Jitayarishe Kukutana na Mungu
Kufuatilia majukumu yaliyowekwa kwa haki, umoja, na usawa yatutayarisha kukutana na Mungu.
Eliza R. Snow, akizungumza juu ya kuwekwa wakfu kwa Hekalu la Kirtland (ambalo alihudhuria), alisema: “Sherehe hizo za kuwekwa wakfu zinaweza kukaririwa, lakini hakuna lugha ya duniani inayoweza kuelezea maonyesho ya mbinguni ya siku hiyo ya ajabu. Malaika waliwajia wengine, hali ya uwepo wa Mungu ilifikia wote waliokuwepo, na kila moyo ukajazwa na furaha isiyoelezeka na kujawa na utukufu.”1
Maonyesho ya Mungu yaliyotokea katika Hekalu la Kirtland yalikuwa ya kimsingi kwa kusudi la Kanisa lililorejeshwa la Yesu Kristo ili kuleta wokovu na kuinuliwa kwa watoto wa Baba yetu wa Mbinguni.2 Tunapojitayarisha kukutana na Mungu, tunaweza kujua ni majukumu gani tuliyopewa na Mungu kwa kukagua upya funguo takatifu zilizorejeshwa katika Hekalu la Kirtland.
Katika sala ya kuweka wakfu, Nabii Joseph Smith alimsihi Bwana kwa unyenyekevu “kukubali nyumba hii … ambayo umetuamuru kujenga.”3
Wiki moja baadaye, siku ya Jumapili ya Pasaka, Bwana alionekana katika maono makuu na kukubali hekalu Lake. Hii ilitokea Aprili 3, 1836, karibu miaka 182 iliyopita kutoka Jumapili hii ya Pasaka. Ilikuwa pia ni msimu wa Pasaka—mojawapo ya nyakati zile chache wakati Pasaka na chakula cha jioni hupishana. Baada ya ono kufungwa, manabii watatu wa kale, Musa, Elia, na Eliya, walitokea na kukabidhiana funguo ambazo zilikuwa muhimu katika kutimiza kusudi la Bwana kwa Kanisa Lake lililorejeshwa katika kipindi hiki. Lengo hilo limeelezwa kwa urahisi, lakini kwa ufanisi, kama kukusanya Israeli, kuwafunga kama familia, na kuandaa ulimwengu kwa ujio wa pili wa Bwana.4
Kuonekana kwa Eliya na Musa pamoja kulikuwa ni “mlinganisho wa kuvutia … [na] utamaduni wa Kiyahudi, ambayo kulingana nayo Musa na Eliya wangekuja pamoja katika ‘mwisho wa nyakati.’”5 Katika mafundisho yetu, ujio huu ulikamilisha msingi wa urejesho wa funguo fulani “zilizotolewa … kwa siku za mwisho na kwa mara ya mwisho, ambayo ni maongozi ya Mungu ya nyakati jalivu.”6
Hekalu la Kirtland, kote eneo na ukubwa, lilikuwa ni fumbo kiasi. Lakini kwa sababu ya umuhimu wake mkubwa kwa wanadamu, lilikuwa ni la kuinua milele. Manabii wa kale walirejesha funguo za ukuhani kwa maagizo ya kuokoa ya milele ya injili ya Yesu Kristo. Hii ilisababisha furaha kubwa kwa waumini waaminifu.
Funguo hizi hutoa “uwezo kutoka juu”7 kwa majukumu yaliyoteuliwa na Mungu ambayo nyakati na sasa zinajumulisha lengo la kimsingi kwa Kanisa.8 Siku hiyo ya Pasaka ya ajabu katika Hekalu la Kirtland, funguo tatu zilirejeshwa:
Kwanza, Musa alitokea na kukabidhiana funguo za kukusanyika kwa Israeli kutoka pande nne za dunia, ambayo ni kazi ya umisionari.9
Pili, Elia alitokea na kukabidhiana funguo za maongozi ya Mungu ya injili ya Ibrahimu, ambayo inajumuisha urejesho wa agano la Ibrahimu.10 Rais Russell M. Nelson amefundisha kwamba madhumuni ya funguo za agano ni kuwaandaa waumini kwa ufalme wa Mungu. Alisema, “Tunajua sisi ni nani na [tunajua] kile ambacho Mungu anatarajia kutoka kwetu.”11
Tatu, Eliya alitokea na kukabidhiana funguo za uwezo wa kufunganisha katika kipindi hiki, ambazo ni kazi ya historia ya familia na maagizo ya hekalu inayowezesha wokovu kwa walio hai na wafu.12
Kunayo, chini ya uongozi wa Urais wa Kwanza na Jamii ya Mitume Kumi na Wawili, mabaraza matatu makuu katika makao makuu ya Kanisa ambayo yanasimamia majukumu haya matatu yaliyoteuliwa kulingana na funguo zilizorejeshwa katika Hekalu la Kirtland. Nayo ni Baraza Kuu za Umisionari, Baraza Kuu ya Ukuhani na Familia, na Baraza Kuu ya Hekalu na Historia ya Familia.
