“Kaaeni katika Pendo Langu”
Upendo wa Mungu hauna mwisho na utadumu milele, lakini kile inamaanisha kwa kila mmoja wetu hutegemea jinsi tunavyojibu upendo Wake.
Biblia inatuambia kwamba “Mungu ni upendo”1 Yeye ni mfano mkamilifu wa upendo, nasi tunamtegemea sana kwa upendo wake wa daima na wenye kumfikia kila mmoja ulimwenguni kote. Kama Rais Thomas S. Monson alivyoelezea: Upendo wa Mungu uko kwa ajili yako iwe unajisikia au haujisikii kustahili upendo wake. Ni kwamba uko hapo daima.”2
Kuna njia nyingi za kuuelezea na kusema juu ya upendo wa kiungu. Moja ya kauli nyingi tunazozisikia leo ni kwamba upendo wa Mungu “hauna masharti.” Huku hilo likiwa kweli, kielezi hauna masharti hakionekani popote katika maandiko matakatifu. Badala yake, upendo Wake unaelezewa katika maandiko matakatifu kama “upendo mkuu na wa ajabu,”3 “upendo mkamilifu,”4 “upendo wenye kukomboa,”5 na “upendo usio na mwisho.”6 Hizi ni kauli njema kwa sababu neno hauna masharti linaweza kuleta taswira potofu juu ya upendo wa kiuungu, kama vile Mungu huvumilia kila kitu na wala hatuhukumu sisi kwa sababu upendo Wake hauna masharti, au Mungu hafanyi madai yo yote juu yetu kwa sababu upendo Wake hauna masharti, au wote wataokolewa katika ufalme wa mbinguni wa Mungu kwa sababu upendo Wake hauna masharti. Upendo wa Mungu hauna mwisho na utadumu milele, lakini kile inamaanisha kwa kila mmoja wetu hutegemea jinsi tunavyojibu upendo Wake.
Yesu alisema:
“Kama vile Baba alivyonipenda mimi, ndivyo nami niwapendavyo ninyi: dumuni katika pendo langu.
“Kama mtashika amri zangu, mtakaa katika pendo langu, hata kama vile Mimi nilivyo shika amri za Baba, na kukaa katika pendo Lake.”7
“Kuendelea” au “kukaa katika” pendo la Mwokozi maana yake ni kupokea neema Yake na kukamilishwa kwayo.8 Ili kupokea neema Yake, ni lazima sisi tuwe na imani katika Yesu Kristo, na kuweka amri zake pamoja na kutubu dhambi zetu, kubatizwa kwa ajili ya ondoleo la dhambi zetu, tumpokee Roho Mtakatifu, na kuendelea katika njia ya utiifu.9
Mungu daima atatupenda, lakini hawezi kutuokoa katika dhambi zetu.10 Kumbukeni maneno ya Amuleki kwa Zeziromu kwamba Mwokozi hatawaokoa watu Wake katika dhambi zao lakini kutokana na dhambi zao,11 sababu ikiwa ni kwamba tukiwa na dhambi tunakuwa wachafu na “hakuna kitu kilicho kichafu kitakachorithi ufalme wa mbinguni”12 au kukaa katika uwepo wa Mungu. “Na [Kristo] ana uwezo aliopewa kutoka kwa Baba kuwakomboa kutoka kwa dhambi [watu Wake] kwa sababu ya toba; kwa hivyo ametuma malaika wake kutangaza habari njema ya hali ya toba, ambayo inaleta uwezo wa Mkombozi, kuwezesha wokovu wa roho zao.”13
Kutoka katika Kitabu cha Mormoni tunajifunza kwamba kusudi la mateso ya Kristo—ni onyesho kubwa la upendo Wake, lilikuwa “ni kuleta rehema, rehema ambayo huishinda haki na ambayo huifichua njia kwa wanadamu kuwa na imani hata kuweza kutubu.
“Na hivyo rehema yaweza kutosheleza matakwa ya sheria, na kuwazungushia mikono ya usalama, wakati yeye ambaye hatumii imani hata kuweza kutubu anawekwa mbele ya sheria yote yenye kudai haki, kwa hiyo, yeye tu aliye na imani hata kuweza kutubu analetwa kwenye mpango ule mkuu na wa milele wa ukombozi.”14
Toba ndiyo zawadi Yake kwetu, tumenunuliwa kwa thamani kubwa.
