“Oktoba 4–10. Mafundisho na Maagano 111–114: ‘Nitapanga Mambo Yote kwa Faida Yenu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)
“Oktoba 4–10. Mafundisho na Maagano 111–114,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2021
Oktoba 4–10
Mafundisho na Maagano 111–114
“Nitapanga Mambo Yote kwa Faida Yenu”
Dada Cheryl A. Esplin, mshauri wa zamani katika Urais Mkuu wa Msingi, alifundisha kwamba tunapaswa “[kusaidia] watoto wetu kuweka mafundisho ndani ya mioyo yao katika njia ambayo … inaakisiwa katika mitazamo na tabia zao katika maisha yao yote” (“Kuwafundisha Watoto Wetu Kuelewa,” Ensign au Liahona, Mei 2012, 10).
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Ili kuwatia moyo watoto kushiriki, leta vitu kadhaa ambavyo vinahusiana na kitu fulani kutoka katika somo lililopita. Waruhusu wazungumze kuhusu kila kitu ulicholeta kinawakumbusha juu ya nini.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo
Mafundisho na Maagano 111:2, 10–11
Mambo ya Mungu yanaweza kuwa hazina kwangu.
Watoto wanapofikiria juu ya neno hazina, wao wanaweza kuweka taswira ya vitu ambavyo ni tofauti na hazina inayomaanishwa katika Mafundisho na Maagano 111:2, 10. Je, ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia kujifunza kuthamini mambo ya Bwana?
Shughuli Yamkini
-
Waalike watoto kuchora kile kinachokuja akilini mwao wasikiapo neno hazina. Tofautisha vitu ulimwengu uvionavyo kuwa ni hazina na vitu Bwana avionavyo kuwa hazina (ona Mafundisho na Maagano 111:2, 10–11), kama vile watu Wake, hekima na haki, na kufanya uchaguzi wa mambo mema.
-
Wasaidie watoto kukamilisha ukurasa wa shughuli ya wiki hii. Je, tunajifunza nini kuhusu Yesu kutokana na vitu Yeye anavyovithamini? Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa zaidi kama Yeye?
Bwana ataniongoza kwa mkono, na kujibu sala zangu.
Mafundisho na Maagano 112:10 inaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kujenga imani kwamba Yesu Kristo atawaongoza na kuwaelekeza katika maisha yao yote.
Shughuli Yamkini
-
Wasaidie watoto kufikiria hali ambapo ni muhimu kumshika mkono mwanafamilia, kama vile wakati wa kuvuka barabara au kumfariji mtu. Wanaweza kufurahia kufanya igizo la baadhi ya mifano wanayoshiriki. Soma Mafundisho na Maagano 112:10. Je, ni kwa nini tunataka Bwana “atuongoze [sisi] kwa kutushika mkono”?
-
Mfumbe macho mmoja wa watoto, na mwambie atembee kuvuka chumba na mtoto mwingine akimwongoza kwa kumshika mkono. Zungumza juu ya uzoefu wako wakati ambapo ulihisi Bwana anakuongoza kwa kukushika mkono.
Yesu anataka nimpende kila mmoja.
Wasaidie watoto kujua kwamba Mwokozi anatutaka tumpende kila mtu, hata wale ambao pengine hawatutendei mema.
Shughuli Yamkini
-
Unaposhiriki na wengine “Sura ya 41: Matatizo Kirtland” (Hadithi za Mafundisho na Maagano, 158–60), waambie watoto kutengeneza umbo la moyo kwa mikono yao wakati wasikiapo mtu fulani amefanya jambo sahihi. Wasaidie kuelewa kwamba Bwana anatutaka kumpenda kila mmoja, hata wale wanaofanya mambo yasiyo sahihi.
-
Chora uso wenye huzuni ubaoni, na waulize watoto tunawezaje kuonesha upendo kwa wengine wasio na furaha (ona Mafundisho na Maagano 112:11). Watoto wanaposhiriki mawazo yao, chora upya uso wenye huzuni kuwa uso wenye furaha. Toa ushuhuda wako juu ya nguvu inayokuja kutokana na kuwapenda wengine. Imbeni pamoja wimbo kuhusu upendo, kama vile “Jesus Said Love Everyone” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 61).
Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa
Ninaweza kuwa mnyenyekevu na kutafuta mwongozo wa Mungu.
Baba wa Mbinguni anataka sisi tuwe wanyenyekevu ili Yeye aweze kutuelekeza. Wasaidie watoto kuelewa namna wanavyoweza kuonesha unyenyekevu mbele za Mungu kwa kufanya mambo kama vile kumwomba Yeye na kuukubali ushauri Wake.