Tunasimama wapi Leo Katika Kutimiza Majukumu Haya Yaliyoteuliwa ya Kiuungu?
Kwanza, kuhusu urejesho wa funguo za Musa za mkusanyiko wa Israeli, leo karibu wamisionari 70,000 wameenea duniani kote wakihubiri Injili Yake ili kukusanya wateule Wake. Huu ndio mwanzo wa utimilifu wa kazi kubwa na ya ajabu ambayo Nefi alitabiri miongoni mwa Wayahudi na nyumba ya Israeli. Nefi aliona wakati wetu ambapo watakatifu wa Mungu watakuwa kote duniani, lakini idadi yao itakuwa kidogo kwa sababu ya uovu. Hata hivyo, alitabiri kwamba “wamejikinga kwa utakatifu na kwa nguvu za Mungu katika utukufu mkuu.”13 Inapotazamwa kote katika historia fupi ya Kanisa lililorejeshwa, jitihada za umisionari zimekuwa za kushangaza zaidi. Tunaona utimilifu wa maono ya Nefi. Ingawa idadi yetu ni ndogo, tutaendeleza juhudi zetu na kuwafikia wale ambao wataitikia ujumbe wa Mwokozi.
Pili, Elia alijtokea na kukabidhiana funguo za maongozi ya Mungu ya injili ya Ibrahimu, akitangaza kwamba kupitia kwetu na uzao wetu vizazi vyote baada yetu vitabarikiwa. Katika mkutano huu, mwongozo muhimu umewasilishwa ili kusaidia katika kuwakamilisha Watakatifu na kuwaandaa kwa ufalme wa Mungu.14 Matangazo katika kikao cha ukuhani kuhusu akidi za wazee na makuhani wakuu yatafumua nguvu na mamlaka ya ukuhani. Ualimu wa nyumbani na Ualimu wa kutembelea, sasa “uhudumiaji,” kama tunavyofunzwa kwa ufasaha kikao hiki, tutawaandaa Watakatifu wa Siku za Mwisho kukukatana na Mungu.
Tatu, Eliya alikabidhiana funguo za kufunganisha za kipindi hiki. Kwa wale kati yetu walio hai wakati huu, ongezeko la mahekalu na kazi ya historia ya familia ni jambo la ajabu. Mwendo huu utaendelea na kuongezeka mpaka Ujio wa Pili wa Mwokozi, la si hivyo, dunia yote “ingeliangamia kabisa wakati wa kuja kwake.”15
Kazi ya historia ya familia, teknolojia iliyobarikiwa kutoka-mbinguni, imeongezeka kwa kiasi kikubwa katika miaka michache iliyopita. Tutakuwa wakosa hekima tunapozembea kuhusu jukumu hili lililoteuliwa na Mungu na kuturajia kwamba Shangazi Jane au jamaa mwingine aliyejitahidi ataifanya. Acha nishiriki maoni kali ya Rais Joseph Fielding Smith: “Hakuna atakayeepuka kwa wajibu huu mkubwa. Inapaswa pia kwa mtume vile vile kwa mzee mnyenyekevu zaidi [au dada]. Mahali, au sifa, au huduma ya muda mrefu Kanisani … haitastahili yeyote kupuuza wokovu wa mtu aliyefariki.”16
Sasa tuna mahekalu duniani kote na rasilimali za mfuko wa msaada wa wateja wa kusaidia wale walio na mahitaji ambao wako mbali na hekalu.