Baadhi watabisha na kusema kuwa Mungu huwabariki watu wote bila kutofautisha—wakionyesha, kwa mfano, maelezo ya Yesu katika Mahubiri ya Mlimani: “[Mungu] hufanya jua lake lichomoze kwa waovu na wema , na hupeleka mvua juu ya wenye haki na wasio haki.”15 Ndiyo, Mungu huleta mvua juu ya watoto Wake wote baraka zote ambazo Yeye anaweza—baraka zote ambazo upendo na sheria na haki na rehema zitaruhusu. Na anatuamuru sisi vile vile kuwa wakarimu.
“Ninakuambieni, Wapendeni adui zenu, wabarikini wenye kuwalaani, watendeeni mema wale wawachukiao, na waombeeni wale wawatumiao vibaya, na kuwatesa;
“Ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu wa mbinguni.”16
Hata hivyo, baraka kuu zaidi za Mungu hutolewa juu ya msingi wa utiifu. Rais Russell M. Nelson alielezea: “Baraka za upendo wa Mungu—ikijumuisha uzima wa milele—hujumuisha baraka zile ambazo ni lazima tufuzu na siyo baraka tutegemeazo kupokea hata kama hatustahili. Wenye dhambi hawawezi kupinda mapenzi Yake yafanane na yao, na kumtaka Yeye awabariki wao katika dhambi [ona Alma 11:37]. Kama wanataka kufurahia kila mchanuo wa maua Yake mazuri, lazima watubu.17
Zaidi ya kumfanya kila mtu mwenye kutubu kuwa hana hatia na pasipo doa ikiwa ni pamoja na ahadi ya “kuinuliwa siku ya mwisho,”18 kuna kipengele muhimu cha pili katika kukaa katika upendo wa Mungu. Kukaa katika pendo Lake kutatuwezesha sisi kufikia hatima yetu kamili, hata kuwa kama Yeye alivyo.19 Kama Rais Dieter F. Uchtdorf alivyosema: “Neema ya Mungu haiturejeshi tu kwenye hali yetu ya awali ya kutokuwa na hatia. … shabaha Yake ni ya juu zaidi. Anatutaka sisi wana na mabinti Zake kuwa kama Yeye alivyo.”20
Kukaa katika pendo lake kwa njia hii humaanisha kujiweka chini kikamilifu kwenye mapenzi Yake. Inamaanisha kukubali masahihisho Yake wakati yanapohitajika, “kwani yeye ambaye Bwana humpenda humrudi.”21 Inamaanisha kuhudumiana kama Yesu alivyotupenda na kutuhudumia.22 Inamaanisha kujifunza “kukaa katika sheria ya ufalme wa selestia” ili kwamba tuweze kukaa katika “utukufu wa selestia.”23 Ili Yeye aweze kutufanya tuwe kile tunaweza kuwa, Baba wa Mbinguni anatusihi tukubali ushawishi wa Roho Mtakatifu, na [kumvua] mtu wa kawaida na [kuwa] mtakatifu kupitia upatanisho wa Kristo aliye Bwana, na [kuwa] kama mtoto, mtiifu, mpole, mnyenyekevu, mvumilivu, mwenye upendo tele, aliye tayari kukubali vitu vyote ambavyo Bwana anampatia, hata kama vile mtoto hunyenyekea kwa baba yake.24
Na Mzee Dallin H. Oaks alielezea: “Hukumu ya Mwisho si tu tathmini ya majumuisho ya matendo mema na mabaya—yale t uliyofanya. Ni utambuzi wa athari ya mwisho ya matendo na mawazo—kile ambacho tume2 kuwa.”25
