Kuwa na Lengo Kuu kwa Kristo
Sisi tunakuwa na lengo kuu kwa Kristo tunapohudumu kwa uaminifu, kukubali kwa unyenyekuvu, kusali kwa hamasa, na kushiriki kwa kustahili.
Wapendwa ndugu na dada zangu, leo ningependa kuzungumza na vijana wa Kanisa pamoja na wamisionari wetu wa ajabu. Bila shaka, ndugu na akina dada ambao ni vijana moyoni mnakaribishwa kwa moyo mkunjufu kusikiliza.
Agosti 12, iliyopita Rais Russell M. Nelson aliweka wakfu Hekalu la Sapporo—hekalu la tatu katika Japani. Hekalu la Sapporo limejengwa kaskazini mwa Japani katika mahali panapoitwa Hokkaido Kama Utah, Hokkaido yalikuwa makazi ya watangulizi wachapakazi, wenye kufanya kazi kwa bidii.
Mnamo 1876, mwalimu mashuhuri aliyeitwa Dkt. William Clark1 alialikwa kuja Hokkaido kufundisha. Aliishi Japani kwa miezi nane tu, lakini roho yake ya Kikristo iliacha alama ya kudumu kwa wanafunzi wake vijana ambao hawakuwa Wakristo. Kabla ya kuondoka, aliwapa wanafunzi wake ujumbe wa kuagana ambao unaishi milele kwenye sanamu hii ya shaba.2 Alisema, “Vijana, muwe na lengo kuu!”— “Muwe na lengo kuu kwa Kristo.”3 Tamko lake la “Kuwa na lengo kuu kwa Kristo” linaweza kusaidia moja kwa moja maamuzi ya kila siku kwa Watakatifu wa Siku za mwisho wa leo.
Inamaanisha nini “kuwa na lengo kuu kwa Kristo”? Kuwa na lengo kuu kwa Kristo inamaanisha kuwa na hamasa, kulenga, na kujitolea kwa dhati katika kazi Yake. Kuwa na lengo kuu kwa Kristo mara chache itamaanisha kwamba sisi tumechaguliwa kwa ajili ya heshima ya umma. Kuwa na lengo kuu kwa Kristo inamaanisha kwamba tunahudumu kwa uaminifu na kwa bidii katika kata zetu na matawi bila malalamiko na kwa mioyo yenye furaha.
Wamisionari wetu wanohudumu ulimwenguni kote ni mifano mizuri ya hao ambao kwa kweli wana lengo kuu kwa Kristo. Miaka michache iliyopita, Dada Yamashita nami tulihudumu katika misheni ya Japani Nagoya. Wamisionari wetu walikuwa na lengo kuu kwa Kristo. Mmoja wa wamisionari hao alikuwa kijana aliyeitwa Mzee Cowan.
Mzee Cowan hakuwa na mguu wa kulia kwa sababu ya ajali ya baiskeli ya ujanani. Wiki chache baada ya yeye kuingia katika misheni, nilipokea simu kutoka kwa mwenzi wake. Mguu wa bandia wa Mzee Cowan ulikuwa umevunjika wakati alipokuwa anaendesha baiskeli yake. Tulimpeleka kwenye mahali pazuri pa kuukarabati, na pale katika chumba cha binafsi, niliuona mguu wake wa mara ya kwanza. Nilitambua jinsi alivyokuwa anateseka. Mguu wake wa bandia ulikarabatiwa, na alirudi kwenye eneo lake.
Hata hivyo, wiki zilivyozidi kuendelia, mguu wake wa bandia uliendelea kuvunjika tena na tena. Daktari Mshauri wa Eneo alipendekeza kwamba Mzee Cowen arudi nyumbani kwa uwezekano wa kupangiwa upya misheni. Nilipinga ushauri huu kwa sababu Mzee Cowan alikuwa mmisionari mwenye uwezo mkubwa, na alitamani sana kubaki Japani. Pole pole hata hivyo, Mzee Cowen alianza kukabili udhaifu wake wa kimwili. Licha ya haya, hakunung’unika wala kulalamika.
Tena, nilishauriwa kwamba Mzee Cowan aruhusiwe kuhudumu mahali ambapo hatahitajika kuendesha baiskeli. Nilitafakri kuhusu hali hii. Nilifikiria kuhusu Mzee Cowan na maisha yake ya baadaye, na nilisali kuhusu jambo hili. Nilisikia kushawishiwa kwamba, ndio, Mzee Cowan hana budi kurudi nyumbani na kungoja kupangiwa upya. Nilimpigia simu na kumweleza upendo wangu kwake na kujali na nilimwambia kuhusu uamuzi wangu. Hakusema lolote kunijibu. Niliweza tu kumsikia akilia upande mwingine wa simu. Nilisema,”Mzee Cowan, huna haja ya kunijibu sasa hivi. Nitakupigia tena kesho. Tafadhali fikiria mapendekezo yangu kwa sala ya dhati.”
Nilipompigia simu asubuhi iliyofuata, kwa unyenyekevu alisema atafuata ushauri wangu.
Wakati wa usaili wangu wa mwisho naye, nilimwuliza swali hili: “Mzee Cowan, Je, uliomba kwenye maombi yako ya umisionari kupelekwa kwenye misheni ambako hutahitaji kuendesha baiskeli?”