Kama watu binafsi, tungefanya vizuri kuchunguza juhudi zetu katika kufuata kazi ya umisionari, kazi ya hekalu na historia ya familia, na kujiandaa kukutana na Mungu.
Uadilifu, Umoja, na Usawa mbele ya Bwana Zinashikilia Majukumu haya Matakatifu
Kuhusu haki, maisha haya ndiyo wakati wa watu kujitayarisha kukutana na Mungu.17 Kitabu cha Mormoni kinatoa mifano mingi ya matokeo mabaya wakati watu au makundi wanaposhindwa kuweka amri za Mungu.18
Wakati wa maisha yangu, masuala ya kidunia na wasiwasi umesonga kutoka kwa pande moja hadi nyingine—kutoka kwa shughuli ndogo ndogo za kipuuzi hadi kwa utovu mkubwa wa maadili. Inapendeza kuwa utovu wa maadili umefichuliwa na kukataliwa.19 Utovu wa maadili ni kinyume na sheria za Mungu na jamii. Hata hivyo, wale wanaoelewa mpango wa Mungu pia wanapaswa pia kupinga utovu huo wa maadili, ambao pia ni dhambi. Tangazo la familia kwa ulimwengu linaonya “kwamba watu wanaovunja maagano ya usafi, wanaowatesa wachumba au watoto [au kwa kweli mtu yeyote] … siku moja watasimama kuwajibika mbele za Mungu.”20
Tunapoangalia kote, tunaona uharibifu wa uovu na uraibu kila pembe. Ikiwa, kama watu binafsi, tunajali sana juu ya hukumu ya mwisho ya Mwokozi, tunapaswa kutafuta toba. Ninaogopa watu wengi hawahisi tena kuwajibika kwa Mungu na hawageukii maandiko au manabii kwa uongozi. Ikiwa sisi, kama jamii, tutafakari juu ya madhara ya dhambi, kutakuwa na upinzani mkubwa wa umma dhidi ya ponografia na wanawake kutumiwa kama vyombo.21 Kama Alma alivyomwambia mtoto wake Koriantoni katika Kitabu cha Mormoni, “Uovu haujapata kuwa furaha”22
Kuhusu umoja, Mwokozi alitangaza, “kama hamna umoja ninyi siyo wangu.”23 Tunajua kwamba roho wa ubishi ni wa shetani.24
Katika siku zetu, umuhimu wa maandiko kwa umoja umepuuzwa sana, na kwa watu wengi msisitizo ni juu ya ukabila,25 mara nyingi ikihusu hali, jinsia, rangi na utajiri. Katika mataifa mengi, watu wamegawanyika sana juu ya jinsi ya kuishi. Katika Kanisa la Bwana, utamaduni pekee tunaozingatia na kufundisha ni utamaduni wa injili ya Yesu Kristo. Umoja tunaotaka ni kuunganishwa na Mwokozi na mafundisho yake.26
Tunapoangalia madhumuni ya msingi ya Kanisa, yote yamelingana na usawa mbele ya Bwana 27 na kufuata utamaduni wa injili ya Yesu Kristo. Kwa kuzingatia kazi ya umisionari, sifa za msingi za kubatizwa ni kujinyenyekeza mbele za Mungu na kuja na moyo uliovunjika na roho iliyopondeka.28 Elimu, utajiri, rangi ya ngozi, au asili ya kitaifa hata hazifikiriwa.
Zaidi ya hayo, wamisionari huhudumu kwa unyenyekevu pale ambapo wameitwa. Hawajaribu kuhudumu kulingana na viwango vya ulimwengu vya hali au maandalizi kwa kazi za baadaye. Wanahudumu kwa moyo wao wote, nguvu, akili, na uwezo kokote walikopangiwa. Hawachagui wenzao wamisionari, na wanatafuta kwa bidii kuendeleza sifa za Kristo, ambazo ni msingi katika utamaduni wa Yesu Kristo.29
Maandiko hutoa mwongozo kwa uhusiano wetu muhimu zaidi. Mwokozi alifundisha kwamba amri ya kwanza ilikuwa ni “kumpenda Bwana Mungu wako.” Na ya pili ni, “Mpende jirani yako kama nafsi yako.”30
Mwokozi kisha alielezea kwamba kila mtu ni jirani yetu.31 Kitabu cha Mormoni kinaeleza wazi kwamba haipaswi kuwa, ukabila, au tabaka.32 Lazima tuungane na tuwe na umoja na usawa mbele za Mungu.
