Kristo Bwana Amefufuka Leo
Hii ni Jumapili ya Pasaka. Kwa heshima ninatoa ushahidi na kutoa ushuhuda juu ya Kristo aliye hai—Yeye alikufa, akazikwa, akafufuka tena siku ya tatu.”
Akina kaka na akina dada wapendwa, wakati wana wetu walikuwa wadogo, niliwasimulia hadithi kuhusu vitoto vya mbwa na kuwaimbia nyimbo kabla ya wao kulala, ikiwa ni pamoja na “Kristo Bwana amefufuka leo.”1 Wakati mwingine nilibadilisha maneno: “Sasa ni wakati wa kwenda kulala—haleluya. Kwa kawaida wana wetu walishikwa na usingizi; au angalau walijua ikiwa wangelala, ningesita kuimba.
Maneno—angalau maneno yangu—hayawezi kuelezea hisia nilizojawa nazo tangu Rais Russell M. Nelson kwa upendo alipoichukua mikono yangu kwake, na mpendwa Susan akiwa pembeni yangu, na kutoa mwito huu mtakatifu kutoka kwa Bwana ambao ulinistaajabisha na kuniacha nikiwa nalia mara nyingi hizi siku zilizopita.
Katika Sabato hii ya Pasaka, ninaimba kwa furaha, “Haleluya.” Wimbo wa upendo wa ukombozi wa Mwokozi wetu aliyefufuka2 unasherehekea upatanifu wa maagano (ambayo yanatuunganisha kwa Mungu na kwa kila mmoja) na Upatanisho wa Yesu Kristo (ambao unatusaidia kumvua yule mwanaume na mwanamke wa kawaida na kukubali ushawishi wa Roho Mtakatifu3).
Kwa pamoja, maagano yetu na Upatanisho wa Mwokozi wetu yanawezesha na kuadilisha. Kwa pamoja, yanatusaidia kushikilia na kuachilia. Kwa pamoja, yanatia utamu, yanahifadhi, yanatakasa, yanakomboa
Alisema Nabii Joseph Smith: “Yawezekana kwa wengine ikaonekana ni mafundisho mazito sana ambayo tunayazungumzia—uwezo ambao huandika au hufunga duniani na kufungwa mbinguni.” Hata hivyo, katika umri wote wa ulimwengu, wakati wowote Bwana alipokuwa ametoa kipindi cha ukuhani kwa mtu yeyote kwa ufunuo halisi, au kwa kundi lolote la wanadamu, uwezo huu daima umekuwa ukitolewa.”4
Na hivyo ndivyo ilivyo hivi leo. Maagano na ibada takatifu, ambazo hazipatikani kwingineko, yanapokelewa katika nyumba 159 takatifu za Bwana katika nchi 43. Baraka zilizoahidiwa zinakuja kupitia funguo za ukuhani, mafundisho, na mamlaka, yaliyorejeshwa, vikiakisi imani yetu, utiifu, na ahadi za Roho Wake Mtakatifu, kwetu katika vizazi vyetu, kwa muda na milele.
Akina kaka na akina dada katika kila taifa, kabila, na lugha, kanisani kote ulimwenguni, asanteni kwa imani yenu iliyo hai, tumaini, na hisani katika kila hatua. Asanteni kwa kuwa sehemu ya mkusanyiko wa utimilifu wa ushuhuda na uzoefu wa injili ya urejesho.
Akina kaka na akina dada, sisi wote ni wa kila mmoja. Tunaweza tukaunganishwa pamoja katika umoja na kwa upendo,5 katika vitu vyote na katika mahali popote.6 Kama vile Bwana Yesu Kristo hutualika kila mmoja wetu, popote tulipo, vyoyvote hali zetu zilivyo, tafadhali “njoo na uone.”7
Leo hii ninaahidi kwa unyenyekevu “kwa akili na nguvu zote za nafsi yangu,”8 lolote litakalo kuwa au litakalo kuja kuwa, kwa Mwokozi wangu, kwa Ndugu zangu, na kwa kila mmoja wenu.
Kila kitu chema na cha milele kinalenga katika uhalisia hai wa Mungu Baba yetu wa Milele na Mwanaye, Yesu Kristo, na Upatanisho Wake, vikishuhudiwa na Roho Mtakatifu.9 Hii ni Jumapili ya Pasaka. Kwa heshima ninatoa ushahidi na kutoa ushuhuda juu ya Kristo aliye hai—Yeye alikufa, akazikwa, akafufuka tena siku ya tatu, na kupaa mbinguni.10 Yeye ni Alfa na Omega11—pamoja nasi kutoka mwanzo, atakuwa nasi hadi mwisho.
Ninatoa ushuhuda kuhusu manabii wa siku za mwisho, kuanzia Nabii Joseph Smith mpaka Rais Russel M. Nelson, ambaye kwa shangwe tunamuidhinisha leo. Kama watoto wetu wa Msingi wanavyoimba, “Mfuate nabii; yeye anaijua njia.”12 Nashuhudia kwamba, kama ilivyotabiriwa katika maandiko matakatifu, ikijumuisha Kitabu cha Mormoni: Ushuhuda Mwingine wa Yesu Kristo, “ufalme wa Mungu umeanzishwa tena duniani, kama matayarisho kwa Ujio wa Pili wa Masiya.13 Katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.