Moyo wa Nabii
Tunaweza kufurahi kwamba nabii wa Bwana yuko hapa na kwamba kazi ya Bwana inafanyika katika namna ambayo Ameielekeza kitakatifu.
Nimeomba kwa dhati kwamba Roho Mtakatifu atakuwa na kila mmoja wetu leo katika huu wasaa wa mbinguni. Kile tulichokishuhudia kwa pamoja kimekuwa cha kuvutia sana pale nabii wa 17 wa kipindi hiki cha maongozi ya Mungu ameidhinishwa katika kusanyiko takatifu.
Pale nilipotafuta muongozo kujua mada Bwana angetaka niizungumzie leo, akili yangu ilielekezwa kwenye mazungumzo ya karibuni na Urais wa Kwanza mpya ulioitwa. Katika mjadala huu, mmoja wa washauri alishiriki maneno kwa namna hii: “Ninatumaini kiundani kwamba uumini wa Kanisa unaweza kutambua ukubwa wa kile kilichotokea kwa kuitwa kwa nabii wetu mpya, Rais Russell M. Nelson, na umuhimu na utakatifu wa kusanyiko takatifu ambalo litafanyika katika mkutano mkuu.” Alitoa wazo zaidi, “Imekuwa ni miaka 10, na wengi, hasa vijana wa Kanisa, hawakumbuki au hawajawahi kupitia hili.”
Hii ilinisababisha kukumbuka uzoefu niliopata. Nabii wa kwanza Ninayemkumbuka ni Rais David O. McKay. Nilikuwa na miaka 14 wakati alipofariki. Ninakumbuka hisia za kumpoteza ambazo ziliambatana na kifo chake na machozi katika macho ya mama yangu na, huzuni ulihisiwa na familia yetu yote. Ninakumbuka jinsi maneno “Tafadhali mbariki Rais David O. McKay” yalivyotoka mdomoni mwangu kiuhalisia katika sala zangu kwamba kama nisingekuwa makini, hata kufuatia kifo chake, nilijipata nikitumia maneno hayo hayo. Sikuwa na uhakika kama moyo na akili yangu vingebadilika kuwa na hisia na msimamo ule ule kwa manabii wanaomfuatia. Lakini karibu sawa na wazazi wanaowapenda kila mmoja wa watoto wao, Nilipata upendo, muunganiko, na ushuhuda wa Rais Joseph Fielding Smith, aliyemfuatia Rais McKay, na kila nabii baada ya hapo: Harold B. Lee, Spencer W. Kimball, Ezra Taft Benson, Howard W. Hunter, Gordon B. Hinckley, Thomas S. Monson, na leo Rais Russell M. Nelson. Kwa moyo wote nilimuidhinisha kila nabii kwa mkono ulioinuliwa—na moyo ulioinuliwa.
Kila mmoja wa manabii wetu wapendwa alipofariki, ni kawaida tu kuhisi hali ya huzuni na kupoteza. Lakini huzuni yetu hupunguzwa kwa furaha na tumaini linalokuja tunapopata mojawapo ya baraka kuu ya Urejesho: kwa kuitwa na kuidhinishwa kwa nabii anayeishi duniani.
Kwa mwisho huo, nitaongelea juu ya huu mchakato mtakatifu kama ulivyofuatwa katika siku hizi 90 zilizopita. Nitaielezea katika vipengele vinne: kwanza, kifo cha nabii wetu na utanguzi wa Urais wa Kwanza; pili, kipindi cha muda kusubiri kuundwa upya kwa Urais wa Kwanza mpya; tatu, kuitwa kwa nabii mpya; na nne, kuidhinishwa kwa nabii mpya na Urais wa Kwanza katika kusanyiko takatifu.
Kifo cha Nabii
Mnamo Januari 2, 2018, nabii wetu mpendwa Thomas S. Monson alikwenda upande mwingine wa pazia. Daima atakuwa na nafasi katika mioyo yetu. Rais Henry B. Eyring alitoa mawazo baada ya kifo cha Rais Monson ambayo yanaelezea dhahiri hisia zetu: “Sifa bainifu ya maisha yake, kama ya Mwokozi, itakuwa kujali kwake katika kuwafikia masikini, wagonjwa—hata watu wote—ulimwenguni kote.”1
Rais Spencer W. Kimball alielezea:
“Pale nyota moja inapozama nyuma ya upeo wa macho, nyingine huja kwenye picha, na kifo huzaa uhai.