Alisema, Ndiyo, Rais, niliomba.”
Nikamjibu, “Mzee Cowan, uliitwa kwenda Misheni ya Japan Nagoya ambako ungetakiwa kuendesha baiskeli. Je, ulimweleza hivi rais wako wa kigingi?”
Nilishangazwa na jibu lake. Alisema,”Hapana, sikumwambia. Niliamua kwamba kama huko ndiko Bwana alikoniita, nitakwenda kwenye ukumbi wa michezo ya mazoezi ya viungo na kuufanyia mazoezi mwili wangu kuweza kuendesha baiskeli.”
Katika kuhitimisha usaili wetu, aliniuliza swali hili na machozi katika machoni mwake: “Rais Yamashika, kwa nini nilikuja Japani? Kwa nini nipo hapa?
Nilimjibu bila kusita: Nilimjibu bila kusita, “Mzee Cowan, Najua sababu moja ya kuja hapa. Ulikuja hapa kwa manufaa yangu. Nimekuja kuelewa ni kijana gani mwenye uwezo mkubwa nimekuwa nikihudumu pamoja naye. Nimebarikiwa kukujua.”
Nafurahi kutoa taarifa kwamba Mzee Cowan alirudi nyumbani kwake anakokupenda na alipangiwa upya kuhudumu katika misheni ambako angetumia gari kwa safari zake. Ninajivunia sio tu kwa Mzee Cowan bali kwa wamisionari wote ulimwengu mzima wanaohudumia kwa hiari bila kunung’unika au kulalamika. Asanteni,wazee na akina dada, kwa imani yenu, kulenga kwenu, na lengo lenu kuu lenye nguvu kwa Kristo.
Kitabu cha Mormoni kina maelezo mengi ya hao ambao walikuwa na lengo kuu kwa Kristo. Alma Mdogo kama kijana alilitesa Kanisa na waumini wake. Baadaye alipitia matukio ya kuvutia ya mabadiliko ya moyo na akahudumu kama mmisionari mwenye nguvu. Alitafuta mwongozo wa Bwana, na aliwabariki wenza wake alipohudumu pamoja nao. Bwana alimuimarisha, na aliyashinda majaribu aliyokumbana nayo.
Alma huyu alimpa mwanawe Helamani ushauri ufuatao:
“Wote watakaoweka imani yao katika Mungu watasaidiwa kwa majaribu yao, na taabu zao, na mateso yao. …
“… Tiini amri za Mungu. …
“Shauriana na Bwana kwenye matendo yako yote, na atakuongoza kwa yale mema.”4
Mwana wetu wa pili aliishi kiasi kikubwa cha maisha yake ya ujana mbali na Kanisa. Alipofikia umri wa miaka 20, alipata tukio ambalo lilimfanya atake kubadili maisha yake. Kwa upendo, sala, na msaada kutoka familia yake na waumini wa Kanisa, na hatimaye kupitia huruma na rehema na neema ya Bwana, alirudi Kanisani.
Baadaye aliitwa kuhudumia katika misheni ya Washington Seattle. Mwanzoni alisumbuka sana kwa kukata tamaa. Kila usiku kwa miezi mitatu ya kwanza, alienda katika bafu na kulia. Kama Mzee Cowan, alitafuta kuelewa, “Kwa nini nipo hapa?”
Baada ya kuhudumu kwa mwaka mmoja, tulipokea barua pepe ambayo ilikuwa ni jibu kwa sala zetu. Aliandika “Kwa sasa kwa kweli ninahisi upendo wa Mungu na Yesu. Nitafanya kazi kwa nguvu niwe kama manabii wa kale. Ingawa ninapata pia matatizo mengi, kwa kweli nina furaha. Kumtumikia Yesu kweli nidyo kitu bora sana. Hakuna chochote cha ajabu kama hili. Mimi nina furaha.
Alijihisi kama alivyojihisi Alma: “Na Ee, furaha gani, na nuru gani ya ajabu niliyoiona; ndiyo, roho yangu ilijawa na furaha iliyokuwa inazidi maumivu yangu!5
Katika maisha yetu tunapata majaribu, lakini tuna lengo kuu kwa Kristo, tunaweza kulenga kwake na hata kuhisi furaha katikati yao. Mkombozi wetu na mfano muhimu. Alielewa huduma yake takatifu na alikuwa mtiifu kwa mapenzi ya Mungu Baba. Ni baraka kuu jinsi gani kuleta mfano Wake wa ajabu kwenye kumbukumbu zetu kila wiki tunapopokea sakramenti.
Wapendwa ndugu na akina dada, sisi tuna lengo kwa Kristo tunapohudumu kwa uaminifu, kukubali kwa unyenyekuvu, kusali kwa hamasa, na kushiriki kwa kustahili.
Tunaweza kuwa na lengo kuu kwa Kristo tunapokubali shida na majaribu yetu kwa uvumilivu na imani na kupata furaha katika njia yetu ya agano.
Ninashuhudia kwamba Bwana anakujua. Anajua mapambano na mahangaiko yako. Anajua matamanio yako kumhudumia kwa upendo na, ndio, hata lengo. Na awaongoze na kuwabariki mnapofanya hivyo. Katika jina la Yesu Kristo, amina.