tunaweza kuwa na nguvu za Mungu katika maisha yetu endapo tu tutakuwa waadilifu.

Shughuli Yamkini

  • Chora mstari pamoja na maneno nguvu za juu kwenye mwisho mmoja na nguvu za chini kwenye mwisho mwingine. Chora mshale ukionesha katikati ya mstari. Chagua maneno kadhaa au vifungu vya maneno kutoka Mafundisho na Maagano 121:34–46 ambayo yanafundisha jinsi tunavyopunguza au kuongeza nguvu za mbinguni katika maisha yetu (kama vile “tunapoficha dhambi zetu,” “kiburi,” “upole,” na “upendo”). Waalike watoto kufanya zamu kuchagua neno, wakiamua kama neno linaongoza kwenye kupunguza au kuongezeka katika nguvu, na kuutembeza mshale kunakohusika. Zungumza na watoto kuhusu watu wanaowajua ambao wamekuwa na ushawishi mwema kwa wengine kwa sababu wanafuata ushauri wa Bwana ulioko katika mistari hii.

  • Soma Mafundisho na Maagano 121:41–42, 45, na watake watoto kuorodhesha sifa katika mistari hii ambazo Bwana anatutaka sisi tuwe nazo. Wasaidie kufafanua neno lolote ambalo hawalielewi. Mpangie kila mtoto sifa moja, na wasaidie kufikiri njia ambayo kwayo wanaweza kuionesha. Mara wote wanapokuwa wameshiriki, waombe wasome mistari 45–46 na waorodheshe baraka watakazopokea kama watakuza sifa hizo.

  • Someni pamoja mstari wa kwanza wa Mafundisho na Maagano 121:46. Ni kwa namna gani Roho Mtakatifu anaweza kuwa mwenzi wetu daima? Imbeni pamoja “The Holy Ghost” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 105) au wimbo mwingine kuhusu kipawa cha Roho Mtakatifu. Je, wimbo unatufundisha nini kuhusu kwa nini tunataka Roho Mtakatifu awe mwenzi wetu daima?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waombe watoto kumfikiria mtu ambaye anapitia wakati mgumu. Wasaidie kutambua jambo ambalo Joseph Smith alijifunza katika Gereza la Liberty ambalo wanaweza kushiriki na mtu huyo.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Saidia Kujifunza Nyumbani. “Wazazi ni walimu muhimu sana wa injili kwa watoto wao—wana vyote jukumu kuu na nguvu kubwa zaidi ya kuwashawishi watoto wao (ona Kumbukumbu la Torati 6:6–7). Unapowafundisha watoto kanisani, kwa maombi tafuta njia za kuwasaidia wazazi wao katika jukumu lao hili muhimu” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 25).

Chapisha