“Kazi ya Bwana haina mwisho. Hata wakati kiongozi mkuu anapokufa, hakuna hata mara moja Kanisa linakosa uongozi, tunashukuru kwa Majaliwa karimu aliyeupa ufalme wake muendelezo na kudumu. Kama ambavyo imekwishatokea … kabla katika kipindi hiki cha maongozi ya Mungu, watu kwa unyenyekevu hufunika kaburi, hufuta machozi yao, na hugeuza nyuso zao kwa yajayo.”2
Kipindi cha Kitume
Kipindi cha muda kati ya kifo cha nabii na kuundwa upya kwa Urais wa Kwanza kinajulikana kama “kipindi cha kitume.” Katika kipindi hiki, Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, chini ya uongozi wa rais ya akidi, kwa pamoja hushikilia funguo za kusimamia uongozi wa Kanisa. Rais Joseph F. Smith alifundisha, “Kumekuwa daima na kiongozi ndani ya Kanisa, na kama Urais wa Kanisa umeondolewa kwa kifo au sababu nyingine, basi kiongozi wa Kanisa anayefuata ni Mitume Kumi na Wawili, mpaka urais utakapoundwa tena.”3
Kipindi cha kitume cha hivi karibuni kilianza wakati Rais Monson alipofariki mnamo Januari 2, na kukoma siku 12 baadaye mnamo Jumapili, Januari 14, 2018. Katika asubuhi ile ya Sabato, Akidi ya Kumi na Wawili ilikutana katika chumba cha juu cha Hekalu la Salt Lake katika roho ya mfungo na sala, chini ya maelekezo ya usimamizi wa Rais Russell M. Nelson, Mtume mkubwa na Rais wa Akidi ya Kumi na Wawili.
Kuitwa kwa Nabii Mpya
Katika mkutano huu mtakatifu na wa kukumbukwa, wakifuata kigezo kilichoasisiwa vyema katika muungano na kwa umoja, Akina kaka walikaa kulingana na vyeo katika nusu duara ya viti 13 na kunyoosha mikono kwanza kuidhinisha kuundwa kwa Urais wa Kwanza na kisha kumuidhinisha Rais Russel Marion Nelson kama Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Uidhinisho huu ulifuatiwa na Akidi ya Kumi na Wawili kukusanyika katika duara na kuweka mikono juu ya kichwa cha Rais Nelson kumtawaza na kumsimika, Mtume mkuu anayefuata akikaimu kama msemaji.
Rais Nelson kisha akawataja washauri wake, Rais Dallin Harris Oaks, Rais Henry Bennion Eyring, na Rais Oaks kama Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili na Rais Melvin Russell Ballard kama Rais mkaimu wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. Kufuatia kura kama hizo za kuidhinisha, kila mmoja wa Akina kaka hawa alisimikwa kwenye ofisi zao husika na Rais Nelson. Huu ulikuwa ni uzoefu mtakatifu wa kina, wenye hisia za ndani za Roho. Ninatoa kwenu ushahidi hakika kwamba mapenzi ya Bwana, ambayo kwayo tuliomba kwa dhati, yalionekana kwa nguvu katika shughuli na matukio ya siku hiyo.
Kwa utawazo wa Rais Nelson na kuundwa upya kwa Urais wa Kwanza, kipindi cha kitume kilikoma, na Urais wa Kwanza mpya ulioteuliwa ajabu ulianza kufanya kazi bila hata sekunde moja ya kuingiliwa katika kuongoza ufalme wa Bwana duniani.
Kusanyiko Takatifu
Asubuhi hii, mchakato mtakatifu umefikia kilele kwa mujibu wa agizo la kimaandiko lililoelezewa katika Mafundisho na Maagano: “Kwani mambo yote lazima yafanyike katika utaratibu, na kwa ridhaa ya wengi katika kanisa, na kwa sala ya imani,”4 na “Makuhani Wakuu Viongozi watatu, … na kuungwa mkono kwa kuaminiwa, imani, na sala ya kanisa, hufanya akidi ya Urais wa Kanisa.”5
Mzee David B. Haight alielezea tukio lililopita la kile tunachoshiriki leo:
“Sisi tu mashahidi na washiriki katika wasaa mtakatifu zaidi—kusanyiko takatifu kufanyia kazi mambo ya mbinguni. Kama nyakati za kale, kumekuwa na kufunga na sala nyingi zikitolewa na Watakatifu ulimwenguni kote kwamba waweze kupokea hisia za ndani za Roho wa Bwana, ambako ni dhahiri … katika wasaa huu asubuhi ya leo.
