Njia Sahihi ya Furaha
Nashuhudia juu ya zawadi kubwa ambayo ni mpango wa Baba yetu kwa ajili yetu. Ni njia moja sahihi kuelekea kwenye amani na furaha.
Wapendwa kina kaka na akina dada, wote mliyopo hapa katika Kituo cha Mikutano na ulimwenguni kote, nina shukrani kiasi gani kwa nafasi ya kushiriki mawazo yangu pamoja nanyi asubuhi hii.
Miaka hamsini iliyopita, mwezi Julai 1964, nilipangiwa kazi katika Jiji la New York wakati maonyesho ya ulimwengu yalifanyika kule. Mapema asubuhi moja nilitembelea Banda la Mormoni kwenye maonyesho yale. Niliwasili kabla tu ya kuonyeshwa filamu ya Kanisa Man’s Search for Happines (Usakaji furaha kwa mwanadamu) maonyesho ya mpango wa wokovu ambao unajulikana vyema na Kanisa. Nilikaa karibu na kijana ambaye alikuwa labda ana umri wa miaka 35. Tulizungumzaa kidogo. Hakuwa muumini wa Kanisa letu. Kisha mwanga ulipunguzwa, na maonyesho yakaanza.
Tulisikiliza sauti ya msimuliaji wakati alipouliza maswali ya maana na ya wakati wote: Nilitoka wapi? Kwa nini nipo hapa? Ninakwenda wapi nitakapoyaacha maisha haya?” Masikio yote yalikazwa kusikia majibu, na macho yote yalikazwa kwenye picha zilizoonyeshwa. Maelezo ya maisha kabla ya kuja duniani yalitolewa, pamoja na maelezo ya kusudi letu duniani. Tulishuhudia onyesho la kugusa la kupita kutoka maisha haya ya babu mzee na muungano mtukufu na wapendwa wake waliomtangulia kwenye ulimwengu wa kiroho.
Katika hitimisho la onyesho hili la kupendeza la mpango wa Baba yetu wa Mbinguni kwa ajili yetu, umati kimya kimya ulitoka nje, wengi wakiwa dhahiri wameguswa na ujumbe wa filamu. Kijana mgeni karibu nami hakuinuka. Nilimwuliza kama amefurahia onyesho. Kwa nguvu alijibu: “Huu ni ukweli!”
Mpango wa Baba yetu kwa furaha yetu na wokovu wetu unashirikishwa na wamisionari wetu ulimwenguni kote. Sio wote wanaosikia ujumbe huu mtakatifu wanakubali na kuchagua kuufuata. Kwa hali yoyote ile, wanaume na wanawake kila mahali, kama vile rafiki yangu kijana kwenye maonyesho ya Ulimwengu ya New York, wanatambua ukweli wake, na wanaweka miguu yao kwenye njia ambayo itawaongoza nyumbani salama. Maisha yao yanabadilika milele.
Muhimu katika mpango huu ni Mwokozi wetu,Yesu Kristo. Bila dhabihu Yake ya upatanisho, yote yangepotea. Haitoshi, hata hivyo, kuamini tu katika Yeye na utumishi Wake. Tunahitaji kufanya kazi na kujifunza, kutafuta na kusali, kutubu na kuboreka. Tunahitaji kujua sheria za Mungu na kuziishi. Tunahitaji kupokea ibada Zake za kuokoa. Ni kwa kufanya hivyo tutapata furaha ya milele.
Tumebarikiwa kuwa na ukweli. Tuna wajibu kushiriki ukweli. Wacha tuishi ukweli ili tuweze kustahili vyote ambavyo Baba anavyo kwa ajili yetu. Hafanyi chochote bali ni kwa manufaa yetu. Ametuambia, “Hii ndiyo ni kazi yangu na utukufu wangu—kuleta kutokufa na uzima wa milele wa mwanadamu”1
Kutoka kwenye kina cha moyo wangu, na kwa unyenyekevu wote, ninashuhudia zawadi kubwa ambayo ni mpango wa Baba yetu kwa ajili yetu Ni njia moja kamilifu ya amani na furaha kote hapa na katika ulimwengu ujao.
Kina kaka na dada zangu, nawaachieni upendo wangu na baraka zangu ninapofunga, na ninafanya hivyo katika jina la Mwokozi na Mkombozi wetu, hata Yesu Kristo, amina.