Shughuli Yamkini
-
Waulize watoto inamaanisha nini kuwa mnyenyekevu. (Wangeweza kusoma “Humility” katika True to the Faith [kurasa 86–87] kama italazimu). Wasaidie kufikiria juu ya maneno au vifungu vya maneno vinavyohusiana na “unyenyekevu,” na waalike kusoma Mafundisho na Maagano 112:10, wakibadilisha moja ya maneno haya au vifungu vya maneno katika mstari kwa “unyenyekevu”. Je, ni kwa nini Baba wa Mbinguni anatutaka sisi tuwe wanyenyekevu? Ili kujifunza zaidi, watoto wanaweza kusoma maandiko ya ziada yaliyoorodheshwa chini ya “Unyenyekevu” katika Mwongozo kwenye Maandiko (scriptures.ChurchofJesusChrist.org).
-
Andika maneno ya Mafundisho na Maagano 112:10 ubaoni, na waombe watoto wayasome kwa sauti. Mwalike mtoto apigie mstari baraka kwa ajili ya wale ambao ni wanyenyekevu zilizotajwa katika mstari huu. Watie moyo watoto kushiriki nyakati ambapo kwa unyenyekevu walitafuta msaada wa Bwana na wakaongozwa na Yeye, kama vile wakati maombi yao yalipojibiwa.
Yesu anataka nimpende kila mmoja.
Yesu Kristo alikuwa mfano mkamilifu wa kumpenda kila mtu, hata wale ambao hawakumtendea mema. Joseph Smith pia alivumilia mateso kutoka kwa wale ambao waliwahi kuwa rafiki zake. Wasaidie watoto kuelewa kwamba tunaweza kuwapenda wengine kama vile Mwokozi na Joseph Smith walivyofanya.
Shughuli Yamkini
-
Waalike watoto kupeana zamu kusoma kutoka “Sura ya 41: Matatizo Kirtland” (Hadithi za Mafundisho na Maagano, 158–60). Je, ni nani katika hadithi alifanya matatizo katika Kirtland kuwa mabaya zaidi? Je, ni nani alikuwa akijaribu kuyaboresha zaidi? Waalike watoto wasome Mafundisho na Maagano 112:11 na zungumza kuhusu kwa nini ni muhimu kumpenda kila mtu.
-
Kwa nini ni muhimu kuwapenda watu walio tofauti na sisi? Je, ni kwa nini Baba wa Mbinguni ametupatia sisi tofauti hizi? Je, ni kwa namna gani tunaweza “kuacha upendo [wetu] ubaki kwa wote” hata wale walio tofauti na sisi? Imba na watoto wimbo kuhusu kuwapenda wengine, kama vile “I’ll Walk with You” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 140–41).
-
Wasaidie watoto kufikiria juu ya mifano ya wakati Mwokozi alipowapenda wale waliomfanyia mabaya Yeye (kwa mfano, ona Luka 23:34).
Mafundisho na Maagano 112:12–15, 26)
Wale ambao wameongoka kwa dhati huja kumjua Yesu Kristo.
Kuja kuongoka kwa Yesu Kristo ni mchakato mrefu wa maisha yote, na kunajumuisha zaidi ya “[kudai] kulijua jina [Lake]” (Mafundisho na Maagano 112:26). Wasaidie watoto kuelewa vyema kile inachomaanisha kumjua Mwokozi kwa hakika.
Shughuli Yamkini
-
Shiriki na watoto kwamba mnamo 1837, baadhi ya Mitume walikuwa wamegeuka dhidi ya Nabii Joseph Smith. Kwa nini ni muhimu kumfuata nabii? (ona mstari wa 15). Wasaidie watoto kutengeneza orodha ya vitu ambavyo Bwana alimwambia Thomas B. Marsh, Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, kufanya (ona Mafundisho na Maagano 112:12–15). Tumia orodha hiyo kujadili namna sisi tunavyoweza kuwa waongofu zaidi kwa Yesu Kristo.
-
Waulize watoto wanafikiri inamaanisha nini kudai kumjua Yesu Kristo lakini hakika hatumjui Yeye (ona Mafundisho na Maagano 112:26). Je, ni nini mstari wa 14 unatufundisha kuwa tunaweza kufanya ili kumjua zaidi Yeye? Wasaidie watoto kuelewa inamamanisha nini “kuchukua msalaba [wetu]” (Tafsiri ya Joseph Smith, Mathayo 16:25–26 [katika kiambatisho cha Biblia]) au “kulisha kondoo [Wake].”
Watie moyo Kujifunza Nyumbani
Waalike watoto kufanya muhtasari wa kile walichojifunza darasani leo. Wasaidie kutengeneza ukumbusho au kuchora picha ambayo itawakumbusha juu ya kile walichojifunza ili waweze kukishiriki na familia zao.