“Kusanyiko takatifu, kama jina linavyodokeza, humaanisha wasaa mtakatifu, mtulivu, na wa unyenyekevu wakati Watakatifu hukusanyika chini ya maelekezo ya Urais wa Kwanza.”6
Kina kaka na kina dada, tunaweza kufurahi—hata kusema Hosanna!—kwamba msemaji wa Bwana, nabii wa Mungu, yuko hapa na kwamba Bwana anapendezwa kwamba kazi Yake inafanyika katika namna ambayo Ameielekeza kitakatifu.
Rais Russell M. Nelson
Mchakato huu mtakatifu wa utawazo huongoza kwenye nabii mtakatifu mwingine aliyeitwa. Kama vile Rais Monson alivyokuwa mmoja wa wakazi muhimu kuneemesha dunia hii, ndivyo alivyo Rais Nelson. Amekuwa akitayarishwa kwa kina na kufunzwa mahususi na Bwana kutuongoza katika wakati huu. Ni baraka kuu kwa sasa kuwa na mpendwa Rais Russell M. Nelson kama nabii mwenye upendo na kujitolea—Rais wa 17 wa Kanisa katika kipindi hiki, cha mwisho cha maongozi ya Mungu.
Rais Nelson kweli ni mtu wa kusifika. Nilipata fursa ya kutumikia naye katika Akidi ya Kumi na Wawili kama rais wangu wa akidi kwa miaka 2½. Nimesafiri pamoja naye na kushangazwa na nguvu zake, mtu lazima atembee kwa haraka ili kwenda naye sambamba. Kwa ujumla, ametembelea nchi 133 katika muda wa maisha yake.
Mfikio wake ni kwa wote, wakubwa kwa wadogo. Anaonekana kumjua kila mtu na hasa amejaliwa kukumbuka majina. Wote wanaomjua huhisi kwamba wao ni kipenzi chake. Na ndivyo ilivyo kwa kila mmoja wetu—kwa sababu ya upendo wake wa kweli na kumjali kila mtu.
Ushirika wangu wa awali na Rais Nelson umekuwa ni katika majukumu ya kikanisa, bado pia nimepata kujua maisha ya taaluma kwamba Rais Nelson aliyokuwa nayo kabla ya kuitwa kama Kiongozi Mkuu. Kama wengi wenu mnavyofahamu, Rais Nelson alikuwa daktari mpasuaji wa moyo mashuhuri ulimwenguni na, mapema katika kazi yake ya tiba, mwendelezaji mwanzilishi wa mashine ya moyo na mapafu. Yeye pia alikuwa katika timu ya utafiti ambayo iliunga mkono upasuaji wa kwanza wa moyo wa binadamu mnamo 1951 kwa kutumia mbinu ya kando ya upasuaji. Rais Nelson alifanya upasuaji wa moyo kwa Rais Spencer W. Kimball muda mfupi kabla ya Rais Kimball kuwa nabii.
Cha kupendeza, wakati wito wa Rais Nelson kwenye Akidi ya Kumi na Wawili miaka 34 iliyopita ulisitisha taaluma ya kazi ya tiba ya kuimarisha na kurekebisha mioyo, ulianzisha huduma kama Mtume akijitolea kuimarisha na kurekebisha mioyo ya makumi ya elfu yasiyohesabika ulimwenguni kote, kila mmoja akiwa ameinuliwa na kuponywa kwa maneno yake na matendo ya hekima, huduma, na upendo.
Moyo kama wa Kristo
Ninapopiga taswira ya moyo kama wa Kristo katika matendo ya kila siku, ninamuona Rais Nelson. Sijawahi kukutana na yeyote anayeonyesha kwa mfano sifa hii katika kiwango kikubwa kuliko anavyofanya. Imekuwa ni malezi yasiyo kifani kwangu mimi kuwa katika nafasi ya kuangalia moja kwa moja madhihirisho ya moyo kama wa Kristo wa Rais Nelson.
