Njia Sahihi ya Furaha
Tunawaomba nyinyi kama walimu wa nyumbani muwe wajumbe wa Mungu kwa watoto Wake, muwapende na muwajali na muwaombee wale watu ambao mmepewa jukumu juu yao.
Si muda mrefu umepita dada mseja, ambaye nitamwita Molly, alirudi nyumbani kutoka kazini akiwa amegundua kama inchi mbili (5nbcm) za maji zimefunika sakafu yote ya nyumba yake ya chini. Mara moja akagundua kwamba majirani zake, ambao walikuwa watumia bomba moja la maji taka, lazima wamefanya ufuaji usio wa kawaida na kuoga siku ile kwa sababu yeye alipata maji yote machafu.
Baada ya kumwita rafiki aje kumsaidia, wawili hao wakaanza kutoa maji na kudeki. Mara kengele ya mlangoni ikalia. Rafiki yake akamwita kwa sauti, “Ni walimu wako wa nyumbani!”
Molly alicheka. “ Ni siku ya mwisho wa mwezi” akajibu, “lakini naweza kukuhakikishia kuwa siyo walimu wangu wa nyumbani”
Akiwa miguu pekupeku, suruali iliyolowa, nywele amezifunga bandana, na amevaa glavu nzuri ya kisasa, Molly alitembea kuelekea mlangoni. Lakini sura yake ngumu haikuweza kulingana na sura ngumu iliyosimama mbele ya macho yake. Ilikuwa ni walimu wake wa nyumbani!
“Wewe ungeweza kunidanganya u rafiki wa fundi bomba!” Aliniambia baadaye. “Huu ulikuwa ni muujiza wa ualimu wa nyumbani—aina ile Ndugu wa ukuhani wanaosimulia katika hotuba za mkutano mkuu!” Aliendelea: Lakini, nikiwa tu najaribu kufanya maamuzi kama niwapige busu au niwape mopu, wao,wakasema, ‘Ee Molly, pole. Tunakuona una shughuli nyingi. Tusingependa kukuingilia, hivyo tutakuja wakati mwingine.’ Na wakatoweka.”
“Walikuwa akina nani? rafiki yake akasema kutoka sehemu ya nyumba ya gorofa ya chini.
“Nilitaka kusema, ‘Ilikuwa wazi si wale Wanefi Watatu,’” Molly alikiri, “lakini nilijizuia mwenyewe na kusema kimya kimya sana, ‘Ilikuwa walimu wangu wa nyumbani, lakini wao walihisi haukuwa wakati muafaka wa kuacha ujumbe wao.’”1
Ndugu zangu wa ukuhani, naomba tutazame kwa kifupi wajibu wetu wa ukuhani kama ilivyofafanuliwa kama “chanzo cha kwanza cha msaada katika Kanisa” kwa watu wake binafsi na kwa familia.2 Misitu mzima umetolewa dhabihu ili kutoa karatasi ili kupanga na kisha kupanga tena. Maelfu ya hotuba zimetolewa ili kujaribu kuwatia moyo. Ni wazi hakuna wakala wa usafirishaji wa Freudia popote ambaye pengine angeweza kupanga idadi ya safari za hatia ambazo jambo hili limechochea. Lakini bado tunahangaika kufikia popote jirani na kiwango kinachokubalika cha utendaji juu ya amri za Bwana ya “kuliangalia kanisa daima”3 kupitia njia ya ukuhani ya ualimu wa nyumbani.
Sehemu ya changamoto tunayokabiliana ni kubadilika kwa kidemografia kwa Kanisa. Waumini wetu sasa wakiwa wamesambaa katika kata na matawi yapatayo zaidi ya 30,000, yaliyoko katika mataifa na nchi 188, ni changamoto kubwa zaidi sasa kutembelea nyumba za kina kaka na dada zetu kuliko ilivyokuwa katika siku za mwanzo za Kanisa wakati ambapo jirani alimfundisha jirani katika kitu fulani kilichoitwa “ ualimu katika mtaa.”
Zaidi ya hayo, katika matawi mengi ya Kanisa, kuna idadi ndogo ya wenye ukuhani kufanya ualimu wa nyumbani, ikiwaacha wale wanaoweza wakiwa na watu wengi hadi kufikia familia 18 au 20—au zaidi—za kuhudumia. Panaweza pia kuwa na hoja za umbali mrefu wa kutembea, gharama kubwa ya usafiri na uhaba wa upatikanaji wa usafiri, na urefu wa masaa ya kufanya kazi katika siku na wiki za kazi. Ongeza juu ya hii adha za kiutamaduni ya baadhi ya watu kutopenda kutembelewa nyumbani na hoja za kiusalama, ambazo ziko katika sehemu nyingi katika sehemu yoyote ya ujirani ulimwenguni—ndiyo tunaanza kuona ugumu wa tatizo hili.
