Kusanyiko Takatifu
Ndugu na akina dada, Rais Nelson ameniomba kwamba niongoze shughuli za kusanyiko takatifu ambalo kwa ajili yake tumekusanyika leo.
Hii ni fursa pekee yenye umuhimu kwa waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ulimwenguni kote.
Kuanzia toka tareha 10 Oktoba, 1880 wakati John Taylor alipoidhinishwa kumrithi Brigham Young kama nabii, mwonaji na mfunuzi na Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, kila mojawapo ya fursa hizi imeonyesha kama kusanyiko takatifu rasmi la jamii ya Kanisa kuelezea sauti ya Kanisa.
Tutaidhinisha kwa akidi na makundi. Popote pale ulipo, unatakiwa usimame pale tu unapoombwa na kuonyesha kwa kuinua mkono wako kama unachagua kuidhinisha wale ambao majina yamewasilishwa. Unatakiwa kuidhinisha pale tu unapoombwa kusimama.
Viongozi Wakuu wenye Mamlaka waliopangwa kwenye Tabenakulo na Ukumbi wa Mkutano kwenye Temple Square wataadhimisha upigaji kura katika sehemu hizo. Katika vituo vya vigingi, mshiriki wa urais wa kigingi ataangalia upigaji kura. Kama yoyote ataidhinisha kinyume chake, watu hao binafsi hawana budi kuwasiliana na marais wa vigingi vyao.
Sasa tunaendelea. Tena, tafadhali simama na idhinisha tu wakati unapoombwa kufanya hivyo.
Tunawaomba washiriki wa Urais wa Kwanza tafadhali msimame.
Inapendekezwa kwamba Urais wa Kwanza umwidhinishe Russell Marion Nelson kama nabii, mwonaji na mfunuzi na Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za mwisho.
Wale wa Urais wa Kwanza wanaokubali, tafadhali onyesheni.
Inapendekezwa kwamba Urais wa Kwanza wamwidhinishe Dallin Harris Oaks kama Mshauri wa Kwanza na Henry Bennion Eyring kama Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza wa Kanisa.
Wale washiriki wa Urais wa Kwanza wanaokubali wanaweza kuonyesha.
Inapendekezwa kwamba Urais wa Kwanza wamwidhinishe Dallin Harris Oaks kama Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili na Melvin Russell Ballard kama Kaimu Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili.
Wale wa Urais wa Kwanza wanaokubali, tafadhali onyesheni.
Inapendekezwa kwamba Urais wa Kwanza wawaidhinishe kama washiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili: M. Russell Ballard, Jeffrey R. Holland, Dieter F. Uchtdorf, David A. Bednar, Quentin L. Cook, D. Todd Christofferson, Neil L. Andersen, Ronald A. Rasband, Gary E. Stevenson, na Dale G. Renlund, Gerrit Walter Gong, na Ulisses Soares.
Wale wa Urais wa Kwanza wanaokubali, tafadhali onyesheni.
Inapendekezwa kwamba Urais wa Kwanza uwaidhinishe washauri katika Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kama manabii, waonaji, na wafunuzi.
Washiriki wa Urais wa Kwanza tafadhali onyesheni.
Urais wa Kwanza sasa wanaweza kuketi.
Tunamkaribisha Mzee Gong na Mzee Soares kuchukuwa nafasi zao pamoja na Akidi ya mitume Kumi na Wawili.
Washiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili tu, ikijumuisha Mzee Gong na Mzee Soares, tafadhali simameni.
Inapendekezwa kwamba Akidi ya Mitume Kumi na Wawili wamwidhinishe Russell Marion Nelson kama nabii, mwonaji, na mfunuzi na Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, pamoja na washauri wake na washiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kama walivyoletwa na kuidhinishwa na Urais wa Kwanza.
Washiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili wanaokubali, tafadhali onyesheni.
Mnaweza kuketi.
Tunawaomba Viongozi Wakuu Wenye Mamlaka na washiriki wa Uaskofu Simamizi tafadhali simameni.
Inapendekezwa kwamba Viongozi Wakuu wote wa Sabini Wenye Mamlaka na Washiriki wa Uaskofu Simamizi Wamwidhinishe Russell Marion Nelson kama nabii, mwonaji, na mfunuzi na Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, pamoja na washauri wake na washiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kama walivyoletwa na kuidhinishwa na Urais wa Kwanza.
Viongozi Wakuu wote wa sabini Wenye Mamlaka na Washiriki wa Uaskofu Saidizi wanaokubali, tafadhali onyesheni.
Mnaweza kuketi.
Tunawaomba wafuatawo tafadhali msimame popote pale ulipo ulimwenguni: Sabini wa Maeneo, baba wakuu waliotawazwa, makuhani wakuu, na wazee.
Inapendekezwa kwamba Russell Marion Nelson aidhinishwe kama nabii, mwonaji, na mfunuzi na Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, pamoja na washauri wake na washiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kama walivyoletwa na kuidhinishwa.
Wote wanaokubali, tafadhali onyesheni.
Wanaopinga wanaweza kuonyesha.
Tafadhali ketini.
Washiriki wote wa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama—yaani wanawake wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea—tafadhali simameni.
Inapendekezwa kwamba Russell Marion Nelson aidhinishwe kama nabii, mwonaji, na mfunuzi na Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, pamoja na washauri wake na washiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kama walivyoletwa na kuidhinishwa.
Wote wanaowakubali, tafadhali onyesheni kwa ishara ya kuinua mkono.
Yeyote anayepinga anaweza kuonyesha.
Mnaweza kuketi.
Wale wote walio na Ukuhani wa Haruni—yaani, makuhani wote waliotawazwa, waalimu, na mashemasi—tafadhali simameni.
Inapendekezwa kwamba Russell Marion Nelson aidhinishwe kama nabii, mwonaji, na mfunuzi na Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, pamoja na washauri wake na washiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kama walivyoletwa na kuidhinishwa.
Wote wanaowakubali, tafadhali onyesheni kwa ishara ya kuinua mkono.
Yeyote anayepinga anaweza kuonyesha.
Mnaweza kuketi.
Wasichana walio na umri wa miaka 12 mpaka miaka 18 tafadhali simameni.
Inapendekezwa kwamba Russell Marion Nelson aidhinishwe kama nabii, mwonaji, na mfunuzi na Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, pamoja na washauri wake na washiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kama walivyoletwa na kuidhinishwa.
Wote wanaowakubali, tafadhali onyesheni kwa ishara ya kuinua mkono.
Yeyote anayepinga anaweza kuonyesha.
Mnaweza kuketi.
Sasa tunaomba kwamba waunimi wote, popote pale mlipo, pamoja na hao waliosimama hii punde, tafadhali simameni.
Inapendekezwa kwamba Russell Marion Nelson aidhinishwe kama nabii, mwonaji, na mfunuzi na Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, pamoja na washauri wake na washiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kama walivyoletwa na kuidhinishwa.
Wote wanaowakubali, tafadhali onyesheni kwa ishara ya kuinua mkono.
Yeyote anayepinga anaweza kuonyesha.
Mnaweza wote kuketi.
Asanteni, ndugu na akina dada, kwa upendo wenu na msaada.