“Njoo, unifuate” kwa Kufanya Upendo na Huduma ya Kikristo
Kama wafuasi wa Mwokozi katika siku za mwisho, tunakuja kwake kwa kuwapenda na kuwatumikia watoto wa Mungu.
Mshindi wa Tuzo Nobeli Elie Wiesel alikuwa hospitalini baada ya upasuaji wa moyo wakati alipokuwa ametembelewa na mjukuu wake wa umri wa miaka mitano. Kijana huyu mdogo alipokuwa akiangalia kwenye macho ya babu yake, aliona machungu yake. “Babu,” aliuliza, “kama nikikupenda zaidi, maumivu yako yatapungua?”1 Leo nauliza swali hilo hilo kwetu: “Kama tunampenda Mwokozi zaidi, tutateseka kidogo?”
Wakati Mwokozi alipowaita wafuasi Wake waje wamfuate, walikuwa wanaishi sheria ya Musa, ikijumuisha kutafuta “jicho kwa jicho, na jino kwa jino,”2 lakini Mwokozi alikuja kutimiza sheria hiyo kwa kutumia Upatanisho Wake. Alifundisha fundisho jipya: “Mpende adui yako, wabariki wanaowalaani, wafanyie mema wale wanaowachukia, na waombeeni wale wanaowachukia, na kuwatesa.”3
Wafuasi walifundisha kugeuka kutoka kwenye njia za mwanadamu wa kawaida hata kwenye njia za Mwokozi za kupenda na kujali kwa kubadilisha mabishano na msahama, ukarimu, na huruma. Amri mpya “pendaneni”4 haikuwa rahisi kuishika. Wakati wafuasi walikuwa na wasiwasi wa kujihusisha na watenda dhambi na baadhi ya matabaka ya watu, Mwokozi kwa upendo alifundisha, “Kadiri mlivyowatendea hawa kaka zangu mmenifanyia mimi.”5 Au, kama nabii wa Kitabu cha Mormoni alivyoelezea, “Mnapowatumikia wanadamu wenzenu mnamtumikia tu Mungu wenu.”6
Kama wafuasi wa Mwokozi katika siku za mwisho, tunakuja kwake kwa kuwapenda na kuwatumikia watoto wa Mungu. Tunavyofanya hivyo, tunaweza tusiwe na uwezo wa kuepuka matatizo, magonjwa, lakini tutapata maumivu kidogo kiroho. Hata kwenye majaribu tunaweza kupata furaha na amani.
Upendo wa Kikristo na huduma kihalisia huanzia nyumbani. Wazazi, mnaombwa kuwa walimu na wamisionari kwa ajili ya watoto na vijana wenu. Wao ni wachunguzi wetu. Unabeba jukumu la kuwasaidia kuongoka. Ki ukweli, kila mmoja wetu anatafuta kuongoka—ikimaanisha kujazwa na upendo wa Mwokozi.
Kama wafuasi wa Yesu Kristo, upendo Wake unatutia motisha kuhimiliana katika safari hii ya maisha ya duniani. Hatuwezi kufanya hivi peke yetu.7 Ulishaniskia nikishiriki fumbo la Kweka hapo awali: Niinue, Nami nitakuinua, na wote tutapaa pamoja milele.8 Kama wafuasi, tunaanza kufanya hivi tunapobatizwa, tukionesha utayari wetu “kubeba mizigo ya mmoja na ya mwingine, ili iwe miepesi.”9
“Kufundishana mafundisho ya Ufalme”10 ni njia ya kupendana na kutumikiana. Wazazi na kina babu na bibi, tunajaribu kusikitikia hali ya dunia—kwamba shule hazifundishi tabia za maadili. Lakini kuna mengi sisi tunaweza kufanya. Sisi tunaweza kutumia vyema fursa za kufundisha katika familia zetu wenyewe—hiyo inamaanisha sasa hivi. Usidhubutu ziponyoke. Pale fursa inapojitokeza kutoa mawazo yako kuhusu injili na masomo ya maisha, acha kila kitu na kaa chini na zungumza na watoto wako na wajukuu.