Ndugu zangu katika ukuhani, katika ubora wa ulimwengu wote na katika mazingira ambako inaweza kufanyika, matembezi ya kila mwezi katika kila nyumba bado ni jambo jema ambalo Kanisa linapaswa kuendelea kujitahidi kufanya. Lakini ukitambua kwamba katika sehemu nyingi duniani kuzunguka dunia kutimiza jambo kama hilo si rahisi na kwamba tunasababisha ndugu zetu makuhani kujisikia kama washindwa pale tunapowaomba wafanye kile ambacho kinaonekana kiukweli hakiwezekani, Urais wa Kwanza uliandika kwa viongozi wa ukuhani wa Kanisa mnamo Disemba 2001 wakitoa ushauri huu wenye maongozi, na usaidizi: “Kuna maeneo katika Kanisa, waliandika, ambako … ualimu wa nyumbani kwa kila nyumba kila mwezi yawezekana kutowezekana kwa sababu ya idadi isiyotosheleza ya ndugu wa ukuhani wanaohudhuria kikamilifu na changamoto nyingine kadhaa za eneo husika. Tumeshataja baadhi yake. Patokeapo mazingira kama haya, viongozi wanapaswa kufanya kila lililo katika uwezo wao kutumia rasilimali walizonazo ili kumwaangalia na kumuiimarisha kila muumini.”4
Ndugu zangu wa ukuhani, kama kata au tawi langu ningekabiliwa na mazingira ya ugumu wa jinsi hii, mwenza wangu Kuhani wa Haruni na mimi tungetumia ushauri huu wa Urais wa Kwanza (ambao sasa ni sera katika kitabu cha mwongozo) katika njia hii: Kwanza, bila kujali ni miezi mingi kiasi gani itatuchukua kutimiza hili, tungetimiza mamlaka yetu ya kimaandiko ya “kutembelea nyumba ya kila muumini,”5 kutengeneza ratiba ambayo ingetupeleka kwenye nyumba hizo kwenye kalenda iwezekanayo na kivitendo. Kwa msingi wa ratiba hiyo tutaupa kipaumbele cha juu muda uliopo na kwa mawasiliano ya mara kwa mara kwa wale wanaotuhitaji sisi zaidi—wachunguzi ambao wanafundishwa na wamisionari, waongofu waliobatizwa hivi karibuni, walio wagonjwa, wapweke, wasiohudhuria kila mara, familia za mzazi mmoja ambazo bado wana watoto nyumbani, na kadhalika.
Wakati tukifanya kazi kupitia ratiba kutembelea nyumba zote, ambayo yaweza kuchukua miezi kadhaa kukamilisha, tungeweza kufanya mawasiliano ya aina nyingine kwa watu binafsi na kwa familia kupitia njia yo yote Bwana aliyoiweka. Ni dhahiri tungeziangalia familia zetu kanisani na kama maandiko yanavyosema, “ningeongea na mmoja na mwingine kuhusiana na ustawi wa nafsi zao.”6 Kwa nyongeza, tungepiga simu, kutuma barua pepe, na ujumbe wa simu, hata kurekodi ujumbe wa salamu kwa njia mojawapo ya vyombo vya habari vya kijamii vilivyopo. Ili kusaidia kutatua shida maalumu, tungeweza kutuma nukuu ya kimaandiko au mstari kutoka katika hotuba ya mkutano mkuu au Ujumbe wa Mormoni uliotolewa kutoka kwenye utajiri mkubwa wa maandishi kwenye LDS.org. Katika lugha ya Urais wa Kwanza, tungefanya kadiri tuwezavyo chini ya mazingira tunayokabiliana nayo kwa kutumia rasilimali zinazopatikana kwetu.
Ndugu zangu, ombi ninalolifanya usiku wa leo ni kwa ninyi kuinua ono lenu juu ya ualimu wa nyumbani. Tafadhali, katika njia mpya zaidi, bora na mjione wenyewe kama wajumbe wa Bwana kwa watoto Wake. Hilo lina maana ni kuacha nyuma utamaduni wa hasira, mfano wa sheria ya Musa—kama, kalenda inasema ni mwisho- wa- mwezi katika hiyo wewe unaharakisha ili kuacha ujumbe wa maandiko kutoka kwenye magazeti ya Kanisa ambayo familia ilikwisha usoma. Tungetumaini, kuliko, kwamba wewe uanzishe, kipindi cha uhalisia, cha kiinjili juu ya kuwajali waumini, kuwaangalia waumini na kujaliana, mkitatua shida za kiroho na kimwili kwa njia yoyote inayoleta usaidizi.
