Kuwakubali Maofisa wa Kanisa
Tunatambua kuwa ripoti ya takwimu za Kanisa ambayo kwa desturi huwasilishwa wakati wa kikao hiki cha Aprili cha Mkutano Mkuu sasa itachapishwa katika LDS.org mara tu baada ya mkutano huu na itajumuishwa katika toleo la Mkutano Mkuu la majarida ya Kanisa.
Na sasa nitawawasilisha Maofisa Wakuu na Sabini wa Maeneo wa Kanisa kwa ajili ya kura ya kuwakubali, na baada ya hapo Ndugu Kevin R. Jergensen, mkurugenzi mkuu wa Idara ya Ukaguzi ya Kanisa, atasoma ripoti ya ukaguzi.
Kwa sababu ya wito wao kuhudumu kama washiriki wapya wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, inapendekezwa kwamba tunawaachilie Wazee Gerrit W. Gong na Ulisess Soares kutoka kuhudumu kama washiriki wa Urais wa Sabini.
Na pia, tunawachilie Wazee Craig C. Christensen, Lynn G. Robibins, na Juan A. Uceda kutoka kwenye huduma yao kama washiriki wa Urais wa Sabini, ifikapo Agosti 1, 2018.
Wale wangependa kuonyesha shukrani zao kwake Ndugu hawa kwa huduma yao ya kujitolea, tafadhali onyesheni.
Inapendekezwa kwamba tuwaachilie wafuatao kutoka kwenye huduma yao kama Sabini wa Eneo: Steven R. Bangerter, Matthew L. Carpenter, Mathias Held, David P. Homer, Kyle S. McKay, R. Scott Runia, na Juan Pablo Villar.
Wale ambao wangependa kuungana nasi katika kutoa shukrani kwa Ndugu hawa kwa huduma yao ya kujitolea mnaweza kufanya hivyo kwa kuinua mkono juu.
Inapendekezwa kwamba tuwapumzishe kwa moyo wa shukrani, Dada Bonnie L. Oscarson, Carol F. McConkie, na Neil F. Marriott kama Urais Mkuu wa Wasichana. Vile vile tunawapumzisha washiriki wa bodi kuu ya Wasichana, ambao wamehudumu vyema sana.
Wale wote wanaopenda kuungana nasi katika kutoa shukrani kwa wakina dada hawa kwa huduma yao bora, na ya kujitoa, tafadhali waonyeshe.
Imependekezwa kwamba tumwaachilie Dada Bonnie H. Cordon kutoka kuhudumu kama Mshauri wa Kwanza katika Urais Mkuu wa Msingi.
Wote wanaotaka kuonyesha shukrani kwa Dada Cordon wanaweza kufanya hivyo kwa mkono ulioinuliwa.
Imependekezwa kwamba tuidhinishe wafuatao kama washiriki wa Urais wa Sabini, kutoka sasa: Wazee Carl B. Cook na Robert C. Gay.
Wafuatao pia watauhudumu kama washiriki wa Urais wa Sabini, ifikapo Agosti 1, 2018: Wazee Terence M. Vinson, José A. Teixeira, na Carlos A. Godoy.
Wote wanaopendelea, tafadhali dhihirisheni.
Wale wanaopinga, ikiwa kuna yeyote.
Inapendekezwa kwamba tuwakubali wafuatao kama Viongozi wenye Mamlaka wa Sabini wapya: Steven R. Bangerter, Matthew L. Carpenter, Jack N. Gerard, Mathias Held, David P. Homer, Kyle S. McKay, Juan Pablo Villar, na Takashi Wada.
Wote wanaokubali, tafadhali onyesheni.
Wale wanaopinga, kwa ishara hiyo hiyo.
Inapendekezwa kwamba tuwakubali wafuatao kama Sabini wa Eneo wapya: Richard K. Ahadjie, Alberto A. Álvarez, Duane D. Bell, Glenn Burgess, Víctor R. Calderón, Ariel E. Chaparro, Daniel Córdova, John N. Craig, Michael Cziesla, William H. Davis, Richard J. DeVries, Kylar G. Dominguez, Sean Douglas, Michael A. Dunn, Kenneth J. Firmage, Edgar Flores, Silvio Flores, Saulo G. Franco, C. Alberto Genaro, Mark A. Gilmour, Sergio A. Gómez, Roberto Gonzalez, Virgilio Gonzalez, Spencer R. Griffin, Matthew S. Harding, David J. Harris, Kevin J. Hathaway, Richard Holzapfel, Eustache Ilunga, Okechukwu I. Imo, Peter M. Johnson, Michael D. Jones, Pungwe S. Kongolo, G. Kenneth Lee, Aretemio C. Maligon, Edgar A. Mantilla, Lincoln P. Martins, Clement M. Matswagothata, Carl R. Maurer, Daniel S. Mehr II, Glen D. Mella, Isaac K. Morrison, Yutaka Nagatomo, Allistair B. Odgers, R. Jeffrey Parker, Victor P. Patrick, Denis E. Pineda, Henrique S. Simplicio, Jeffrey H. Singer, Michael L. Staheli, Djarot Subiantoro, Jeffrey K. Wetzel, Michael S. Wilstead, Helmut Wondra, and David L. Wright,
Wote wanaokubali, tafadhali onyesheni.
Wale wanaopinga, kama yuko.
Imependekezwa kwamba tumwidhinishe Bonnie H. Cordon kuhudumu kama Rais Mkuu wa Wasichana, pamoja na Michelle Lynn Craig kama Mshauri wa Kwanza na Rebecca Lynn Craven kama mshauri wa pili.
Wote wanaokubali, wanaweza kuonyesha.
Wanaopinga wanaweza kuonyesha vivyo hivyo.
Inapendekezwa kwamba tumwidhinishe Lisa Rene Harkness ahudumu kama Mshauri wa Kwanza katika Urais Mkuu wa Msingi.
Wote wanaokubali, wanaweza kuonyesha.
Wale wanaopinga, kama yuko.
Inapendekezwa kwamba tuwakubali Viongozi Wakuu wengine, Sabini wa Eneo, na Urais Mkuu wa Makundi Saidizi kama ilivyo sasa.
Wote wanaokubali, tafadhali onyesheni.
Wale wanaopinga, kama yuko.
Rais Nelson, upigaji kura umekamilika. Tunawaalika wale wote ambao inawezekana kuwa wamepinga mapendekezo yo yote kati ya haya kuwasiliana na marais wao wa vigingi.
Kwa kura za kukubali ambazo zimefanyika punde tu, sasa tunao viongozi wakuu wenye mamlaka 116. Karibia asilimia 40 ya hao wamezaliwa nje ya Marekani—huko Ujerumani, Brazili, Mexico, New Zealand, Scotland, Kanada, Korea Kusini, Guatemala, Arjentina, Italia, Zimbabwe, Urugwai, Peru, Afrika Kusini, Samoa ya Kiamerika, Uingereza, Puerto Rico, Australia, Venezuela, Kenya, Ufilipino, Ureno, Fiji, China, Japani, Chile, Colombia, na Ufaransa.
Wakina kaka na wakina dada, asanteni kwa imani na sala zenu endelevu kwa niaba ya viongozi wa Kanisa.
Sasa tunawaalika Viongozi Wakuu Wenye Mamlaka wapya na Urais Mkuu Mpya wa Wasichana, kuchukua nafasi zao jukwaani.