Ndani ya majuma kadhaa ya wito wangu kwenye Kumi na Wawili mnamo Oktoba 2015, nilipata nafasi ya kuona kwa karibu kidogo maisha ya nyuma ya taaluma ya Rais Nelson. Nilialikwa kuhudhuria tukio ambapo alituzwa kama mpasuaji wa moyo mwanzilishi. Nilipoingia ukumbini, nilishangazwa kuona idadi kubwa ya wenye taaluma pale kutoa heshima na kutambua kazi ambayo Rais Nelson alifanya miaka mingi kabla kama daktari wa madawa na mpasuaji.
Jioni hiyo, wanataaluma wengi walisimama na kuelezea heshima yao na matamanio kwa mchango wa kuonekana wa Rais Nelson katika utaalamu wake wa tiba. Kama ilivyokuwa ya kuvutia kwa kila mwasilishaji katika kuelezea mafanikio mbalimbali ya Rais Nelson, nilistaajabishwa zaidi na maongezi niliyofanya na mtu aliyekaa karibu yangu. Hakujua mimi ni nani, lakini alimjua Rais Nelson, kama Daktari Nelson, mkurugenzi wa programu ya upasuaji wa kifua katika shule ya tiba mnamo 1955.
Mtu huyu alikuwa mwanafunzi wa zamani wa Rais Nelson. Alishiriki kumbukumbu nyingi. Cha kuvutia zaidi ilikuwa ni maelezo yake ya aina ya ufundishaji wa Rais Nelson, ambao, alisema, ulileta kiwango kikubwa cha kuaziriwa. Alielezea kwamba mengi ya mafunzo ya upasuaji wa moyo kwa wanafunzi yalitekelezwa katika chumba cha upasuaji. Hapo, wanafunzi waliangalia na kufanya upasuaji chini ya uangalizi welekevu, kama darasa la maabara. Alishiriki kwamba mazingira ya chumba cha upasuaji chini ya baadhi ya wapasuaji waelekezi yalikuwa ya vurugu, ushindani, yaliyojaa shinikizo, na hata ubinafsi. Mtu huyu aliyaelezea kama mazingira magumu, wakati mwingine hata ya kudhalilisha. Matokeo yake, wapasuaji wanafunzi hata walihisi kazi zao zilikuwa kwenye hatarini.
Kisha akaelezea mazingira ya kipekee yaliyokuwepo katika chumba cha upasuaji cha Rais Nelson. Yalikuwa ya amani, utulivu, na yenye heshima. Wanafunzi walichukuliwa kwa heshima kubwa. Hata hivyo, kufuatia ufafanuzi wa hatua, Daktari Nelson alitarajia kiwango cha juu zaidi cha utendaji kutoka kwa kila mwanafunzi. Mtu huyu aliendelea kuelezea jinsi matokeo mazuri zaidi ya mgonjwa na upasuaji mzuri zaidi vilitoka kwenye chumba cha Daktari Nelson.
Hii hainishangazi hata kidogo. Hiki ndicho nimekuwa nikikiona moja kwa moja, na kubarikiwa nacho katika Akidi ya Kumi na Wawili. Ninahisi kama nimekuwa, katika mawazo, mmoja wa “mwanafunzi wake katika mafunzo.”
Rais Nelson ana njia ya kipekee ya kuwafundisha wengine na kutoa masahihisho katika namna chanya, ya heshima na ya kuinua. Yeye ni mfano halisi wa moyo kama wa Kristo na mfano kwetu sote. Kutoka kwake, tunajifunza kwamba katika hali yoyote tunajipata, matendo yetu na mioyo vinaweza kuwa kufuatana na kanuni za injili ya Yesu Kristo.
Sasa tuna baraka kuu ya kumuidhinisha nabii wetu, Rais Russell M. Nelson. Katika maisha yake yote, amekuza majukumu yake mengi kama mwanafunzi, baba, profesa, mume, daktari, kiongozi wa ukuhani, babu, na Mtume Alitimiza majukumu haya wakati huo—na anaendelea kufanya hivyo—kwa moyo wa nabii.
Akina kaka na akina dada, kile ambacho tumeshuhudia na kushiriki leo, ni kusanyiko takatifu, kinaongoza hata kwenye ushahidi wangu kwamba Rais Russell M. Nelson ndiye msemaji aliyehai wa Bwana kwa wanadamu wote. Mimi pia ninaongezea ushuhuda wangu wa Mungu Baba, wa Yesu Kristo, na jukumu Lake kama Mwokozi wetu na Mkombozi wetu. Katika jina la Yesu Kristo, amina.