Maagizo matakatifu na majukumu ya Mungu hujengwa juu ya nguzo hii. Natarajia kuwa uzoefu wako mwenyewe katika hekalu ungekuwa sawa na wangu. Nilipokuwa nikiondoka kutoka kwa ulimwengu wangu wa kazi huko San Francisco na kufika Hekalu la Oakland, ningepata hisia kubwa ya upendo na amani. Sehemu kubwa ya hiyo ilikuwa nikihisi kuwa nilikuwa karibu na Mungu na makusudi Yake. Ibada za kuokoa zilikuwa lengo langu kuu, lakini sehemu muhimu ya hisia hizo nzuri ni usawa na umoja unaozunguka hekaluni. Kila mtu huvalia nguo nyeupe. Hakuna ushahidi wa utajiri, cheo, au kiwango cha elimu; sisi sote ni ndugu na dada wanaonyenyekea mbele za Mungu.
Katika chumba kitakatifu cha kufunganishwa, ibada ya ndoa ya milele ni sawa kwa kila mtu. Ninapenda ukweli kwamba wanandoa wasio matajiri na wanandoa wenye historia ya utajiri wanapata uzoefu sawa. Wanavaa aina moja ya joho na kufanya maagano yanayofanana katika madhabahu yale yale. Pia wanapokea baraka za ukuhani za milele sawa sawa. Hii inafanyika katika hekalu zuri liliojengwa na zaka za Watakatifu kama nyumba takatifu ya Bwana.
Kutimiza majukumu yaliyoteuliwa ya kiuungu, kulingana na haki, umoja, na usawa mbele ya Bwana, huleta furaha na amani ya kibinafsi katika ulimwengu huu na kututayarisha kwa uzima wa milele katika ulimwengu ujao.33 Hututayarisha kukutana na Mungu.34
Tunaomba kwamba kila mmoja wenu, bila kujali hali yako ya sasa, utashauriana na askofu wako na kustahili kupata sifu ya hekalu.35
Tunashukuru kuwa washiriki wengi wanajitayarisha kwenda hekaluni. Kumekuwa na ongezeko kubwa ya idadi ya watu wazima wanaomiliki sifu ya hekalu kwa miaka mingi. Sifu ya muda mfupi kwa vijana wanaostahiki imeongezeka kwa kasi kwa miaka miwili iliyopita. Kwa kweli waumini waaminifu wengi wa Kanisa hawajawahi kuwa na nguvu sana kuliko hivi sasa.
Kwa kutamatisha, tafadhali muwe na uhakika kuwa viongozi wakuu wa Kanisa wanaosimamia madhumuni takatifu ya Kanisa yaliyoteuliwa hupokea msaada wa kiuungu. Mwongozo huu unatoka kwa Roho na wakati mwingine moja kwa moja kutoka kwa Mwokozi. Aina zote za mwongozo wa kiroho hutolewa. Ninashukuru kwa kupata msaada huo. Lakini mwongozo hutolewa katika wakati wa Bwana, mstari juu ya mstari na amri juu ya amri, kanuni juu ya kanuni,36 wakati “Bwana ajuaye yote anaamua makusudi kutufundisha.”37 Mwongozo kwa Kanisa kwa ujumla huja tu kupitia kwa nabii Wake.
Tumekuwa na fursa ya kumidhinisha Rais Russell M. Nelson kama nabii wetu na Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho katika mkutano huu. Wale kumi na wawili, kama kikundi na watu binafsi, tulipata uzoefu mkubwa wa kiroho tulipoweka mikono yetu juu ya kichwa cha Rais Nelson na Rais Dallin H. Oaks, akiwa kama sauti, tulimtawaza yeye na kumtenga kama Rais wa Kanisa. Ninashuhudia kuwa aliteuliwa mbeleni na ameandaliwa maishani mwake mwote kuwa nabii wa Bwana kwa siku zetu. Katika jina la Yesu Kristo, amina.