Juu ya nini cha “muhimu” kama mwalimu wa nyumbani, kila kitu ufanyacho ni “muhimu,” hivyo vitolee taarifa vyote! Ripoti ya muhimu kuliko zote ni namna gani umebariki na kuwajali wale walio chini ya usimamizi wako, mambo ambayo hayana uhusiano na kalenda maalumu au eneo mahususi. Kitu cha muhimu ni kwamba wewe unawapenda watu wako na unatekeleza amri ya “kuliangalia kanisa daima.”7
Mnamo Mei 30 mwaka uliopita, rafiki yangu Troy Russell alilitoa gari lake dogo la mizigo kutoka kwenye gereji yake akienda kutoa msaada bidhaa kwenye Viwanda vya Deseret. Alihisi tairi lake la nyuma likizunguka kwenye tuta. Akidhania baadhi ya vitu vimeanguka kutoka garini, akatoka na kugundua kwamba mtoto wake mdogo wa kiume wa umri–wa miaka–tisa ameanguka kifudifudi barabarani. Makelele ya mshituko, baraka za ukuhani, wahudumu wa paramedika, na wafanya kazi wa hospitali walikuwa, katika hali yoyote, hawakufua dafu. Austen alikuwa ameaga.
Asiweze kulala au kupata amani, Troy hakuweza kufarijika, Yeye alisema lilikuwa zaidi ya analoweza kubeba na kwamba hatoweza kuendelea Lakini katika kile kipindi kifupi cha machungu kulikuja nguvu tatu za kukomboa.
Kwanza kulikuwa upendo na roho wa uhakikisho wa Baba wa Mbinguni, uwepo uliowasilishwa kupitia Roho Mtakatifu ambaye alimfariji Troy, kwa upendo akamfundisha na kumnong’oneza kwamba Mungu anajua kila kitu juu ya kumpoteza Mwana mzuri na mkamilifu. Pili alikuwa mke wake, Deedra, ambaye alimshika Troy mikononi mwake na kumpenda na akamkumbusha kwamba naye pia amepoteza mwana yule na kwamba amedhamiria hatampoteza na mume pia. Wa tatu katika hadithi hii ni John Manning, mwalimu wa nyumbani maalum.
Mimi sijui katika ratiba ipi John na mwenza wake mdogo walifanya matembezi katika nyumba ya Russell, au ujumbe wao ulikuwa ni upi walipofika huko, au namna gani waliripoti tukio hili. Kile ninachokijua ni kwamba majira ya kuchipua yaliyopita Kaka Manning alishuka na kumnyakua Troy Russell kutoka kwenye janga lile la barabarani kama vile tu alikuwa akimnyakua mtoto Austin mwenyewe. Kama vile mwalimu wa nyumbani au mlinzi au ndugu katika injili alivyopaswa kuwa, John alitimiza uchungaji wa ukuhani na kumtunza Troy Russell. Alianza kwa kusema, “Troy, Austin anakutaka wewe usimame kwa miguu yako—ikijumuisha kuwa kwenye uwanja wa mpira wa kikapu—kwa hiyo nitakuwa hapa kila asubuhi saa 11:15. Uwe tayari kwa sababu sitaki mimi nije kukuamsha— na ujue Deedra hatopendezwa na hilo.
“Sikupenda kwenda,” Troy alinieleza baadaye, “kwa sababu daima nimekuwa nikimchukua Austin pamoja nami asubuhi zile na nilijua kumbu kumbu hizo zingekuwa na uchungu mwingi. Lakini John alisisitiza, basi nikaenda. Tangu siku ile ya kwanza niliporudi pale, tuliongea—au pengine mimi niliongea na John alisikiliza. Nilizungumza njia nzima hadi kanisani na kisha hadi nyumbani. Wakati mwingine niliongea nikiwa nimepaki gari njiani na kuangalia jua likichomoza juu ya Las Vegas. Mwanzoni ilikuwa vigumu, lakini kadiri nilivyoendelea nilijiona nimepata nguvu zangu katika mtindo wa taratibu sana wa futi 6 inchi 2 (1.88 m) mcheza mpira wa Kanisa, mwenye utupaji wa wazi wa hovyo, lakini ni nani aliyenipenda na kunisikiliza hadi jua hatimaye kimechomoza tena juu ya maisha yangu.”8
Ndugu zangu wa ukuhani, tunapozungumza juu ya ualimu wa nyumbani, au huduma ya ulinzi, au huduma binafsi ya kikuhani—au ita utakavyo—hili ndilo tunaloliongelea. Tunawaombeni ninyi kama walimu wa nyumbani kuwa wajumbe wa Mungu kwa watoto Wake, kuwapenda, kuwajali na kuwaombea watu uliopewa wajibu juu yao, kama vile sisi tunavyowapenda na kuwajali na kuomba kwa ajili yenu. Na muwe macho katika kuchunga zizi la Mungu katika njia zinazolingana na mazingira yenu, ninaomba, katika jina la yule Mchungaji Mwema wetu sote, ambaye mimi ni shahidi wake, hata Bwana Yesu Kristo, amina.