Hatupaswi kuwa na wasiwasi kwamba sisi si walimu wa injili waliofunzwa kwa ustadi. Hakuna darasa la mafunzo au kitabu cha kiada kilicho cha msaada kama ulivyo kujifunza maandiko, kusali, kutafakari, na kutafuta mwongozo wa Roho Mtakatifu. Roho itakuongoza kwenda mbele Nawaahidi: mwito wa kuwa mzazi unajumuisha kipawa cha kufundisha katika njia ambayo ni sahihi kwako na watoto wako. Kumbuka, Nguvu ya Mungu kushawishi katika haki ni upendo Wake. “Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza.”11
Vijana, ninyi ni baadhi ya walimu wetu wa injili wenye nguvu. Mnakuja kanisani kujifunza ili kwamba mwende nyumbani kuwafundisha na kuwatumikia familia, majirani, na marafiki zenu. Msiwe na hofu. Kuweni na imani ya kushuhudia kile mnachokijua kuwa ni cha kweli. Fikiria jinsi gani wamisionari wanakua kwa sababu wanaishi maisha ya kujitolea—wakitumia muda na talanta zao na wakishuhudia ili kuwatumikia na kuwabariki wengine. Unaposhiriki ushuhuda wako wa injili, imani yako itakua na kujiamini kwako kutaongezeka!
Baadhi ya huduma zetu za Kikristo zenye athari hutolewa kwa kuwa na mafunzo ya maandiko ya familia, sala ya familia, mikutano ya baraza la familia. Kwa zaidi ya miaka mia moja, viongozi wa Kanisa wametuhimiza tutenge muda usiokatizwa kila wiki. Lakini wengi wetu bado tunakosa baraka hizi. Jioni ya familia nyumbani siyo mhadhara kutoka kwa Mama au Baba Ni muda wa familia wa kushiriki mawazo rahisi ya injili na uzoefu, kuwasaidia watoto wetu wajifunze kujali na kushiriki, kuwa na furaha pamoja, kutoa ushuhuda pamoja, na kukua na kuendelea pamoja. Tunapokuwa na jioni ya familia nyumbani kila wiki, upendo wetu kwa kila mmoja wetu utakuwa imara, na hatutateseka sana.
Na tukumbuke, kazi ya muhimu tunayoifanya katika familia zetu ni kupitia nguvu ya Roho Mtakatifu. Wakati wowote tunapoinua sauti zetu kwa hasira, Roho huondoka kwenye uwepo wetu na familia zetu. Tunapozungumza kwa upendo, Roho anaweza kuwa pamoja na sisi. Na tukumbuke kwamba watoto na wajukuu wetu wanapima upendo wetu kwa jinsi gani tunajitolea katika muda tunaowapa. Juu ya yote, usipoteze subira na usikate tamaa!
Maandiko yanatuambia kwamba wakati baadhi ya roho za Baba yetu wa Mbinguni zilipochagua kutofuata mpango Wake, mbingu zililia.12 Baadhi ya wazazi ambao wamewapenda na kuwafundisha watoto wao pia hulia pale watoto wao wazima wanapoamua kutofuata mpango wa Bwana. Wazazi wanaweza kufanya nini? Hawatuwezi kupuuza haki ya wengine ya kujiamulia. Kumbuka baba wa mwana mpotevu, ambaye alisubiri kwa unyenyekevu ili mtoto wake “ajirudie mwenyewe,” wakati wote akimngojea. Na “alipokuwa angali mbali” alimkimbilia.”13 Tunaweza kuomba mwongozo kuhusu lini tuongee na nini cha kusema, na nyakati zingine, lini tuwe kimya. Kumbuka, watoto wetu na wana familia tayari walichagua kumfuata Mwokozi katika maisha kabla ya hapa. Wakati mwingine ni kwa ajili ya uzoefu wa maisha yao wenyewe ndiyo hisia hizo tukufu huamshwa tena. Mwishowe, uamuzi wa kumpenda na kumfuata Bwana inabidi uwe wao wenyewe.