Hadithi ya Helen Keller ni jambo kama fumbo linaloonyesha namna upendo wa kiungu unaweza kubadilisha nafsi iliyo tayari. Helen alizaliwa katika jimbo la Alabama katika Marekani katika mwaka wa 1880. Alipokuwa na umri wa miezi 19 aliugua maradhi yasiyotambulika, ambayo yalimwacha akiwa kiziwi na kipofu. Alikuwa na akili nyingi sana na akawa amechanganyikiwa alipojaribu kutaka kuelewa na kuelwa na mazingira yake. Wakati Helen alipohisi midomo ya mwana familia ikitingishika na kutambua kwamba wao walitumia vinywa vyao kuongea “akakasikrika sana [kwa sababu] yeye hakuweza kuungana nao katika maongezi.”26 Helen alipofika umri wa miaka sita, haja yake kutaka kuwasiliana na mkanganyiko wake ulikua na kuwa mkali sana kiasi kwamba “mpasuko wake ulijitokeza kila siku, wakati mwingine kila saa.”27
Wazazi wa Helen walimwajiri mwalimu kwa ajili ya binti yao, mwanamke aliyeitwa Anna Sullivan. Kama vile tulivyo katika Yesu Kristo anayeelewa, mapungufu yetu,28 Anna Sullivan alikuwa amehangaika na ulemavu na magumu yake mwenyewe, na hivyo akaelewa mapungufu ya Helen. Katika umri wa miaka 5 Anne alipata maambukizi ya maradhi yaliyosababisha maumivu na majeraha ya konea na kumwacha akiwa karibu kipofu. Anne alipotimu umri wa miaka minane, mama yake akafariki; baba yake akamtelekeza yeye na kaka yake mdogo, Jimmie; na wakapelekwa kwenye “nyumba ya watu maskini” mahali ambapo hali ya maisha ilikuwa duni sana kiasi kwamba Jimmie alifariki baada ya miezi mitatu tu. Kupitia kwa jitihada zake pasipo kuchoka, Anne alikubaliwa kuingia katika Shule ya Perkins ya Vipofu na wenye ulemavu wa kuona, ambapo alifanikiwa vizuri kimasomo. Huduma ya Upasuaji ilimpa uoni ulioboreshwa kiasi cha kumwezesha kusoma maandiko ya kupigwa chapa Baba yake Helen Keller alipowasiliana na Shule ya Perkins akitafuta mtu wa kuwa mwalimu wa binti yake, Anna alichaguliwa.29
Halikuwa tukio la kufurahisha mwanzoni. Helen “alimpiga, alimchuna, na kupiga mateke mwalimu wake na kutoa moja ya jino lake. [Anne] hatimaye alipata udhibiti kwa kuondoka pamoja [Helen] na kuishi katika nyumba ndogo kwenye shamba la Keller. Kwa njia ya uvumilivu na mwendelezo thabiti, hatimaye alipata kuaminiwa na kupendwa na mtoto yule.30 Vivyo hivyo, kama tunakuja kuamini kuliko kushindana na Mwalimu wetu mtukufu, Yeye anaweza kufanya kazi nasi ili kutuangaza na kutuinua hadi kwenye uhalisia mpya.31
Ili kumsaidia Helen kujifunza maneno, Anne angeandika herufi moja moja za vitu vinavyofahamika sana kwa vidole vya kiganja cha mkono wa Helen. “[Helen] alifurahia “mchezo huu wa vidole,” lakini hakuwa akielewa hadi pale wakati maarufu [Anne] alipoandika herufi ‘m-a-j-i’ huku akimwaga maji juu ya kiganja cha mkono wake [Helen]. Helen baadaye alaindika:
“‘Ghafla taratibu nikaja kutambua kama kitu fulani ambacho kilionekana kama vile nilikuwa nimekisahau; na kwa namna fulani siri hii ya lugha ilikuwa imefunuliwa kwangu. Nilijua hapo kuwa “m-a-j-i” ilimaanisha kitu hiki kizuri ambacho kinatiririka juu ya mkono wangu. Neno hilo hai liliamsha nafsi, likaipa nuru, tumaini, furaha, likaiweka huru! … Kila kitu kina jina, na kila jina lilizalisha wazo jipya. Tuliporudi nyumbani kila kitu … nilichokigusa kilionekana kujaa uhai.’”32
Kadiri Helen Keller alivyokuwa akikua na kuwa mtu mzima, akaja kujulikana kwa mapenzi yake juu ya lugha, ustadi wake kama mwandishi, na umahiri wake kama mzungumzaji wa umma.