Kuna njia nyingine maalumu wafuasi huonyesha upendo wao kwa Mwokozi. Leo natoa shukrani zangu kwa wale wote wanamtumikia Bwana kama watunzaji. Jinsi gani Bwana anawapenda! Katika huduma yako ya kimya kimya, unamfuata Yeye ambaye aliahidi, “Baba yenu ambaye huona kwa siri, mwenyewe atawalipa wazi.”14
Namfikiria jirani yangu ambaye mke wake alikuwa na maradhi ya Udhaifu wa akili. Kila Jumapili angemsaidia kuvaa nguo kwa ajili ya mikutano ya Kanisa, akamchana nywele, akamrembesha uso, na kumvisha vipuli. Katika kutoa huduma hii, yeye alikuwa ni mfano kwa kila mwanaume na mwanamke katika kata yetu—hasa kwa dunia. Siku moja mke wake alimwambia, “Ningependa kumwona mme wangu tena na kuwa naye.”
Akajibu, “Mimi ni mme wako.”
Kwa upendo akajibu, “ Aha, vyema!”
Siwezi kuzungumzia kuhusu kutoa huduma bila kutambua mtunzaji maalum katika maisha yangu—mwanafunzi maalum wa Mwokozi. Ametoa yote katika upendo na malezi ya huruma. Mikono yake iliakisi mguso Wake laini, wa kuhimili. Singweza kuwa hapa bila yeye. Na nikiwa naye, nitaweza kuvumilia hadi mwisho na kuwa pamoja naye katika uzima wa milele.
Kama unapata shida peke yako, pamoja na wengine au peke yako, nakusihi umuache Mwokozi awe mtunzaji wako. Egemea kwenye mkono Wake wa maridhawa.15 Kubali hakikisho Lake. “Sitawaacha ninyi yatima: Naja kwenu.”16
Kina kaka na kina dada, kama hatujafanya hivyo kikamilifu hivyo, acha tugeuke zaidi kuelekea msamaha, ukarimu, na upendo. Acha tukatae vita ambavyo vinapamba moto kila mara katika mwanadamu wa kawaida na kutangaza utunzaji, upendo, na amani ya Kristo.17
Kama “kama vile mmefahamu utukufu [wema] wa Mungu”18 na pia “upatanisho ambao ulitayarishwa tangu msingi wa ulimwengu,”19 “hamtataka kuumizana, lakini mtaishi kwa amani. … Na hamtakubali watoto … wavunje sheria za Mungu, na kupigana na kutetanisha moja kwa mwingine. … Lakini nyinyi mtawafunza … kupendana, na kutumikiana.”20
Punde kabla Usulubisho wa Mwokozi, Yeye aliwafundisha Mitume Wake: “Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi”21 na “Mkinipenda, mtazishika amri zangu.”22
Mimi nashuhudia kwamba mkao wa kweli wa Mwokozi juu yetu ni ule mkao wa mikono iliyonyooshwa sana ya sanamu ya Kristasiya Thorvaldsen. Yeye anaendelea kunyoosha mikono Yake zaidi,23 akituita, “Njoo, unifuate.” Tunamfuata Yeye kwa kupendana na kutumikiana na kushika amri Zake.
Natoa ushuhuda wangu maalumu kwamba Yeye yu hai na anatupenda kwa upendo thabiti. Hili ni Kanisa lake Thomas S. Monson ni nabii Wake duniani leo hii. Kwamba tumpende zaidi Baba yetu wa Mbinguni na Mwanawe na tuteseke kidogo ndiyo maombi yangu. Katika jina la Yesu Kristo, Amina.