Katika sinema inayoelezea maisha ya Helen Keller, wazazi wake wanaonyeshwa kama watu walioridhika na kazi ya Anna Sullivan baada ya kuwa amemtuliza binti yao mkorofi kiasi cha kumfanya Helen aweze kukaa kwa adabu wakati wa chakula, na kula kawaida, na akakunja kitambaa chake cha mezani mwishoni mwa mlo. Lakini Anne alimjua Helen kuwa na uwezo wa kufanya mengi, mengi zaidi na kwamba alikuwa na mchango mkubwa kufanya.33 Hata hivyo, tunaweza kuridhika sana na kile ambacho tumefanya katika maisha yetu, na kwamba hivyo ndivyo sisi tulivyo tu, wakati Mwokozi anafahamu hatima tukufu ambayo sisi tunaiona tu, “kupitia kioo, kwa mbali.”34 Kila mmoja wetu anaweza kuhisi furaha juu ya hatima takatifu ikijifungua ndani yetu, ni sawa na furaha ile Helen Keller aliyoisikia wakati maneno yalikuwa yenye uhai kwake, yakitoa nuru katika nafsi yake na kuiweka huru. Kila mmoja wetu anaweza kumpenda na kumtumikia Mungu na kuwezeshwa kubariki watu wenzetu. “Kama ilivyoandikwa, Jicho hajapata kuona, wala sikio halijapata kusikia, wala haijapata kuingia moyoni mwa mwanadamu, mambo yale ambayo Mungu amewaandalia wao wampendao.”35
Hebu tutafakari gharama ya upendo wa Mungu wenye thamani. Yesu Kristo amefunua kwamba ili kutulipia dhambi sisi na kutukomboa kutokana na mauti, yote ya kimwili na kiroho, mateso Yake yalimsababishia yeye mwenyewe, “hata Mungu, mkuu kuliko yote kutetemeka kwa sababu ya maumivu, na kutokwa na damu kwenye kila kinyweleo, na kuteseka yote mwili na roho, na kutamani nisinywe kikombe kichungu, na kusita.”36 Mateso yake pale Gethsemani na pale msalabani yalikuwa makubwa sana kuliko yale ambayo mwanadamu katika mwili wenye kufa anayoweza kuvumilia.37 Hata hivyo, kwa sababu ya upendo Wake kwa Baba Yake na kwetu sisi, Yeye alivumilia, na kama matokeo yake, anaweza kutupa sisi yote maisha yasiyo na mwisho na uzima wa milele.
Ni ishara ya kina kwamba “damu [ikaja] kutoka kila kinyweleo”38 wakati Yesu akiteseka katika Gethsemani, mahali pa kisindiko cha mzeituni. Ili kuzalisha mafuta nyakati za Mwokozi, zeituni kwanza zilipondwa kwa kuwekwa jiwe kubwa juu yake. “Rojorojo” iliyofanyika kisha iliwekwa kwenye vikapu vya kusukwa laini, vyenye matundu ambavyo viliwekwa kimoja juu ya kingine. Uzito wa mrundikano huu ulikamua mafuta ya kwanza na safi. Halafu mkamuo ukaongezwa kwa kuwekewa nguzo kubwa au gogo juu ya mrundikano ule wa makapu, na kutoa mafuta mengi zaidi. Mwishoni kabisa, ili kutoa mafuta ya mwisho, nguzo au gogo liliwekewa mawe juu yake kwa upande mmoja ili kuleta mkandamizo na kukamua zaidi.39 Na ndiyo, mafuta ni mekundu kama damu wakati yanatoka.
Ninafikiria juu ya historia iliyoandikwa na Mathayo juu ya Mwokozi wakati akiingia Gethsemane usiku huo wa tukio ya kwamba “akaanza kuwa mwenye huzuni na kulemewa. …
“Na akaenda kitambo kidogo, na akaanguka kifudifudi, na kusali akisema, Ee Baba, kama ikiwezekana kikombe hiki kinipite mbali: yasiwe kama nipendavyo mimi, lakini kama upendavyo wewe.”40
Basi, kama ninavyofikiria wakati uchungu ulipozidi kukua na kuwa mkali zaidi, Yeye alisihi kwa mara ya pili ili apate msaada na, mwishoni, pengine akiwa katika kilele cha mateso Yake, mara ya tatu. Alistahimili maumivu makubwa sana hadi pale haki iliporidhishwa hadi tone la mwisho.41 Hili Yeye alilifanya ili kutukomboa wewe na mimi.
Ni zawadi ya thamani kiasi gani upendo wa kiuungu! Akijawa na upendo, Yesu alisema, “Je mtarudi kwangu sasa, na kutubu dhambi zenu, na kugeuka ili niwaponye?42 Kwa upole Yeye anatuhakikishia, “Tazama, mkono wangu wa rehema umenyoshwa kwenu, na yeyote atakayekuja … nitampokea; na heri ni wao ambao huja kwangu.”43
Je, wewe hutampenda Yeye ambaye alikupenda wewe kwanza?44 Basi shika amri Zake.45 Je, wewe hutakuwa rafiki Yake Yeye aliye utoa uhai Wake kwa ajili ya rafiki Zake?46 Basi shika amri Zake.47 Je, wewe hutakaa katika pendo Lake na kupokea yote anayokupa kwa neema? Basi shika amri Zake.48 Ni maombi yangu kwamba tutakaa kikamilifu katika pendo Lake, katika jina la Yesu Krist, amina.